Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
SOA: Samahani ndugu yangu. Hayo maneno niliyosema ni maneno ya Kiswahili ambayo kwa hakika ndiyo khasa lugha yangu kwa zaidi maana mimi sijui "vernecular" moja ya misiba ya kuzaliwa na kukulia mjini. Hakika vikao vya kahawa ni mjoa wa utamaduni wetu sisi watu wa pwani ila katika viako hivyo hapana lugha chafu. Hili ningependa ulielewe. Ikiwa misemo hiyo umehisi ni kinyume cha uungwana nakutaka radhi sana ndugu yangu. Ama hili la kazi yangu kueleza kuwa zimechapwa na wachapaji maarufu nia ni kuwaridhisha wanaonisoma wanichukulie kwa uzito unaostahili wasiipuuze haya nisemayo. Kuhusu lugha ya Kiingereza uliposema nahitaji ujuzi wa lugha nyingine mimi sikimudu sana kwa hiyo naogopa kujitia katika ujuzi nisioumudu. Mtume wetu (SAW) katufunza anasema: "Arehemewe yule anaejua mwisho wa uwezo wake."