Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
.....384...Huyu adui ujinga na umaskini hachagui dini wala kabila, mikakati tutakayoiweka
kama taifa lazima vile vile sehemu nyingine zenye upungufu wa maendeleo, jambo ambalo sote tunalikubali kuwa ni tatizo
..424...Sisi sote ni watanzania na ni lazima tufaidike na matunda ya uhuru, lakini kama
hujitayarishi kufaidi matunda haya nani atakulazimisha?
.439....Sasa leo mwananchi wa Tanzania anapochukea a leaf, ukurasa mmoja tu katika historia ya Tanganyika na kuifanya ndio utetezi wake kwa waislamu wote, hapo napata wasi wasi wa hatima ya Tanzania na umoja wake.
.444.....Sasa ni juu ya mtoa mada ambaye ni responsible awabebe watanzania wote au awabwage kwa yale anyoyatumikia
.....500..Pale mtakapoelewa kwamba maisha ya mtanzania pamoja na imani yake , ni umoja ,utaifa na maendeleo kwa kwenda mbele.
Mimi nawaona kwa utetezi wenu na hali mliyonayo ninyi ni wadandiaji tu wa mustakabali wa nchi hii.
..504...Wihout other Tanzanians support this issue will just smack on their faces.

UCHAMBUZI WA AMI
...384...
Wewe ni mtu wa porojo tu,nani anasikiliza ushauri wako huko serikalini.Unasema sote tunakubali kuhusu upungufu wa maendeleo sehemu nyengine.Unajua nini kuhusu sehemu za waislamu zilizokuwa na maendeleo halafu nyenzo za maendeleo zikaondoshwa?
...424...
Nani unayemjuwa hataki au hajajitayarisha kufaidi matunda ya uhuru?.Ukweli ni kuwa Nyerere na mtandao wake aliouwacha ndio wanaowanyima watu hasa waislamu kufaidi matunda ya uhuru.
...439...
Hii leaf ni ipi?.Mbona Mohammed Said kaandika volumes kutokana na utafiti wake!.
...444..na ..504....
Hapa hueleweki wakusudia nini,ni kama kwamba unaweweseka.Ukichoka pumzika kwanza.
...500...
Hilo la umoja na utaifa ndilo tunalopenda,lakini kwa sasa hatudanganyiki,kwani umoja na utaifa ni lazima uendane na lengo la kuumbwa kwetu na haki ya kikatiba ya kubaki na dini yetu.
Wadandiaji katika historia ya kupigania uhuru ni nyinyi akina Gwasika,lakini sasa mumeshika na kung'ang'ania udereva.

Tukubaliane sote kuwa huyu jamaa anatatizo la kimsingi.
Kwanza soma vizuri kabla ya kukurupuka mantiki ndani ya ushauri wangu.My pen name is LOLE GWAKISA na si Lole Gwasika! Naweza kujifunza toka maandiko yako kuwa wewe si mtu makini katika masuala ya nchi hii.
Usipoteze muda wako kubadili mada iliyopo mbele yetu, mada ambayo imeshachukua sura mbaya ya udini, historia ya TANU na waanzilishi wake kamwe haiwezi kuchukua sura kuwa ilikuwa ni mapambano kati ya Ukristo na Uislamu.
Na hapo ndio nashangaa akili ya watu wa aina ya AMI na wateteaji wa Udini uliolemea Uislamu kutaka kuredress kitu ambacho ni cha kudhania.
Matatizo ya kimaendeleo yapo na kila mtu anakubali hili, lakini kuweka assumption kuwa Wakristo tu ndio wamefaidika na Uhuru ni ukosefu wa upeo wa kufikiri.
Dont economize your brains capacity ndugu Ami.
Kama unafikiri unaweza kuleta maendeleo kwa waislamu, bila juhudi za Taifa zima , basi you are more than welcome, ingawaje I strongly doubt your means and ways.
Tunapotetea umoja wa kitaifa, hata Mwalimu aliwahi kusema , inabidi uonekane kama mwenda wazimu vile , au kama Padri au Shekhe.Maana matunda yake huyaoni in your life time.
Ami, Mohammed Said,nimesema bila kuwabeba waTanzania wote kwenye mikakati yenu ya the future of your own selves hamfiki mbali sana, you will hoplessly get bogged down in a messy quagmire ya ubaguzi, udini zaidi na mabishano ya nani zaidi katika Uislamu.Haya tunayaona hata leo.
Nyie ndugu zetu, na pengine tunawaelewa zaidi kuliko ninyi mnavyojielewa.
Juhudi, umoja na kodi yangu na yako ndivyo vitakavyo tuwezesha.
 
Historian,Mohamed said,naomba sana unieleze khabar ya Aboud Jumbe,maana naona kama vile huyu naye historia inatishia kumsahau-natanguliza shukurani.
 
Swali kwa bwana Mohamed Said:
1. Hivi huyo Abdulwahid Sykes na wenzake ambao unajitahidi kuwapigia chapuo (ambao karibu wote wewe unasema walikuwa waislamu) ilikuwaje wakazidiwa ujanja na Nyerere ambaye hata jiji alikuwa halijui sawasawa kipindi anatambulishwa Tanu/TAA?

2. Unasema Nyerere kaingia Tanu 1954, sawa, iweje hawa watu waliojenga misingi ya TANU KWA MIAKA YOTE HIYO ya awali wakazidiwa ujanja na mtu mmoja ndani ya mwaka mmoja? (1954-1955)tena unasema walikuwa ni watu wenye akili sana.

Nina mashaka kuwa udini umekutawala sana kiasi kwamba unakuwa na "biasness" kwenye story yako. Mimi nafikiri kuna jambo ambalo wakina Abdulwahid Sykes walishindwa kulifanya ni kuwa uwezo wao katika harakati za kutafuta uhuru uilifika kikomo na Nyerere akawapokea kijiti.

