Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
Again unaweka issues za Wazanzibar hapa kuchanganya wasomaji..kwanini hukakamai ktk mada husika. Ukiona issue za Wazanzibar basi weka Thread ingine tujadili. Still hoja zako zajibika, ila nachelea kwenda nje ya mada ya sasa ya Tanganyika.
 
Lole naona unaanza kuharibu Mada Makusudi. ..Issue ya CUF imeingiaje hapa?...au Pombe zishakujaa Kichwani?
 
Mohammed Said kama mwanahistoria..alikuwa anafanya kazi ya kihistoria....ya Kuchukua Picha za kumbukumbu hata za Chadema/CCM anazo...!!!
Kitabu cha Mohammed Said kimetoka kabla hata ya Vyama Vingi....Hilo la CUF kutoa baraka limetoka wapi?..au yeye kama yeye asishiriki mikutano ya wanasiasa?

Kitabu cha Mohammed Said Kimetoka Nyerere yu Hai...
 
Na Nyerere alisema 'hakuna atakayemwamini." Mjadala kwisha!
 
Lole naona unaanza kuharibu Mada Makusudi. ..Issue ya CUF imeingiaje hapa?...au Pombe zishakujaa Kichwani?

Maalim Chuma usiharibu siku zangu za mfungo sindikiza, sijanywa pombe wala nini , na nasherehekea Eid kama waTanzania wengine.
Mohammed Said na CUF naona wana shabihiana kwa maono.Fununu imejitokeza katika andiko lake mwenyewe Mohammed Said.
 
Mohammed Said ni jipu la kutokea tu huo udini mkuu wangu.U
dini haukuanza leo wala jana.Na CUF ni fertile breeding grounds za political leanings za huo udini.
Na ndio maana wanajaribu kujipatia credit kuwa waislamu ndio walioleta uhuru nchi hii.Mwalimu yeye alipewa tu uenyekiti.
Sasa nina post kwa MARA YA TATU ushahidi wa Prof Mhina ili uende kitandani ukalale na urudi na jibu la udini huu.

Lole Gwakisa(post441)
Paper: Religions and Challenges of Development in Tanzania; Firefighters and Arsonists.
By: Dr. Amos Mhina, Associate Professor, Department of Political Science and Public Administration, University of Dar Es Salaam, Tanzania/ Visiting Scholar, Carleton University, Ottawa.​

Some Muslim groups were in a collision course with the coming nationalist government even before independence. As TANU and Nyerere were on course to independence in the late 1950s many Muslims supported the nationalist movement. There were however some conservative coastal Muslims who opposed TANU. According to Illife the most serious dissent came from the All Muslim National Union of Tanganyika (AMNUT) mostly based in Dar Es Salaam. In August 1959 its leaders went to the extent of proposing that Independence be delayed until Muslims achieved educational equality with Christians. (Illife 1979 pp.551-52). The nationalist party was able to calm moderate Muslims by promising to deal with the disparity after Independence.

Sasa jibu hoja kwa hoja mkuu wangu Chuma, udini ulianza hata kabla ya uhuru, kwa leo CUF ni mlezi tu wa mawazo hayo.
 
Maalim Chuma usiharibu siku zangu za mfungo sindikiza, sijanywa pombe wala nini , na nasherehekea Eid kama waTanzania wengine.
Mohammed Said na CUF naona wana shabihiana kwa maono.Fununu imejitokeza katika andiko lake mwenyewe Mohammed Said.

Wanaukumbi Wote: Hii mada ya CUF ni nzuri sana na mimi namshukuru Mungu kwa kunijaalia kuwa mmoja wa vijana (wakati ule) wa Kiislam ambao walikubali kuwa masikini lakini Uislam na Waislam wapate heshima inayostahili. Hili silionei aibu lakini kwa sasa hii mada ya CUF tuiweke pembeni tutaizungumza kwa marefu na mapana yake Insha Allah. Naamini ukumbi utastawi kwani nina mengi ambayo wengi hamyajui. Hii ndiyo ya faida ya kufanya mahojiano kiungwana. Kwa sasa tuzungumze historia ya Tanganyika hadi tuihitimishe Insha Allah.
 