Halafu mbona unaendelea kulia-lia kuwa waislamu wanakandamizwa wakati leo hii waislamu ndio mlioshika hiyo serikali, Rais, Makamu wa Rais etc mnataka mpewe nini ndio mridhike?
 
swali kwa bwana mohamed said:
1. Hivi huyo abdulwahid sykes na wenzake ambao unajitahidi kuwapigia chapuo (ambao karibu wote wewe unasema walikuwa waislamu) ilikuwaje wakazidiwa ujanja na nyerere ambaye hata jiji alikuwa halijui sawasawa kipindi anatambulishwa tanu/taa?

2. Unasema nyerere kaingia tanu 1954, sawa, iweje hawa watu waliojenga misingi ya tanu kwa miaka yote hiyo ya awali wakazidiwa ujanja na mtu mmoja ndani ya mwaka mmoja? (1954-1955)tena unasema walikuwa ni watu wenye akili sana.

Nina mashaka kuwa udini umekutawala sana kiasi kwamba unakuwa na "biasness" kwenye story yako. Mimi nafikiri kuna jambo ambalo wakina abdulwahid sykes walishindwa kulifanya ni kuwa uwezo wao katika harakati za kutafuta uhuru uilifika kikomo na nyerere akawapokea kijiti.

Halafu mbona unaendelea kulia-lia kuwa waislamu wanakandamizwa wakati leo hii waislamu ndio mlioshika hiyo serikali, rais, makamu wa rais etc mnataka mpewe nini ndio mridhike?

wanataka sharia iendeshe nchi. Bila sharia mohamedi said na wenziwe atapambana mpaka tone la mwisho.
 
LG: Ahsante kwa mchango wako na nathamini sana fikra zako kuna mengi unanisomesha na kwa hili siwezi kukutoa shukurani. Tuendelee na mjadala Insha Allah.
 
Deodat: Karibu katika mjadala. Mimi nina kawaida moja ninapoona mwenzangu lugha yake si ya kiungwana basi hujiweka pembeni na kuacha kufanyanae mjadala. Nakuomba uepuke lugha kama "kulialia" ili mjadala ustawi. Hili ni jambo la namna mtu anavyoona jambo na hapana ubaya kutofautiana. Siwezi mimi kukukejeli kwa kuwa tu hujakubaliana nami. Nikifanya hivyo ntakuwa nimetoka katika ustaarabu.
 
SOA: Mzee Jumbe ameandika kitabu "The Partnership" kitafute ukisome.
 
FM: Hapana tusende huko hata kama katika kuchangia mada hii Muislam nitakuwa peke yangu dhidi ya kundi kubwa la Wakristo hiyo si shida kwangu kwa kuwa zinazozungumza ni hoja.
 
FM: Kuwa Waislam ndiyo walioongoza mapambano dhidi ya ukoloni hilo sibadili kauli. Nimelieleza kwa kirefu sana katika kitabu na wametokea watu wakanipinga katika hili kama Fr Smith wa Catholic Church, Dr Kiwanuka wa CCM na wengine wengi. Na kisa cha kukataliwa kuandikwa historia ya kweli na kuja ile ya Chuo cha Kivukoni ni ile hofu ya kuwatukuza Waislam:

In supporting Nyerere for his recent call and taking up the challenge to record a correct history which he had for the first advanced in 1974 and again in 1985 the present author published an article in African Events in which Abdulwahid and other forgotten TANU pioneers received prominence. In that article the author did what no other scholar had done before. He mentioned the fact that Muslims were in the forefront during the struggle for independence. It was at that time taboo to associate Islam or Muslims with the independence movement. The author received sharp rebuke from a Party historian, Dr Mayanja Kiwanuka, a leading member of the panel which wrote the Party book Historia ya Chama Cha TANU 1954-1977, the official history of the Party. The Party historian had this to say:

"(the)... article...argues that although Muslims in Tanzania played a crucial role in the struggle for independence, there is a deliberate effort to downplay their contribution. Consequently, the entire article contains half-baked fairy tales to sustain his argument, more so by mentioning names of several TANU stalwarts who happened to be Muslims...The greatness of TANU, indeed that of its founder-leader, Mwalimu Nyerere, is that, in so short a time since its inception, it managed to weave together into a formidable, relatively homogenous nationalist movement, a people so ethnically, culturally and religiously diverse... Said's major goal is to sow seeds of discord, and at any price, truth to him is a matter to be ignored."

This was the reaction from Kiwanuka, who supervised the research on the official history of the party, reducing a research article to what he called a ‘fairy tale'. The author was also accused of lying. Kiwanuka, not deviating from the Party stand, emphasised ‘the greatness of the party and its founder-leader'. Kiwanuka was at that time the Assistant Secretary in the Department of Political Propaganda and Mass Mobilisation of the Chama Cha Mapinduzi. Kiwanuka had as an undergraduate student at University of Dar es Salaam, written on post-independence Muslim-Christian relations.

In response to the author's interpretation of Tanzania's political history which posits Islam as an ideology of resistance to colonial rule, Fr. Peter Smith, a Catholic priest and a resource person in Muslim-Christian relations, responded with two papers to counter the Muslim factor in the independence movement. In one of them he argues that:

"There are revisionist histories being attempted today which are trying to show these early movements in support of TANU as Islamic Movements. The truth is that Muslims were involved; so, too, were Christians-the movement was mainly nationalistic and the ethos, though not anti-religious, was decidedly secular."

Father Smith of the Roman Catholic Church and the Party seem to be of the same mind on this dissension. Both Kiwanuka and Fr Smith are expressing their own personal opinion, not facts. No one denies the fact that some Christians were there. Indeed Christian names appear in the dramatis personae of the play. But no one can deny the truth that they did not occupy centre stage. This work has given a descriptive analysis of the role of urban Muslims in the struggle for independence; their contribution in the founding of TANU; in membership drives and composition which took strong Muslim characteristics. Dar es Salaam Province TANU Elders Council under its chairman Sheikh Suleiman Takadir had 173 members who were all Muslims.

In response to Kiwanuka's criticism the author published a short biography of Abdulwahid to commemorate twenty years of his death. This was followed by a memorial by the family in the Party and Government papers. This was not to pass without incident. The editor of the Daily News, the government paper, rang up the family late in the night informing them that he would not publish Abdulwahid's memorial the following day until he got permission from Party headquarters in Dodoma. The reason given was that his life history touched important events and personalities in the history of the nation. But somehow the memorial was published in both the Party and government dailies the following morning. Two years earlier in 1986, after a silence of almost twenty-five years, Ally Sykes gave an interview to a British journalist, Paula Park. Park wrote a full page article on the family's political history. When the article was published Ally Sykes received telephone calls from both friends and business associates asking him if he was quoted correctly. Shortly after, Park was quietly asked by immigration officials to leave the country.
 
FUNDI MCHUNDO
.....Tangazo hilo, ingawa lilisema limefuata maagizo ya rais lakini halikuwa la Rais. Ungetaka kuwa sahihi, ungesema tangazo lillilotolewa na Omari muhaji kwa niaba ya Julius Nyerere.
MOHAMMED SAID
.....FM: Ahsane kwa mchango wako. Waziri wa Mambo ya Ndani alikuwa Said Maswanya. Naheshimu fikra zako teundelee na mjadala.
FUNDI FUNDI MCHUNDO
....Kumbe ulikuwa unamjua! Asante kwa kunisahihisha.
Sasa Waziri wa Mambo ya Ndani, Said Maswanya alikuwa mkristu au mkatoliki?
Amandla........

UCHAMBUZI WA AMI
Na wewe iwapo hukuwa na uhakika,kwanini ukamtaja.Huoni kwamba unabahatisha tu.Tutakuamini vipi na maneno yako mengine iwapo si maneno ya kutoka akili mwako tu.
Huoni kwamba unapoteza muda wasomaji bure kujadili kitu ambacho huna elimu nacho ya kutosha!.
 
Mkandara: Ni Abdu ndiye aliyenipeleka tena siku zile alikuwa na Peugeot 504 Station Wagon rangi ya bluu. Hapana hofu jiridhishe na nimefurahi kuwa wewe ni rafiki ya mdogo wangu.
 
FM: Hapana sijigambi hicho nilichokueleza ni kitu kidogo sana nimetoa taarifa kustawisha mjadala na msomaji aelewe mantiki, saikoloji na haiba yangu. Laiti ningetaka kujinasibu ningesema makubwa.
 
Mwalimu Myerere alitaifisha huduma nyingi alizozikuta.
Lakini alifanya hivyo kwa faida ya wengi wasio na msaada wowote katika jamii.
Hata wale aliotaifisha malizao waliendelea kumheshimu kutokana na kuelewa mantiki ya kutaifisha huko.
Huduna za Aga Khan pamoja na zile za Kikristo ni kati ya huduma nyingi zilzotaifishwa ili wengi wpate huduma hizo bila ubaguzi.
Hapa akiwa na HE Prince Sadrudin Aga Khan
701114tanzania.jpg
 
Wakuu wangu Al Saidy,Mohammed Said,Ami,Fundi Mchundo , Mkandara ,Jasusi, Son of Alaska,Chama ,Chuma,KGM,Joka Kuu,Sylver,Pasco,Kiranga,Mag3 na wadau wote wa mjadala huu, nawatakia EID MUBARAK!!! na tuenzi mema yote ya Uislam Insha Allah.
 
MOHAMED said,against all expectations,a rare occurence umeenda many steps further then the four corners of the madras class.For a kariakoo boy you deserve a big salute for this is not usually the norm.Unfortunately you thrive on christian bashing,as if your living depends on this,you is bigger then this-unaleta dharau"eti nawaonea,vitabu vyangu vinapuplishiwa na big publishers,nyundo imepiga msumari,these are mafumbo"s more associated with vikao vya ghahawa.may i ask you kwani haya mambo ya kusoma hayako katika damu?wewe ndio alpha na omega?
Mimi nategemea an academic powerhouse of your stature,kupresent issues in their totality na sio kutupa one sided loops under the guise of udini.UNLIKE elsewhere you should by now have realized that in JF,yuo need more then KISWAHILI to ride the waves
 
Wakuu mjadala uendelee sana tena sana wachovu wa historia ya taifa letu tunapata faida tuliyoikosa madarasani.Wenye akili nzuri tunachuja,tunachambua na hatimae tunatoka na hitimisho zuri.Hakika JF ni kisima cha maarifa makubwa kuliko nilivyofikiri kabla ya kujiunga mwaka 2008.

Mohamed Said,LG,FM,SA,Mkandara,Jasusi na wengine nawapongeza kwa darasa mnaloliendesha hapa jamvini hakika kizazi chetu na kizazi kijacho kitafaidi elimu yenu.
Tumshukuru mwenyezi mungu sayansi na technology imewezekana watu wa kawaida kama sisi na wewe kupeana maarifa haya bila vizuizi wala vipingamiz tena bure bila malipo yoyotei.Tafadhali sana tuepuke lugha ya kuudhi ili mtiririko wa mjadala uende sawa sawa.