LG: Hili lingekuwa la maana sana kama ungemfahamisha Prof.Mhina kuwa Mohamed Said kasema kadha wa kadha sasa nakuomba uingie ukumbini umjibu. Kutumia paper ya Prof. Mhina kunijibu sidhani kama itanogesha mjadala. Natoa changamoto kwa wanaukumbi kwa ujumla tafadhalini mtafuteni Prof. Mhina popote alipo kama mnamfahamu aje Insha Allah na yeye achangie sote tunufaike.
 
Maalim Chuma usiharibu siku zangu za mfungo sindikiza, sijanywa pombe wala nini , na nasherehekea Eid kama waTanzania wengine.
Mohammed Said na CUF naona wana shabihiana kwa maono.Fununu imejitokeza katika andiko lake mwenyewe Mohammed Said.

Hili la CUF Insha Allah nimelieleza Insha Allah tutastarehe wakati ukifika na wanaukumbi wahakikishe kuwa wana bytes za kutosha zisiwakatikie katikati na usiku maduka yamefungwa.
 
Na Nyerere alisema 'hakuna atakayemwamini." Mjadala kwisha!

Hii historia niliyoandika ni maarufu sana hasa katika jamii za Kiislam kwa kuwa imetoa majibu ya maswali mengi hususan kwa vijana waliozaliwa baada ya uhuru. Napata mialiko mingi katika vyuo na shule za Kiislam kuzungumza kiasi kwamba inaniwia taabu sana kuweza kukidhi mialiko yote.

Kuna kijana sasa hivi ni mwalimu wa historia katika moja ya vyuo vikuu vyetu hapa nchini wakati anaandika tasnifu yake uzamili alikujanihoji. Hivi karibuni nilikuwa mjini kwake akanialika chakula cha mchana nyumbani kwake. Katika mazungumzo yake akanambia kuwa katika darasa lake la historia huwa anafundisha historia rasmi na inapobaki "lecture" kama mbili hivi huwasomesha hii niliyoandika mimi. Anasema hali ya hewa katika darasa inakuwa kama imetiwa umeme wanafunzi wanakuwa wametulia tuli kama wako kwa kinyozi wananyolewa. Akanieleza kuwa wanafunzi wake wanapendezewa sana na historia hii yangu kuliko ile rasmi. Huyu kijana kitu kizuri ni kuwa sio Musilam. Dunia ndivyo ilivyo watu hamuwezi kukubaliana katika kila jambo. Nyerere aliamini kuwa mimi nitaitwa muongo na kweli kuna watu hawaniamini lakini kwa upande mwingine kuna watu hivi sasa wamemgeuka kiasi wanamwita Baba wa Kanisa.
 
Na Nyerere alisema 'hakuna atakayemwamini." Mjadala kwisha!

Jasusi: Hili nimeshalitolea jibu.

Kuna kijana sasa hivi ni mwalimu wa historia katika moja ya vyuo vikuu vyetu hapa nchini wakati anaandika tasnifu yake uzamili alikujanihoji. Hivi karibuni nilikuwa mjini kwake akanialika chakula cha mchana nyumbani kwake. Katika mazungumzo yake akanambia kuwa katika darasa lake la historia huwa anafundisha historia rasmi na inapobaki "lecture" kama mbili hivi huwasomesha hii niliyoandika mimi. Anasema hali ya hewa katika darasa inakuwa kama imetiwa umeme wanafunzi wanakuwa wametulia tuli kama wako kwa kinyozi wananyolewa. Akanieleza kuwa wanafunzi wake wanapendezewa sana na historia hii yangu kuliko ile rasmi. Huyu kijana kitu kizuri ni kuwa sio Musilam. Dunia ndivyo ilivyo watu hamuwezi kukubaliana katika kila jambo. Nyerere aliamini kuwa mimi nitaitwa muongo na kweli kuna watu hawaniamini lakini kwa upande mwingine kuna watu hivi sasa wamemgeuka kiasi wanamwita Baba wa Kanisa.
 