Idd mubarak.
 
siku zote nilikuwa najiuliza mbona waasisi wa TAA hawafahamiki na kwa nini? kwa nini nyerere historia inambeba wakati yeye tiyari alikuta watu wanapigania uhuru? so kwa post kama hizi nahisi nitapata jibu
 
Ngongo: Ahsante sana ndugu yangu. Nashukuru kuwa umenufaika na mjadala huu na zaidi nakushukuru kwa kutukumbusha kuwa lugha ambazo si za kiungwana zinaharibu mazungumzo. Toka tumeanza mjadala we ndiyo mchangiaji wa kwanza kutoa tahadhari hiyo na kwa ajili hiyo nakuzawadia kitu hichi hapa chini nakusihi kipokee:

VIPANDE, VIDOKEZO, VIONJO NA DONDOO KATIKA UTAFITI NA UANDISHI WA KITABU MASHUHURI KWAHERI UKOLONI KWAHERI UHURU! KILICHOANDIKWA NA Dkt. HARITH GHASSANY

Na Mohamed Said

Mohamed Omari Mkwawa (Tindo) mwanamapinduzi aliyesahauliwa, mwamasishaji, mpelelezi, mtekelezaji mipango ya upigaji kura Zanzibar 1963, mwanamapinduzi Zanzibar 1964, askari wa msituni wa Afro Shirazi Party, mvushaji askari mamluki wa Kimakonde na makabila mengineo kwenda Zanzibar kupiga kura na kushiriki katika mapinduzi akiwa amekishika kitabu Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! (Hapa ingelikuwa picha ya Mzee Mkwawa lakini nimeshindwa kuiweka)

Utangulizi

Kwa kipindi kirefu historia ya mapinduzi ya Zanzibar ilikuwa ni ile historia rasmi ambayo imeathiri historia nyingi Afrika. Viongozi wa Afrika wanapenda ile historia itakayowakweza na kuwaonyesha wao katika mwanga wa kupendeza. Vinginevyo historia hiyo haitakiwi. Wazalendo wenyewe hawakuwa na hamu ya kuandika historia hii na watu wa nje walioandika historia ya mapinduzi ya Zanzibar hawakupata kuifanyia haki historia ya Zanzibar labda kwa ugeni wao na kwa kuyaamini maelezo yaliyokuwa "wazi" kwa wakati ule, mfano mkubwa ukiwa ni kule kuamini kuwa mapinduzi ya Zanzibar yalipangwa na makomredi wa Umma Party.

Hapajakuwapo udanganyifu mkubwa katika uandishi na utafiti kama huu. Dkt Ghassany amekiweka chano uwanjani bila kawa. Akizungumza na Abdushakur Aboud wa Sauti ya Amerika Dkt Ghassany amesema kuwa historia ya Zanzibar ni historia ya kujijuwa maisha yake akiwa mjukuu wa babu wa mababu Muomani na mabibi wa Kimanyema na Kimwera– mchanganyiko wa damu ya Kiarabu na Kiafrika. Hii kwa hakika ndiyo historia ya wananchi wa Zanzibar. Ni tabu sana kumpata huyo Muarabu Zanzibar kila umuonae Muarabu basi ana mjomba na shangazi Mwafrika. Maadui wa Zanzibar wakiweka mkazo katika ubaguzi wa rangi na kuwafitinisha Wazanzibari. Ukweli huu ndiyo chanzo cha matatizo yote yaliyoikumba Zanzibar toka vyama vya siasa vilipoanza katika miaka 1950 na matatizo yaliyosababisha mauaji ya mwisho yakiwa mwaka 2001.

Mohamed Omari Mkwawa

Mwaka 1995 wakati wa uchaguzi wa kwanza wa vyama vyingi Tanzania nilibahatika kufuatana na mgombea urais wa CUF Prof. Ibrahim Haruna Lipumba katika kampeni za uchaguzi katika mikoa ya Kilimanjaro na Tanga. Prof. Lipumba alifanya mkutano mkubwa sana Tangamano kiasi cha kuishtua CCM. Baada ya mkutano ule Prof. Lipumba na ujumbe wake walialikwa nyumbani kwa mama mmoja akijulikana kama Mama Ummie (sasa ni marehemu) ambako walifanyiwa dhifa kubwa. Kote tukipita mitaa ya Tanga msafara wetu ulikuwa ukishangiliwa kwa nguvu sana. CUF ilikuwa imeingia Tanga kwa kishindo kikubwa.

Mimi kazi yangu ilikuwa kuangalia niliyokuwanayaona na kupiga picha. Kwa hakika nilikuwa nikishuhudia historia ikijiandika. Historia ambayo ilikuwa imeshahibiana sana na ile ya wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika katika miaka 1950. Lakini ninalotaka kusema si hili bali ni picha ambayo niliipiga ndani ya nyumba ya Mama Ummie. Picha hii ilikuwa inamuonyesha mzee mmoja wa makamo aliyevaa fulana ya CUF mbele ikiwa na picha ya Prof. Lipumba. Mzee huyu alikuwa amekaa nyuma ya Prof. Lipumba. Kwa wakati ule picha hii haikuwa na maana yoyote kwangu na hata nilipokuwa naitazama mara kwa mara sura yake si iliyokuwa inanivutia bali ile fulana ya CUF aliyovaa ambayo ilikuwa na picha ya rafiki yangu Prof. Lipumba.

Mungu ana mipango yake. Mihangaiko ya kutafuta riziki yakanihamishia Tanga na nikawa karibu sana na baadhi ya viongozi wa CUF na wanachama wake. Sasa hapa ndipo nilipokujakuonana uso kwa uso na mzee yule kwenye picha yangu niliyoipiga hata kwa wakati ule ilikuwa miaka mingi iliyopita. Jina la huyu mzee wangu ni Mohamed Omar Mkwawa. Ilikuwa katika barza yetu ya kawaida ya kunywa kahawa na kula pweza huku tukijadili historia ya Tanzania ambako siku moja Mzee Mkwawa alinambia, "Mohamed nataka nikuambie kitu. Unajua mimi nimehusika sana katika mapinduzi ya Zanzibar?"

Nilimuangalia Mzee Mkwawa kwa makini. Fikra yangu ya utafiti na uandishi ishashtuka haipo tena usingizini. Mzee Mkwawa aliendelea, "Mimi ndiye niliyekuwa nikiwavusha Wamakonde kutoka Kipumbwi kwenda Zanzibar kuipigia kura ASP na wakati wa mapinduzi mie ndiye niliyewavusha Wamakonde kwenda kuipindua serikali ya Jamshid." Sasa moyo wangu ukaanza kudunda kwa nguvu. Naisemesha nafsi yangu, "Huyu mzee anajua uzito wa maneno haya?" Tuishie hapa. Kuanzia siku ile nikawa sasa namtazama Mzee Mkwawa kwa jicho jingine na heshima yangu kwake ikawa imepanda maradufu. Nilikuwa nimeshatambua kuwa Mzee Mohamed Omari Mkwawa alikuwa mmoja wa wanahistoria waliosahaulika katika historia ya Tanganyika na Zanzibar. Juu ya hayo nilishangazwa na kitu kimoja. Iweje leo huyu mwanamapinduzi wa ASP ambae Abeid Amani Karume alimpa jina la "Tindo" kwa ujasiri wake amekuwa mstari wa mbele CUF chama ambacho kinanasibishwa na Hizbu hasimu mkubwa wa ASP?

Dr Harith Ghassany

Nilikutana na Dr Harith Ghassany mwaka 1999 nyumbani kwake Maskati, Oman. Naikumbuka siku ile kama jana vile. Kanipeleka kwake mwenyeji wangu Farouk Abdulla lakini kabla ya kunipeleka nilikuwa nimeshalisikia jina lake mara nyingi sana pale Maskati kila nikikutana na jamaa wenye asili ya Tanzania jina lake litaibuka. Katika fikra yangu ikanijia kuwa Dkt Ghassany atakuwa ni mtu mzima. Sielewe kwa nini nilipata picha hii. Tulipopiga hodi na akatokea Dkt Ghassany kuja kutufungulia mlango nikapata mshangao mkubwa.

Aliyekuwa mbele yangu alikuwa ni kijana mdogo sana tofauti na nilivyodhani. Kwa njia ya utani hata kabla sijatoa salamu. Nikamgeukia Farouk nikasema, "Ah! Dkt Ghassany, Dkt Ghassany, Dkt mwenyewe ndiye huyu?" Mila na tamaduni za watu wa pwani wakikutana hazipishani. Maskhara ni dalili ya mapenzi. Dkt Ghassany pale pale alipokea yale maskhara na akajibu, "Bwana wangu we wanakutisha bure kwani we ulidhani litakuwa jitu kubwa?" Urafiki na udugu wetu umedumu hadi leo na ndipo katika mazungumzo aliponifahamisha kuwa anataka kuandika historia ya kweli ya mapinduzi ya Zanzibar. Hapo ndipo nilipomjuvya kuhusu Mzee Mkwawa na nikamuomba aje Tanga amuhoji.

Kitu kimoja mashuhuri kwa mashujaa wa harakati za siasa katika Tanzania ni kuwa takriban wote wana hali ngumu sana za maisha. Sikujua vyema hali ya Mzee Mkwawa hadi nilipofika nyumbani kwake na Dkt Ghassany. Utu uzima na udhaifu wa maisha ulikuwa umempiga barabara. Nilimjulisha Dkt Ghassany kwa Mzee Mkwawa na kuwaacha waendelee na maongezi yao. Niliporudi mchana kumchukua Dkt Ghassany rafiki yangu alinambia nimuache nije jioni kumfuata. Niliporudi jioni nilimkuta Dkt Ghassany amechoka na uso umesawijika. Tukiwa ndani ya gari yangu tunaondoka nikamuuliza kulikoni. Dkt Ghassany akanambia maneno ambayo hadi leo yamebaki kichwani mwangu, "Mohamed ufunguo wa kitabu changu anao Mzee Mkwakwa na kama nisingeonana nae utafiti wangu wote wa kabla ungelikuwa hauna maana yoyote."

Dkt Ghassany alikuwa amechukuliwa na Mzee Mkwawa katika safari ya zaidi ya nusu karne. Mzee Mkwawa akimshika mkono kwanza kumpeleka Pemba ambako akiwa kijana wa kiasi cha miaka 25 akifanya kazi ya uashi. Huo ndio ulikuwa wakati wa siasa za ASP na Hizbu zimepamba moto. Mzee Mkwawa alikuwa mmoja wa wachezaji wa ngoma ile hata kama alikuwa anatoka Tanganyika. Dkt Harith akavushwa na kuletwa pwani ya Kipumbwi na Sakura ambako Mzee Mkwawa alikuwa akisimamia kambi ya mafunzo iliyokuwa msituni ya wakata mkonge wengi wao wakiwa Wamakonde, kambi ambayo ilitoa askari waliotumika kuipindua serikali ya Mohamed Shamte 12 Aprili 1964.

Dkt Ghassany hakuwa amejitayarisha kwa haya. Alishangwazwa na uwezo wa kumbukumbu wa Mzee Mkwawa, akitaja majina na mahali na akirudia mazungumzo neno kwa neno kati yake na maofisa wa serikali ya Tanganyika kutoka vyombo vya usalama waliomtia katika operesheni maalum ya kuipindua Zanzibar kutoka Tanganyika. Majina ya Abdulla Kassim Hanga, Jumanne Abdallah, Ali Mwinyi Tambwe, Victor Mkello, Oscar Kambona na wengine yakawa yanadondoka moja baada ya lingine. Taarifa hizi ndizo zilizommaliza Dkt Ghassany na kumsawajisha uso.