Maalim Chuma usiharibu siku zangu za mfungo sindikiza, sijanywa pombe wala nini , na nasherehekea Eid kama waTanzania wengine.
Mohammed Said na CUF naona wana shabihiana kwa maono.Fununu imejitokeza katika andiko lake mwenyewe Mohammed Said.

Hili nishalitolea jibu:

Wanaukumbi Wote: Hii mada ya CUF ni nzuri sana na mimi namshukuru Mungu kwa kunijaalia kuwa mmoja wa vijana (wakati ule) wa Kiislam ambao walikubali kuwa masikini lakini Uislam na Waislam wapate heshima inayostahili. Hili silionei aibu lakini kwa sasa hii mada ya CUF tuiweke pembeni tutaizungumza kwa marefu na mapana yake Insha Allah. Naamini ukumbi utastawi kwani nina mengi ambayo wengi hamyajui. Hii ndiyo ya faida ya kufanya mahojiano kiungwana. Kwa sasa tuzungumze historia ya Tanganyika hadi tuihitimishe Insha Allah.
 
Kiufupi lengo la Mohammed au Waislam si kuwachukiwa wakristo kama unavyotaka kuweka. lengo ni kuwa wazi historia ya Tanganyika. lkn Pia any imbalances zisiwepo kwa wachache kujiona wao ndio wenye Mamlaka na kuwadhulumu wengine.

1. Nyerere Kumpisha Muislam eti haitoshi...? kampisha? au ....!!!
2. Mkapa kawapa chuo waislam...Haitoshi..?..kwani wakristo kawapa Vingapi?
3. Kikweke ameteua waislam wengi..? wangapi? hao wachache tu waliochaguliwa mnamuona JK mdini...!!! kwani mlishazoea mfumo wa nyinyi kuwa wengi ktk Serikali, wawili/watatu kwenu wengi...!!!

Waislam wanataka HAKI Itendeke.
 
LG: Waswahili tuna msemo akutukanae hakuchgulii tusi. Bahati mbaya hunifahamu. Mimi si mtu wa kupewa... kama ulivyosema. Wewe huijui historia ya wazee wangu soma hapo chini:

Babu yangu Salum Abdallah alishiriki mgomo wa kwanza wa mwaka 1947 akiwa kiongozi. 1953 akiwa mwanachama wa TAA Tabora alitoa fedha nyingi sana kumwezesha Germano Pacha (mmoja wa wale 17waliaoasisi TANU) kusafiri Dar es Salaam kuja kuhudhuria mkutano ule. Akina George Magembe walikimbia harakati zile na hawakutaka kujihusisha na watu kama Salum Abdallah wakiogopa serikali ya Muingereza. Mwaka 1955 alikuwa Mwenyekiti wa kwanza wa Tanganyika Railway African Union. 1960 aliongoza mgomo wa kihistoria uliodumu siku 82. Mwaka 1964 akiwekwa kizuizini kwa shutuma za kupanga njama za kupindua serikali ya Nyerere. Sisi hatuna historia ya kulamba viatu vya madhalimu wala kujipendekeza kwa wakubwa. Mohamed Said anatoka katika mifupa ya watu hawa.
 
Kumbe kuandika kwako koote ilikuwa kutaka kuuthibitishia umma wa Watanganyika kuwa JKN ni Baba wa Kanisa................naendelea kuungana na wanaJF wanao sema maandishi yako yana msukumo mkubwa sana wa udini..............hence uchochezi
 
Hili la CUF Insha Allah nimelieleza Insha Allah tutastarehe wakati ukifika na wanaukumbi wahakikishe kuwa wana bytes za kutosha zisiwakatikie katikati na usiku maduka yamefungwa.

Shekhe Mohammed...ni vema kuhusu CUF na Zanzibar itabidi uweke Thread Mpya. Muhim tuijadili hii mada ya Tanganyika.
 