Mimi binafsi nilipigwa na butwaa. Nilibaini kama alivyobaini Dkt Ghassany kuwa Mzee Mkwawa alikuwa hazina na tulikuwa tumevumbua mgodi wa dhahabu. Kazi yetu sasa ilikuwa kuchimba tu. Kumekuwa na uvumi kwa miaka mingi katika duru za wanasiasa wapya na wa zamani na katika wanafunzi wa historia ya Tanzania na Mapinduzi ya Zanzibar kuwa Ali Mwinyi Tambwe alihusika sana katika kupinduliwa kwa serikali ya Zanzibar lakini hakuna aliyejuwa ni kwa kiwango gani na alihusika vipi. Lakini zito ni kuwa yeye mwenyewe akiudhika sana mtu akimuuliza habari zile. Kwa nini ilikuwa hivyo? Kitabu cha Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru cha Dkt Ghassany kilikuja kutoa majibu. Hakuna binadamu apendae historia yake ihusishwe na mauaji na dhulma na kufutwa kwa nchi yake.

Kwa kipindi cha takriban miaka saba Dkt Ghassany alikuwa akija Tanga kwa mahojiano na Mzee Mkwawa na katika kipindi hicho Mzee Mkwawa alitupeleka Kipumbwi na Sakura na kutuonyesha sehemu zile ambazo walikuwa na kambi na wakifanya mazoezi ya kivita na matumizi ya silaha. Mkahawa ambao wale wakata mkonge walikuwa wakila chakula cha usiku kabla ya kuvushwa kwa vyombo vya bahari kwenda Unguja bado upo hadi leo ingawa kwa sasa kijumba kile hakitumiki tena kama mkawaha. Endapo itakuja siku serikali ya Zanzibar itataka kuhifadhi historia ya Mapinduzi ya Zanzibar bila shaka moja ya vitu vitakavyokuwa katika makumbusho ni picha ya hicho kibanda.

Victor Mkello

Kipumbwi haijabadilika iko kama vilevile iliyokuwa miaka ya 1960. Kipumbwi imebaki vilevile kama kijiji cha uvuvi. Mzee Mkwawa alitupeleka hadi sehemu ambapo bahari imeingia katika kijiji lakini sehemu hiyo imefunikwa na mikoko mingi na vichaka. Tuliingia ndani na kuangalia mandhari ya pale mahali. Hakika pale palikuwa sehemu nzuri ya kujificha. Leo imekuwa sehemu hii ni maarufu kwa watu wa magendo. Mzee Mkwawa alitueleza kuwa hapo ndipo walipojificha na ndipo walipopandia vyombo vyao kwa usiri mkubwa wakati wote wakiwa wamevaa nguo matambara na kofia za makuti kama wavuvi. Tanga ilikuwa kituo muhimu cha kufanikisha mapinduzi ya Zanzibar. Haikuwa bure kuwa Ali Mwinyi Tambwe, Jumanne Abdallah na Victor Mkello walikuwa hapo na wala haistaajabishi kwa Dkt Ghassany kutueleza kuwa vinara wa mapinduzi kwa upande wa bara, Mkello na wenzake, walisubiri taarifa za mapinduzi katika mkesha ndani ya ofisi ya TANU Tanga.

Napenda kukiri kuwa sikupata kushiriki kama msikilizaji wa mahojiano wakati wa utafiti wa Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru. Kazi yangu kubwa sana ilikuwa kufungua milango na kumwendesha daktari. Kwa ufupi kazi yangu ilikuwa kumwekea mwandishi mazingira mazuri ili kazi yake iwe nyepesi. Kwa hakika ilikuwa kazi ambayo na mimi vilevile nilisoma, kujifunza mengi na kupata faida kubwa. Katika haya nakumbuka sakata la kumtafuta Victor Mkello. Leo si wengi wanaomjua Victor Mkello au hata kupata kusikia jina lake likitajwa. Lakini kwa sisi tuliokuwa wadogo tukiwa shule katika miaka ya 1960 Mkello alikuwa hapungia katika magazeti ya Ngurumo na Mwafrika. Mzee Mkwawa ndiye aliyetusaidia kumtafuta alipo. Victor Mkello ndiyo aliyekuwa "Amiri Jeshi Mkuu" wa lile jeshi la Wamakonde lililokuwa na makao yake makuu katika mashamba ya mkonge ya Sakura na Kipumbwi. Bila ya kupata kauli ya Mkello kitabu kisingeweza kuandikika.

Ilichukua muda kuweza kumpata. Kwanza tulikwenda Muheza ambako ndiko kwao. Huko tukaambiwa kuwa hakuwapo hapo bali kwa muda mrefu alikuwa Tanga. Mwishowe tulimkuta nyumbani kwake Nguvu Mali. Mkello alikuwa katika kitanda cha mauti. Kisukari kilikuwa kikimla kiwiliwili chake. Hakuwa anaweza kunyanyuka kitandani wala kukaa. Kwa hakika alikuwa anasikitisha. Huyu hakuwa Victor Mkello niliyekuwa namsoma katika magazeti wala yule ambae Mzee Mkwawa alikuwa akituelezea. Mtu mjanja aliepambana na Magiriki wamiliki wa mashamba ya mkonge akitetea haki za Waafrika katika miaka ya 1960. Huyu kwa kweli hakuwa yule Victor Mkello aliyekuwa akisaidiana na TANU na Mwalimu Julius Nyerere kupigania uhuru wa Tanganyika. Hiki mbele yetu kilikuwa kivuli chake. Hapakuwa na wasiwasi wowote Victor Mkello alikuwa akisubiri malaika wa mauti amtembelee na yeye hilo alikuwa akilijua fika.

Victor Mkello na Mzee Mkwawa wanamapinduzi waliofutwa katika historia walitazamana na wakasalimiana kama vile hakuwapata kujuana. Jicho la Mkello lilikwenda kwa Dkt Ghassany kisha likaangukia kwangu kisha likarudi kwa mwanamapinduzi mwenzake Mzee Mkwawa. Baada ya utambulisho uliofanywa na Mzee Mkwawa nilihisi woga na wasiwasi kwenye sura ya Victor Mkello. Hakuwa anaamini kuwa Dkt Ghassany katoka Maskati kwa ajili ya utafiti wa historia na hili lilijidhihirisha alipofunua kinywa kuzungumza. Victor Mkello alikuwa na hisia kuwa alifuatwa kukamatwa kwa vifo vya Waarabu vilivyotokea Zanzibar wakati wa mapinduzi ili apelekwe Mahakama ya Kimataifa. Baadae Dkt Ghassany alinifahamisha kuwa jinsi Waingereza walivyomueleza katika taarifa zao za siri ambazo yeye alizisoma London zimeafikiana kabisa na jinsi alivyomuona pale. Waingereza walimsifia Mkello kwa kusema kuwa alikuwa bingwa wa kuteleza kama samaki ndani ya maji.

Kufupisha maelezo. Ilichukua karibu miaka mitatu kwa Victor Mkello kukubali kuzungumza kuhusu mapinduzi ya Zanzibar. Dkt Ghassany akienda Maskati na kurudi Tanga na kila akienda kwa Victor Mkello, Mkello hakuwa tayari kueleza kile alichokijua kuhusu mapinduzi ya Zanzibar. Kila nilipokwenda na Dkt Ghassany kumuona Mkello hali yake ilikuwa inazidi kudidimia. Sasa alikuwa kakatwa mguu mmoja kwa ajili ya kisukari. Ilikuwa katika hali ile katika siku zake za mwisho ndipo siku moja alipomwambia Dkt Ghassany aje siku ya pili na yeye atazungumza na angependa azungumze mbele ya mkewe ili amkumbushe pale atakapokuwa kasahau kitu.

Hapa ndipo ilipo moja ya sehemu tamu kabisa ya kitabu hiki Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru. Victor Mkello Amiri Jeshi Mkuu wa Mamluki wa Kimakonde alizungumza. Mimi sikushiriki katika mazungumzo yale nilijiweka pembeni ili Mkello azungumze na Dkt Ghassany kwa utulivu. Nilikuwa nimeegesha gari yangu karibu ya msikiti jirani ya nyumba ya Mkello nikimsubiri daktari akamilishe upasuaje mgonjwa apate nafuu. Mwendo wa Dkt Ghassany wa kudunda alipokuwa ananijia pale nilipoegesha gari ulidhihirisha furaha yake.

Haukupita muda mrefu baada ya mazungumzo yale na Dkt Ghassany, Victor Mkello akaaga dunia kimya kimya. Hakuna mtu aliyejua kifo chake kama ilivyokuwa vifo vingi vya mashujaa waliopigania uhuru wa Tanganyika. Hakuna hata gazeti moja lililotoa taazia yake wala hotuba hazikusomwa kaburini kwake. Mkello aliondoka katika historia ya Tanzania kimya kama jinsi mamluki wake walivyokuwa wakiingia Zanzibar kimya kimya usiku mkuu na kwa siri, mapanga yao makali ya kukata mkonge yakiwa chini ya nguo zao za ndani yakisubiri kuivamia Zanzibar na kuua watu wasio na hatia. Kazi hii kwao haikuhitaji mafunzo kwani mafunzo walikuwanayo muda mrefu katika kazi yao ya kukata mkonge katika mashamba ya mkonge ya Tanga. Pigo moja lilitosha kuangusha chini jani zito la mkonge seuze kiungo cha binadamu.

Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru ni kitabu kilichoandikwa kwa staili ya pekee wahusika wenyewe wa matokeo katika mapinduzi kujitolea kueleza kile kilichotokea katika mapinduzi, kabla na baada yake. Kuanzia mipango ya kuangusha serikali ya Zanzibar hadi katika kuwaua wale waliokujakushukiwa kuwa ni maadui wa mapinduzi hadi kufikia hata kuweka wazi jinsi walivyoshiriki katika mengi ya kusikitisha kupelekea hata msomaji kujiuliza kwa nini hawa watu baada ya miaka yote hiyo kupita wameamua kueleza yote hayo. Vipi Abdallah Kassim Hanga, Othman Shariff, Mdungi Ussi, Jaha Ubwa, Abdulaziz Twala na wengineo walivyouliwa, nani alitoa amri ya mauaji, nani aliwauwa na katika mazingira gani. Kifo cha Karume mwenyewe kwa mtutu wa bunduki hakikuwekewa pazia na chanzo cha kuamuliwa kuwa auawe ni tofauti ya kilichozoeleka kuelezwa. Karume hakuuawa na "wapinga mapinduzi" kama ilivyozoeleka kuelezwa katika historia rasmi.

Kwa kumaliza tusubiri mapitio ya kitabu hiki na ni wazi kuwa wasomaji watapata mengi ya kuelimisha na kuhuisha. Tunategemea wasomi wa somo la historia watakaopitia kitabu hiki watatufanyia hisani kubwa kwa kuwaleta katika picha wahusika wakuu wa mapinduzi – Mwalimu Julius Nyerere – fundi mkuu mwenye kishindo kikubwa lakini hakisikiki, mkono wake wa chuma hauonekani, uso wake nyuma ya pazia, Abdallah Kassim Hanga – kiongozi hasa na mpangaji wa mapinduzi, Victor Mkello – mtumishi wa Hanga na Nyerere bila ya yeye mwenyewe kujua kati ya hao wawili nani aliyekuwa bingwa kumshinda mwenzake katika mchezo mchafu wa siasa ya kuiuwa Zanzibar na Wazanzibari na wengineo.