Babu yako ambae unadai alitoa pesa nyingi sana kumwezesha Germano Pacha (mkristu) kusafiri kwa treni kutoka Tabora hadi Dar es Salaam ( bila shaka kwa daraja la tatu) unamuona shujaa. John Rupia aliyelipa sehemu kubwa ya nauli ya ndege na gharama nyingine kumwezesha Julius Nyerere kwenda New York kutoka Dar es Salaam, haumuoni shujaa kwa sababu hakuwa muislamu! Ukweli ni kuwa si babu yako au John Rupia peke yao waliowachangia wanaharakati wa uhuru wetu. Wengi tu walichangia na wengine kwa zaidi yao maana sisi wamisheni tunaamini kuwa kipimo si kiasi gani ulichotoa bali ni kiasi gani ulichobaki nacho baada ya kutoa. Unamtupia madongo George Magembe lakini ni wewe uliyesema haya katika article yako nyingine:

Nimeitoa hapa: Wako wapi mashujaa wa Uhuru Tanganyika?

Huyo ambaye leo unadai hakutaka kushirikiana na babu yako, awali ulikiri kuwa alishirikiana nae katika kumsafirisha Germano Pacha kuja Dar es Salaam. Mbaya zaidi unataka kutuaminisha kuwa ni babu yako peke yake ndiye aliyehusika na safari hiyo!

Katika article hiyo hiyo una haya ya kusema kuhusu wazalendo waliopigania uhuru wetu:

Wewe ni mchochezi na mpindishaji wa historia. Hausiti kupindisha historia ili mradi ipandikize chuki katika jamii yetu!

Amandla.......
 
1. Hivi unaamini kuwa kuna mtu ambae alikuwa na ubavu wa kumzuia Nyerere kuendelea na urais au kumkataa mtu yeyote kumrishi? Nyerere asingetaka Mwinyi achukue madaraka, Mwinyi asingechukua madaraka, period.
2. Nitajie chuo kikuu kimoja kilichojengwa kwa pesa za walipa kodi ( iwe serikali kuu au shirika la umma) ambacho Mkapa aliwapa wakristu. Au hata shule moja ya chekechea ambayo aliikabidhi kwa wakristu!
3. Makamu wa Rais, Waziri wa Fedha, IGP, Mkuu wa TISS,,,,,, tayari wamezidi watatu! Kama hawa mnaona wachache basi heri mngesema angeteua wangapi ndiyo angewaridisha.

Hiyo HAKI itatendekaje wakati hamtaki kuifafanua! Tutajuaje kama HAKI imetendeka au la wakati hamjaeleza kipimo chake? Au wenyewe hamjui mnachokitaka?

Amandla.......
 
MOHAMED SAID,umeyasikia hayo-kulikuwa na kiumbe yoyote tanzania,ambaye angeweza kumzuia nyerere asiendelee uraisi? na bila ridhaa YAKE hata huyo mwinyi uraisi si angeusikia katika bomba tu
 
Huyu Mohammed said ni kati ya wale wanaotafuta umaarufu wa kisiasa kwa kupitia mgongo wa dini. Ni kukosa shukrani kabisa kwa Mungu kudai Nyerere aliyechukua shule zote za kikristu na kuzifanya kuwa za serikali ili watoto waote wasome bila kujali dini zao. Kikwete Mwenyewe aliwahi kukiri kusoma kupitia shule zilizokuwa za kikatoliki lakini zikataifishwa na Nyerere ili watanzania wote wasome bila kujali dini zao. Miaka yote ya madarakani wasadizi wakubwa wa Nyerere wlikuwa ni waislamu; kuna wakati alikuwa na makamu wa rais wote wawili wakiwa ni waislamu, na kuna wakati wizara zote nyeti za fedha, ulinzi, mambo ya nje, na mambo ya ndani zilikuwa chini ya waislamu. Kujaribu kujadili upuuzi huu ni kuturudisha nyuma sana wakati watu tunafikiria namna ya kuondokana na utawala lemavu wa CCM.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…