Lakini juu ya hayo yote mipango hii ilikuwa ni ya akina Nyerere, Hanga na Mkello pekee? Dkt Ghassany anaeleza nini kuhusu mkono wa Waingereza, Algeria, Misri, Wachina, Warusi, Marekani na Mayahudi? Nini kilichowasukuma hao wote katika mapinduzi ya Zanzibar? Nini kilimsukuma Nyerere, kuwapindua Waislam walioupigania Uhuru wa Tanganyika na baadae kuwapinduwa Waislam walioupigania Uhuru wa Zanzibar na kuendelea kuwadhibiti hata baada ya kuipindua Zanzibar? Nini kilichowasukuma Waingereza na Wamerekani kuachia mapinduzi yafanyike? Lakini kubwa zaidi kipi kilichowasukuma Wayahudi kuingia na kusaidia mapinduzi, ni ile chuki yao ya asili dhidi ya Waarabu au kulikuwa na jengine ambalo liliwatia khofu? Na kwanini kitabu kiitwe Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru: Zanzibar na Mapinduzi ya Afrabia? Kitabu kina majibu ya haya maswali mengine ambayo bado hayajaulizwa na chemchemu mpya za utafiti.

Dkt Ghassany anastahili pongezi kubwa sana kwa kuinusuru historia ya mapinduzi ya Zanzibar na kuwaamsha Wazanzibari na Watanganyika toka lepe zito la usingizi ili wajitambue na wamjue adui yao. Anastahiki pongezi kubwa zaidi si kwa kukiandika kitabu cha Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru bali kwa kutumia mrengo usiokuwa na mrengo. Huna pa kumuweka Dkt Ghassany na baada ya kumaliza kukisoma kitabu ukaridhika napo. Kama utafikiria kuwa kitabu ni cha CUF basi baada ya kusoma mpaka mwisho utavunjika moyo. Kama utamtumbukiza ndani ya CCM basi ataelea. La kama unataka upae nje ya masunduku na mapakacha basi utamuona katulia ndani ya uhuisho wa umoja wa Zanzibar na Tanganyika Mpya – Tanzania Mpya.

Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru ni ngoma nzito ambayo watu wameanza kuicheza hata mdundo haujaanza kupigwa! Tayari imeshaingia katika rikodi za Hansard za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Tayari imeshasikika katika Sauti ya Marekani. Tayari daktari anafuatilia kwa karibu ukweli wa Maridhiano na kuwa kwa mara nyengine tena ukweli wake umeshaanza kupotoshwa na waroho na tayari historia mpya na kubwa zaidi hata kuliko ile ya Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964 imeshaanza kuvurugwa.

Watengenezaji wa filamu Hollywood wana mtindo wa kumaliza senema zao za matokeo ya kweli kwa kueleza katika maandishi yale yaliyowafika wahusika wa kisa kilichotengenezwa hiyo senema. Huonyesha majina na mwisho wa hao wahusika, kama wahai, wako wapi, wamekufa na kama wamekufa ni kwa kuuliwa au kwa amri ya Mungu nk. Katika Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru majina ya wahusika machache ambayo yametajwa katika makala haya yako kama hivi:

1. Mohamed Omar Mkwawa: Yu hai na anaishi Makorola Tanga
2. Abeid Amani Karume: Ameuawa 1972
3. Abdallah Kassim Hanga: Ameuawa 1967/68
4. Mustafa Songambele Yuhai anaishi Songea.
5. Victor Mkello Amekufa kifo cha kawaida
6. Ali Mwinyi Tambwe Baada ya mapinduzi alikuja kuhusika katika mchakato wa kuunda muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Amekufa kifo cha kawaida.
7. Jumanne Abdallah Alitumikia serikali kwa muda mrefu hadi alipofariki kifo cha kawaida
8. Oscar Kambona Aligombana na Nyerere na akakimbia nchi mwaka 1967 na kwenda kuishi uhamishoni Uingereza
9. Kuna vigogo kadhaa ambavyo viko hai na kwa sasa wameomba majina yao yahifadhiwe.

17 Ramadhani 1431
28 August 2010
 
Mnyikungu: Ni katika maajabu ya Mungu kuwa watu wakubwa wanatishwa na vitu vidogo sana. Inabidi mtu atafakari sana. Nyerere akitishika sana na historia ya kudai uhuru wa Tanganyika. Alitaka sana ianze na yeye na katika uhai wake wote alitumia kila juhudi kuififilisha historia ya kweli. Bahati mbaya hakujua kuwa Mungu hana khiyana si katika sifa zake yeye ni hakimu muadilifu. Kila mtu humpa haki anayostahili. Historia ya kudai uhuru wa Tanganyika imeandikwa akiwa hai na alipoisoma na baada ya kuwekewa shinikizo na baadhi ya watu wake wa karibu walimudu kumshawishi na akakubali kueleza upande wake wa historia hiyo. (Juzi nimepewa kitabu "Farewell to the President" kinachomuhusu marehemu Prof. Haroub Othman. Ndani imeelezwa kuwa kazi ya kuandika maisha ya Nyerere alipewa Prof. Haroub). Wakati kwa bahati mbaya ulikuwa umemtupa mkono Mwalimu. Hakuwahi kuifanya kazi hiyo kwa msaada wa Prof. Haroub na wataalam wengine. Historia ile ile aliyoitaka ndiyo hiyo hiyo Mungu aliyomhitimishanayo huku akijua historia aliyokuwa akiiogopa sasa ni mashuhuri. Hili ni funzo kubwa kwa siye tuliobaki nyuma. Inabidi tutafakari sana kwa kila tulifanyalo.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom