Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
Aaaah nashukuru the power ya Mtandao.... Nimefanya ku google na nimepata kipande hiki kuthibitisha kile nilichosema mimi....

Monday, 19 April 2010
KARUME MWANZILISHI WA YANGA NA JINA LA SIMBA SPORTS CLUB

Na Ibrahim Mkamba

HISTORIA yetu katika mambo mengi imepotoshwa ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya.Ni upotoshaji wa historia mtu anapoizungumzia klabu ya Young Africans maarufu kama Yanga bila kumzungumzia hayati Sheikh Abeid Aman Karume ambaye tangu atutoke kwa kupigwa risasi mwaka 1972, tarehe 7 mwezi huu na mwak huu ilitimia miaka 38 kamili.Ni upotoshaji wa historia mtu anapozungumzia jina la Simba Sports Club bila kumtaja Rais huyo wa kwanza wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza, wa kwanza, wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha,ni kosa kubwa kiimani na kimaadili mtu kuzipongeza klabu za Simba na Yanga kuwa na majengo yake bila kumhusisha kwa kiwango kikubwa hayati Karume.Kutomhusisha huko,kiimani ni dhambi ambapo kimaadili ni utovu mkubwa wa shukrani.Kwa maneno mengine,klabu za Yanga na Simba zilifanyiwa makubwa mno na hayati Karume kinyume cha jinsi historia inavyofanyiwa jitihada kwa Mwenyekiti huyo wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar kutosikika sana ndani ya klabu hizo za soka zenye mashabiki wengi ndani ya Jamhuri nzima ya Muungano wa Tanzania.

Aliyoyafanya Karume kwa Yanga

Historia iliyoandikwa haielezi vizuri ukweli kwamba Sheikh Abeid Aman Karume alikuwa mhamasishaji mkubwa wa kuanzishwa kwa klabu ya soka ambayo sasa ndiyo hii inayoitwa Young Africans yaani Yanga.Baada ya kufanya kazi ya ubaharia iliyomuwezesha kuzunguka karibu dunia nzima kwa miaka kadhaa akiwa kijana mdogo, Karume alipata uzoefu wa yaliyotokea kwenye nchi mbalimbali alizozunguka duniani na kugundua kwamba serikali za kikoloni zilipiga vita uanzishwaji wa vyama vya siasa na wananchi wazawa lakini zilikuwa hazipingi vyama vya kijamii kama klabu za michezo.

Baada ya kuufahamu ukweli huo,akiwa nyumbani Zanzibar,Karume alijiunga na wenzake na kuunda klabu ya soka iliyojulikana kama African Sports Club,mwenyewe akiwa mchezaji mahiri wa timu ya klabu hiyo.Humo humo kwenye mikutano ya kisoka ndimo yeye na Wazanzibari wenzake walikuwa wakijadili jinsi ya kujinasua toka kwenye utawala wa kisultani uliokuwa ukilindwa na Waingereza.

Ni hayati Karume ndiye aliyehamasisha kuanzishwa kwa matawi ya hiyo African Sports ya Zanzibar na akafanikiwa kuanzishwa kwa tawi la timu hiyo jijini Dar es Salaam ambalo kwa sasa ndilo hii klabu kubwa sana ya Yanga na kule Tanga alifanikisha kuanzishwa kwa tawi jingine ambalo ni African Sports ya Tanga.Kumbuka kuwa kwenye miaka hiyo ya nyuma miji ya Dar es Salaam,Bagamoyo,Pangani na Tanga ilikuwa na ukaribu sana wa kimahusiano na miji ya visiwa vya Unguja na Pemba.

Baada ya kuanzishwa,timu hizo tatu za Yanga ya sasa,African Sports ya Zanzibar na African Sports ya Tanga zilitengeneza undugu wa damu mkubwa mno.Zote tatu zilikuwa chimbuko la hayati Karume ingawa historia haiuweki wazi ukweli huo.

Kwa Yanga pia, hayati Karume ndiye alitoa kiasi kikubwa cha pesa,kama siyo chote, mwaka 1971 kwa kufanikisha ujenzi wa jengo la makao makuu ya Yanga la sasa lililopo kwenye makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani,Kariakoo jijini Dar es Salaam.Alifanya hivyo kwa Yanga baada ya kushirikiana na wana Simba kupata jengo lao kwenye mtaa wa Msimbazi,Kariakoo,jijini Dar es Salaam mwaka huo 1971 kwa kuchangia kiasi cha pesa. Ki msingi,hayati Karume alishiriki kujenga majengo yote mawili ya klabu za Yanga na Simba ingawa historia iliyoandikwa haitaki kuuweka wazi ukweli huo.

Hivyo ndivyo hayati Karume alivyoifanyia klabu ya Yanga tangu kuanzishwa kwake mpaka kupata jengo la makao makuu yake.Ukitaka kuamini jinsi jengo la Yanga lilivyo na mahusiano na Wazanzibari,tangaza leo kupigwa kwake mnada,uone jinsi utakavyoshukiwa kwa hasira na Wazanzibari.Kama huamini,nitakukumbusha.Mwaka 1988 jengo hilo lilikuwa lipigwe mnada baada ya Yanga ya kina Ally Bwamkuu kudaiwa kiasi fulani kikubwa cha pesa.Kila kitu kilikamilika kwa hatua hiyo kutekelezwa lakini hilo halikufanyika baada ya jopo la Wazanzibari kadhaa kutia timu Dar es Salaam na kuweka pingamizi dhidi ya hatua hiyo kwa sababu kulikuwa na mkono wa Wazanzibari kwenye ujenzi wa jengo hilo.Mnada haukuwepo na deni lililipwa kwa njia nyingine.
 
Yaya: Ahsante kwa mchango wako kama alivyosema Imam Shaffi kasema yeye anaweza kusimama na hata watu mia moja kwa hoja lakini akashindwa na mjinga mmoja. Kama ni hii historia ya wazee wangu sihitaji kuja kufunzwa na mtu. Naijua vyema sana. Nyerere alishindwa kumtaja Abdulwahid Sykes kwa kuwa yeye alijua historia yake mwenyewe ya awali katika kupigania uhuru wa Tanganyika akimtia Abdu atakuwa kajikata shingo. Abdu alikuwa mtu tofauti sana katika wazee wetu. Kapasi kuingia Makerere College mwaka 1942 akiwa na miaka 17. Alikuwa na akili kali sana. Soma kitabu changu utapambana na mambo ya ajabu hujapata kusikia. Humu ukumbini watu wamepata mshtuko nilipowaambia hotuba ya aliyosoma Nyerere UNO 1955 iliandikwa na marehemu Abdulwahid Sykes 1950. Akili zao zimekataa katu katu kuamini. Kwao ni sawa na kubebeshwa mlima lakini wepesi kuamini kuwa Nyerere kaja Dar es Salaam, kaanzisha TANU, kapata wanachama, ofisi na hela za kuendesha chama peke yake!
 
Hakuna mtu aliyepinga lolote kuhusiana na AbdulWakil au mchango wake ktk harakati za Uhuru na Nyerere sii mwandishi wa historia ya Tanzania au Tanganyika.
Makosa ya mwandishi kama kina Makongo, na wewe pia umeandika Historia ya Uhuru wetu kwa makosa yale yale unayodai kutaka haki na ukweli tena basi wewe ukitukana na kukashifu upande wa pili jambo ambalo hata huyo Makongo hakufanya wala kuandika kwa sababu yeye ni mkristu. Wewe umefanya hivyo na ndicho tunachokipinga sote hapa.

Tumekuomba kama unataka kuandika Historia ya Uhuru wa Tanganyika au Tanzania andika kama tunavyofahamu sote, wengine hatuna kipaji cha kuandika isipokuwa tunafahamu baadhi ya mambo muhimu ambayo tumekuchangia isipokuwa wewe hutaki ila yako tu (kitabu chako) ndiyo yenye ukweli wa mwisho..
 
Ibrahim Mkamba: Hongera sana ndugu yangu. We si mjukuu wa Sheikh Idris bin Saad Khalifa wa Tariqa Askariyya au majina yamefanana?
 
Huu mjadala kwa kiasi kikubwa umeshaisha na kuna watu wameishiwa hoja.Ingekuwa ni masumbwi yenye mwamuzi,basi angeshaingilia kati kumuokoa Fundi Mchundo,Mkandara,Lole Gwasika.Kuna pahala Muhammed amesema hakumsoma Mkandara pale alipokuwa anafoka foka na kutoa matusi kama vile ujinga!,ujinga!.Hapa ndipo mimi na Mkandara tunapofanana kwa kufoka, na ingekuwa ni mitaani basi tungekuwa wa mwanzo kuzidunda.
Tuangalie jinsi watu walivyoishiwa nguvu:
1.
Mkandara:
....Na maadam umeacha kunisoma basi nakuweka wewe katika fungu la wale wanafikiria wanajua kumbe hawajui na wala hawatakji kujua.
.....lakini wewe pia ndio mwepesi wa kumlaumu Nyerere aliyekusomesha wewe toka shule ya msingi hadi chuo Kikuu ukiwa Muislaam na hata kufanya ibada katika shule ilojengwa na Nyerere ikiwa na msikiti ndani
.....Sifa zote kapewa Kenyatta, na hata ukienda Zambia kwa Kaunda, South Africa kwa Mandela yaani kote historia ya nchi hizi imeandikwa na mwaandishi wetu
Uchambuzi wa Ami:
Huu ndio ubinafsi wa wakristo wa Tanzania,ati kwa sababu Muhammed kasoma kwenye shule iliyojengwa na Nyerere iwe ndio basi inatosha.Muhammed anawakumbuka mamilioni ya ndugu zake waislamu ambao wameshindwa kupata elimu kama yake kutokana na mtandao wa kuwakandamiza waislamu.
Mkandara anashangaa kule Kenya kwa sifa zote kupewa Kenyatta ilhali wako wapigania uhuru wengine.Hili si ndilo tunalolaumu hapa kwetu kuhusu waasisi wa TANU!.Haiwezekani kuwataja wote lakini hata waasisi pia akina Sykes.Haionekani hilo ni tatizo?.
Mkandara akienda kijijini hukuta watu wengi aliowasahau.Watu wa kawaida munaoonana mara moja waweza kuwasahau,lakini iwapo una akili nzuri mpaka ukafikia kuwa raisi si rahisi kuwasahau watu muliokaa pamoja kwa muda mrefu na kufanya vitu muhimu pamoja,hata ikiwa kakonda basi sauti yake tu itakushtua.Ukimsahau basi wewe ni mtu mwenye dharau na kibri.

2.
Mohammed Said
.......Huyu Sheikh Hassan bin Amir nguvu zake kwa Waislam wakati ule ni kama Kadinali Pengo kwa Wakatoliki hivi sasa
Fundi Mchundo
.......Hakuna kiongozi wa dhehebu la wasunni anayeweza kuwa na nguvu sawa na kadinali kwa
wakatoliki
Ami
......Katika mjadala huu Mohammed Said anaweza kuwa ndiye thiqqa.
Mkandara
......Ni kazi yetu sisi woote na ajabu ya Mungu ni pale unapofikiria kumpa Mohamed Said
hadhi ya Thiqqa kwamba kapokea hadithi kama wakati wa Mtume hali haya yote tunayozungumza ni mambo ambayo yametokea wakati wetu na sii hadithi.

Uchambuzi wa AMI
Mohammed kasema Hassan bin Amir ni kama Pengo,Fundi Mchundo anazungumzia usawa.Hapa matumizi ya lugha katika mazungumzo na uandishi yamempita.Tatizo kama hilo kalirudia Mkandara.Wakati AMI nimesema Muhammed anaweza kuwa Thiqqa.Mkandara anasema Nimekufuru kwa kumuita Muhammed kuwa ni mpokezi wa hadithi za Mtume (s.a.w).Hilo sio maana ya Thiqqa,hii ni aina ya wapokezi wa hadithi na hii ni sayansi ya hadithi ambayo imekuja baada ya kutawafu Mtume.Kukaa kwako Saudia Mkandara yaonesha hukusoma chochote cha kiislamu.
3
Fundi Mchundo
.......Mambo yalianza 1922, na si Dar bali Tanga. Nani anaikumbuka TTACSA ambako walitoka wengi wa waasisi wa AA? Conveniently, historian Mohamed Said amewasahau wote hawa na kumuona
Kleist Sykes peke yake! Ukweli ni kuwa hakuwa peke yake. Walikuwepo wengi.
Mohammed SAID
........FM: Ahsante ndiyo maana nasisitiza kuwa ingekuwa busara sana kama ungelisoma kitabu
changu ndiyo uingie katika mjadala. Hayo uloandika nilmeyaeleza katika kitabu. Nakudondoshea kidogo hapa chini nilivyoiona TTACSA:
Uchambuzi wa AMI
Soma jibu lote uone kushindwa kihoja kwa Fundi Mchundo na ukaidi wake unavyomfedhehesha.
4
Mkandara
.......Ulizia sisi watu tulowahi kuishi nchi zenye Ubaguzi. Hiyo Saudia yenyewe wanatubagua sisi pamoja na kuwa Waislaam...Unapokwenda kwao wanachukua hadi passport yako ya kusafiria na kukufanyisha kazi masaa 30 hadi 36 wasikupe hata muda wa kusali na huna mahala pa kwenda kuomba haki yako. Sana sana utafukuzwa nchini mwao
Uchambuzi wa AMI
Kule Saudia wewe Mkandara ni mgeni na mambo ya kule inabidi uvumilie.Hushangai ubaguzi na chuki vya hapa kwetu vinavyofanywa na wakristo kwa wananchi wenzao waislamu?.Juzi tu hakimu mkristo kamfunga muislamu kwa kukataa kuvua kofia mahakamani ambalo ndilo vazi lake.Soma mkasa wenyewe hapa unaotaka kufanywa sheria.

5.
Muhammed Said
......Kwao wao nimepokea heshima, na mialiko. Ajabu naiona kwenu kila mkisoma hoja zangu hamaki zinapanda.
Uchambuzi wa Ami
Hii ajabu ya hawa wachangiaji hapa ndiyo ajabu ya wakristo wa Tanzania.Utashangaa vitu vinavyoonekana ni vya maana na hata wakristo nchi nyengine hapa kwetu pindi inapokuwa vinawahusu waislamu basi inakuwa ni nongwa.Hivyo usishangae kwamba utafiti wako umethaminiwa na wasomi mbali mbali lakini unabezwa na akina mie hapa JF,na wala hawaoni aibu kupinga suala la kielimu huku wenyewe wakijidai kuthamini elimu.
Hii yote ni kiburi iliyojengwa na Nyerere kwa mafanikio dhidi ya waislamu,kwa kuvunja nguvu zao na hata kufuta historia yao katika kudai uhuru.
Mimi ningekuwa ni muamuzi ningesitisha pambano kuokoa maisha ya wanaogaragara sakafuni.Kwa hapa JF ningekuwa moderator ningeufunga mjadala na kumwambia Muhammed Said "Muhammed nenda zako hawakuwezi hawa na hawana hoja!."
 
Ami,
Mkuu wangu wee hutaelewa maana kwa sababu unaongozwa na Udini. Hakuna mahala popote wala kitabu chochote kilichomsifia Nyerere na viongozi wengine kwa UKRISTU wao kufanikisha Uhuru wa nchi zao. Sasa iweje wewe uone kama Nyerere ni mkristu kwanza kabla ya Utaifa wake kwa sababu tu unamwona AbdulWahid na wengine kuwa ni waislaam..Mohammed said anawajua kina Sykes nasi pia tunawajua vile vile na tunaongea mnao kama anavyoongea nao yeye. Hawakufanya lolote kwa sababu ni Waislaam isipokuwa kwa sababu ni wazalendo.

Hoja ya kuandika vitabu mtu yeyote anaweza kuandika. Nyerere hakuandika historia ya Uhuru wetu ila ni sisi tunaoandika kama alivyoandika Mohamed Said na Nyerere asimweke hatiani pamoja na kwamba kafany vitu ambavyo tunatishwa kwamba Nyerere angechukua hatua kubwa sana. ndipo tunajiuliza mbona Mohamed said yupo na hakupatwa na mabaya yoyote tena akijisifu kwamba hakumwogopa Nyerere!

- Kabla ya Uhuru Waislaam walikuwa asilimia ndogo sana chini ya 20 lakini baada ya kuingia Nyerere hadi kufikia sasa wamefika hesabu sawa na wakristu kama sii zaidi. Kuhusiana na Jumuiya ya Waislaam wa East Afrika nimekwambia ni Waislaam wenyewe kina Adma Nassibu ndio walitia fitna ikafungwa na hata kuanzisha uhasama mkubwa baina ya serikali na Waislaam.

- Ni nyerere aliyetaifisha shule zote za Kikristu ili sote tupate elimu ikiwa ni pamoja na wewe, Mohamed Said na waislaam kibao ambao leo hii wanajivunia elimu waliyopata. na amini maneno yangu mimi siamini kama Wakristu wamesoma kuliko Waislaam - I don't believe that hadi niambiwe wanatumia kipimo gani.

- Mwinyi ndiye alirudisha mahusiano ya Israel wakati Nyerere chini ya uongozi wake alikataa katakata kuwatambua, na kwa taarifa yako moja ya mashartii magumu ya IMF ilikuwa kuitambua Israel.. Nyerere alikataa na tukala unga wa njano kwa miaka 10 - It's a fact

- Jumuiya ya waislaam Afrika mashariki ilifutwa na Waislaam wenyewe kina Adma Nassibu ambao walikuja jenga uhasama mkubwa baina ya serikali na waislaam hadi masheikh kibao waliopingana kukamatwa na wengine kupoteza hata maisha yao kwa sababu ya hilo li BAKWATA - It's a fact

- Makahama ya kadhi ilifutwa na Kaluta Amri Abeid akiwa waziri wa sheria mwaka 1963 kama sikosei laa sivyo ingekuwepo hadi leo na wala msingesumbuana na wakristu leo hii. - It's a fact.

- Haya kama nilivyotabiri, dunia nzima Idd El fitr ni Ijumaa, Tanzania na hao Bakwata sijui kadhi mtasherehekea Jumamosi najua ujinga wa Bongo. Yaani nyie mnapanga mnavyotaka hata siku za sherehe ya Idd.

Wakati wa Nyerere mihadhara ya kiislaam ilifanyika uwanja wa Mnazimmoja pasipo vurugu wala mishker na Watu wengi waliukubali Uislaam kuliko wakati wowote wa utawala wa viongozi wetu na hata Zanzibar walikuwa huru zaidi na Uislaam kuliko leo hii chini ya viongozi waislaam.

Nyerere ametuondoa kajenga msikiti wakati hajawahi jenga kanisa.. tena kajenga kwao na unajua fika thabwabu za kufanya kitendo hicho. Hawa woote wanamlalamikia Nyerere hata tofali la msikiti au shule hawajawahi changia.

Ni kweli kabisa UDSM ina mahala dedicated kwa ibada ya sala kwa waislaam jambo ambalo huwezi kuliona ktk tawala yeyote ya mbaguzi wa kidini. Na hakika wakati wa Nyerere tulikuwa tukipata waislaam wote muda wa kwenda sali Ijumaa..

Huyu Nyerere aloukwaza Uislaam au kupiga vita harakati za Waislaam ni yupi tupeni jambo moja tu ambalo sisi wote tunalikubuka kwani hakuna mtu alozaliwa jana hapa. Sote ni matunda ya Uhuru, utawala wa Nyerere wote tunaukumbuka kama jana.
 
Mkandara: Ahsante kwa mchango wako. Tuendelee kusomeshana. Nafaidika sana na fikra zako.
 
Ami:Ahsante sana lakini mimi ningependa kuwasikia wao wenyewe wakitoa mbukwa.
 
Mkandara: Mimi nimefunzwa kwetu. Siwezi kutukana hata kidogo. Soma majibu yangu na isanifu lugha yangu.
 
Ami:Ahsante sana lakini mimi ningependa kuwasikia wao wenyewe wakitoa mbukwa.
Huyo Ami hana lolote hata dini yenyewe haijui vizuri. Ati majuzi hakimu Mkristu kamfunga muislamu kwa kukataa kuvua kofia mahakamani ambalo ndilo vazi lake.
Nani kamwambia kofia ni vazi la kiislaam?.

Oooh! lugha yako tamu tena wajua sana kuandika mkuu wangu lakini machungu yake huyaoni kwa sababu umejifungia ndani ya kabati la Udini. Mimi Muislaam kama wewe na najua nachoongea na nakuhakikishia kabisa leo hii Tanzania kuna Udini kupita wakati wowote ule na ndio maana wewe upo hapa.
 
Mkandara: Naweka hapa chini kitu kidogo kutoka kurasa za kitabu changu kwa faida ya wana-ukumbi wapya na wa zamani katika mjadala:

Mkutano wa kwanza wa uzinduzi wa TANU pale Ukumbi wa Arnautouglo ulihudhuriwa na kikundi kidogo cha takriban watu 20 miongoni mwao Julius Nyerere, Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajabu Diwani, Schneider Plantan, Marsha Bilali, Rashid Ally Meli, Frederick Njiliwa, Iddi Faiz Mafongo, Iddi Tulio, Denis Phombeah na wengineo.

Kuna picha mashuhuri sana ya wanachama waasisi wa TANU. Katika picha hiyo wanachama watatu hawaonekani, Ally Sykes, Tewa Said Tewa na Kasella Bantu. Hawa walikuwa watumishi wa serikali na kwa kanuni za utumishi katika serikali ya Kiingereza, watumishi wa serikali walikuwa hawaruhusiwi kujihusisha na siasa. Mwafrika yoyote aliyevunja amri hiyo kuu adhabu yake ilikuwa kufukuzwa kazi mara moja. Kwa hiyo picha hiyo ilipopigwa Ally, Tewa na Kasella Bantu walijondoa. Picha hiyo ilipigwa na Gomes mpiga picha maarufu sana wa Ki-Goa katika siku zile. Abdulwahid alikuwa amepatana na Gomes aje makao makuu ya TAA kupiga picha hiyo ya historia. Kwa bahati mbaya Gomes alichelewa kufika ofisi ya TAA. Abdulwahid alikosa subira kwa hiyo, alimwomba mdogo wake Abbas kwenda kumchukua Gomes kutoka kwenye studio yake Acacia Avenue (siku hizi Samora Avenue) katikati ya mji. Chombo pekee cha usafiri walichokuwa nacho TAA ilikuwa baiskeli moja iliyochakaa. Wakati Abbas ananyonga baiskeli kuelekea mjini kumchukua Gomes, Gomes alikuwa keshaondoka anakuja makao makuu ya TAA; kwa hiyo wakapishana njiani. Hivi ndivyo Abbas Sykes alivyokosa kuwepo ndani ya picha hiyo mashuhuri.

Lakini picha hii maarufu ilizua ubishi watu fulani waliupachika uso wa Kasella Bantu kewenye picha hiyo ili ionekane kama kwamba Bantu pia alikuwepo wakati ilipopigwa. Mkono wa mtu umechafua picha ile kwa kuingiza kwa ustadi uso wa Kasella Bantu ndani ya picha ile ili ionekane kama kuwa na yeye alikuwemo katika ile picha ilipopigwa. Uso wa Kasella Bantu umebandikwa katikati ya Abdulwahid na Chifu Patrick Kunambi kwa ustadi. Ingeweza kueleweka kama picha za Ally na Tewa zingeingizwa vilevile. Hivi leo kuna picha mbili za kihistori kwa kwa tokeo moja. Hivi sasa ipo ile nakala halisi isiyokuwa na wale wanachama watatu waasisi; na hii nakala mpya yenye kuonyesha uso uliobandikwa wa Kasella Bantu, lakini bila ya wale wenzake Ally na Tewa ambao hawakuwapo ndani ya picha toka awali. Germano Pacha amefafanua kwamba, kama isingekuwa kwa picha ile kungekuwepo na wanachama wengi waasisi wa TANU kuliko wale 17 wa mwanzo waliokutana mjini Dar es Salaam tarehe 7 Julai, 1954.

Mchunguzi mmoja wa mambo ameandika kuwa:

"...uso wa (Bantu) katika ile picha ya kihistoria uliingizwa na kitengo cha upigaji picha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mnamo Mei, 1974, miaka 20 baada ya kupigwa (picha hiyo). Pili, dai lake (Kasella Bantu) kuwa ilikuwa yeye aliyeitisha mkutano mkuu linamuonyesha kuwa ni mtu aliyelewa njozi ya historia. Rais Nyerere alichaguliwa rais wa TAA mnamo Oktoba, 1953 badala ya Kleist Sykes. Alikabidhiwa kazi ya kukigeuza TAA kuwa chama chenye nguvu cha kudai uhuru. Dai la Kasella Bantu la kutaka sifa (kwa hayo anayosema ametenda) haliungwi mkono na historia."

Ijapokuwa maelezo ya hapo juu yamesaidia kuonyesha jinsi historia ya Tanganyika ilivyojaa matatizo, mtu yoyote mwenye kuifahamu vyema historia ya TANU hatashindwa kuona makosa machache katika maelezo hayo. Julius Nyerere alichaguliwa kuwa rais tarehe 17 Aprili, 1953 na siyo Oktoba, 1953; na Nyerere hakuwa rais badala ya Kleist Sykes, lakini badala ya Abdulwahid Sykesm mwanawe Kleist Sykes.

Kasella Bantu ndiyo mtu aliyempeleka Julius Nyerere kwa Abdulwahid kumtambulisha. Hii ilikuwa mwaka wa 1952. Bantu na Nyerere walifahamiana toka huko nyuma walipokuwa wakifundisha Tabora. Chama hakiwezi kupinga ukweli kwamba Kasella Bantu alikuwa miongoni mwa wale wanachama 17 waasisi wa TANU. Hali kadhalika chama hakiwezi, kupinga ule ukweli wa historia kuwa Kasella Bantu alishiriki katika ìkuandikaî ile katiba ya TANU. Kasella Bantu anakerwa sana na kupotoshwa kwa historia. Kila alipopata fursa kuanzia alipokuwa ng'ambo uhamishoni na hata baada ya kurudi nyumbani kutoka uhamishoni, Kasella Bantu ameeleza kuhusu mambo haya mawili ya kihistoria, kuwa aliandika katiba ya TANU na ni mmoja wa waasisi wa TANU. Bantu kama waanzilishi wengine wengi anahisi kwamba mchango wake katika harakati za uhuru wa Tanganyika haujathaminiwa.

Ally Sykes ndiye aliyechora kadi ya TANU na kuchagua rangi na nembo yake. Rangi alizochagua zilikuwa, nyeusi kuwakilisha taifa la Kiafrika na kijani ardhi ya Tanganyika. Mfano wa kadi ya TANU ulitokana na kadi yake ya Tanganyika Legion. Baada ya kumaliza kuichora ile kadi, aliwaendea Tanganyika Standard Newspapers ili wamchapishie. Kutoka mfukoni mwake mwenyewe alichapisha kadi 1000 za kwanza na akitumia fedha za TAGSA alichapisha kadi nyingine 2000. Kadi nambari 1 ilitolewa na Ally Sykes kwa rais wa TANU, Julius Kambarage Nyerere na Ally aliweka sahihi yake kama afisa aliyeitoa. Ilipendekezwa kwamba kadi chache za mwanzo lazima zipigwe mnada na fedha zitakazokusanywa zitiwe kwenye hazina ya chama. Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz, Rupia na wengine walipanda dau kununua kadi hizo. Ally alimshinda kaka yake Abdulwahid kwa bei akapata kadi ya TANU nambari 2; Abdulwahid alipewa kadi nambari 3; Dossa Aziz kadi nambari 4; Phombeah kadi nambari 5; Dome Okochi, mmoja wa wale wazalendo kutoka Kenya katika TANU alipata kadi nambari 6 na Rupia kadi nambari 7. Bibi Titi kadi nambari 16; Iddi Tosiri kadi nambari 25.
 
Mohamed Said,
Mkuu wangu mengi uloandika hayana ubishi hata kidogo isipokuwa nambie hicho kichwa cha kitabu chako kinaitwa nini? na je vipo vitabu au sehemu yeyote inayopinga kwamba Waislaam hawakuchangia Uhuru wa Tanganyika? Na kama hakuna ni kina nani walioandika hivyo vitabu kama sii watu kama wewe.

Je ilikuwa kazi ya kina nani kuandika Historia safi isiyokuwa na utata kuhusu majina ya watu waliochangia harakati za Uhuru?. Je ni kutokana na msukumo wa dini zao au Uzalendo ndio uliwafanya wapiganie Uhuru wetu. Kama ndivyo what about their tribes haiwezi kuwa sababu pia na je unaweza ku prove moja ya hili kuwa ndio msingi wa Uhuru wa Tanganyika.

Je imekuwaje wewe ambaye huna hata wadhifa mkubwa serikali ya Nyerere au hii ya leo umeweza kuandika kitabu chenye utata zaidi kwa kutaja Waislaam kuwa ndio waliopigania Uhuru umeweza kuishi salama na pasipo kukwazwa lakini tunaambiwa Nyerere aliwakwaza wengi wasiandike Ukweli. Ni ukweli upi mzito kwa Nyerere kama angekuwa mdini kuliko wako?

Mimi hunigusa sana watu wanapotumia dini kuwa sababu ya Utawala dhalimu kwa mfano mauaji ya Pemba.. Nina hakika waliokuwa wakipinga CCM - Zanzibar (waislaam) ni Wapemba na wanachama wa CUF iweje swala lile lihusishwe na Uislaam hali ni la kisiasa. Ndio kusema CCM zanzibar ni wakristu kwa sababu tu walipingana na CUF.

Niko 100% askari waliokwenda Pemba na kufanya mauaji walikwenda huko kwa baraka za viongozi wa Zanzibar (Unguja) amnbao ni Waislaam sasa iweje lawama wapewe wakristu hali historia inaonyesha wazi kwamba ni Waislaam wenyewe hupanga mbinu za kuwamaliza wenzao huku wao wakifukia vichwa vyaomchangani kama mbuni! Tunayaona Iraq na Afghanstan yakiendelea na tusiwalaumu waislaam wenyewe kama haya ni ya Uislaam.

ndio maana mimi hata siku moja siwezi chukua dhamana ya mtu kwa sababu ni Muislaam kwani Uislaam sio mtu na jina lake isipokuwa ni kufanya ibada kama ulivyoagizwa na mitume. Binafsi naamini Unafiki ni dhambi kubwa sana kuliko hata kula nguruwe au kunywa pombe - utanisamehe. Waislaam wengi ni wanafiki sana tena kwa dini yao wenyewe.
 
Huu mjadala kwa kiasi kikubwa umeshaisha na kuna watu wameishiwa hoja.Ingekuwa ni masumbwi yenye mwamuzi,basi angeshaingilia kati kumuokoa Fundi Mchundo,Mkandara,Lole Gwasika.Kuna pahala Muhammed amesema hakumsoma Mkandara pale alipokuwa anafoka foka na kutoa matusi kama vile ujinga!,ujinga!.Hapa ndipo mimi na Mkandara tunapofanana kwa kufoka, na ingekuwa ni mitaani basi tungekuwa wa mwanzo kuzidunda.
Tuangalie jinsi watu walivyoishiwa nguvu:
1.
Mkandara:
....Na maadam umeacha kunisoma basi nakuweka wewe katika fungu la wale wanafikiria wanajua kumbe hawajui na wala hawatakji kujua.
.....lakini wewe pia ndio mwepesi wa kumlaumu Nyerere aliyekusomesha wewe toka shule ya msingi hadi chuo Kikuu ukiwa Muislaam na hata kufanya ibada katika shule ilojengwa na Nyerere ikiwa na msikiti ndani
.....Sifa zote kapewa Kenyatta, na hata ukienda Zambia kwa Kaunda, South Africa kwa Mandela yaani kote historia ya nchi hizi imeandikwa na mwaandishi wetu
Uchambuzi wa Ami:
Huu ndio ubinafsi wa wakristo wa Tanzania,ati kwa sababu Muhammed kasoma kwenye shule iliyojengwa na Nyerere iwe ndio basi inatosha.Muhammed anawakumbuka mamilioni ya ndugu zake waislamu ambao wameshindwa kupata elimu kama yake kutokana na mtandao wa kuwakandamiza waislamu.
Mkandara anashangaa kule Kenya kwa sifa zote kupewa Kenyatta ilhali wako wapigania uhuru wengine.Hili si ndilo tunalolaumu hapa kwetu kuhusu waasisi wa TANU!.Haiwezekani kuwataja wote lakini hata waasisi pia akina Sykes.Haionekani hilo ni tatizo?.
Mkandara akienda kijijini hukuta watu wengi aliowasahau.Watu wa kawaida munaoonana mara moja waweza kuwasahau,lakini iwapo una akili nzuri mpaka ukafikia kuwa raisi si rahisi kuwasahau watu muliokaa pamoja kwa muda mrefu na kufanya vitu muhimu pamoja,hata ikiwa kakonda basi sauti yake tu itakushtua.Ukimsahau basi wewe ni mtu mwenye dharau na kibri.

2.
Mohammed Said
.......Huyu Sheikh Hassan bin Amir nguvu zake kwa Waislam wakati ule ni kama Kadinali Pengo kwa Wakatoliki hivi sasa
Fundi Mchundo
.......Hakuna kiongozi wa dhehebu la wasunni anayeweza kuwa na nguvu sawa na kadinali kwa
wakatoliki
Ami
......Katika mjadala huu Mohammed Said anaweza kuwa ndiye thiqqa.
Mkandara
......Ni kazi yetu sisi woote na ajabu ya Mungu ni pale unapofikiria kumpa Mohamed Said
hadhi ya Thiqqa kwamba kapokea hadithi kama wakati wa Mtume hali haya yote tunayozungumza ni mambo ambayo yametokea wakati wetu na sii hadithi.

Uchambuzi wa AMI
Mohammed kasema Hassan bin Amir ni kama Pengo,Fundi Mchundo anazungumzia usawa.Hapa matumizi ya lugha katika mazungumzo na uandishi yamempita.Tatizo kama hilo kalirudia Mkandara.Wakati AMI nimesema Muhammed anaweza kuwa Thiqqa.Mkandara anasema Nimekufuru kwa kumuita Muhammed kuwa ni mpokezi wa hadithi za Mtume (s.a.w).Hilo sio maana ya Thiqqa,hii ni aina ya wapokezi wa hadithi na hii ni sayansi ya hadithi ambayo imekuja baada ya kutawafu Mtume.Kukaa kwako Saudia Mkandara yaonesha hukusoma chochote cha kiislamu.
3
Fundi Mchundo
.......Mambo yalianza 1922, na si Dar bali Tanga. Nani anaikumbuka TTACSA ambako walitoka wengi wa waasisi wa AA? Conveniently, historian Mohamed Said amewasahau wote hawa na kumuona
Kleist Sykes peke yake! Ukweli ni kuwa hakuwa peke yake. Walikuwepo wengi.
Mohammed SAID
........FM: Ahsante ndiyo maana nasisitiza kuwa ingekuwa busara sana kama ungelisoma kitabu
changu ndiyo uingie katika mjadala. Hayo uloandika nilmeyaeleza katika kitabu. Nakudondoshea kidogo hapa chini nilivyoiona TTACSA:
Uchambuzi wa AMI
Soma jibu lote uone kushindwa kihoja kwa Fundi Mchundo na ukaidi wake unavyomfedhehesha.
4
Mkandara
.......Ulizia sisi watu tulowahi kuishi nchi zenye Ubaguzi. Hiyo Saudia yenyewe wanatubagua sisi pamoja na kuwa Waislaam...Unapokwenda kwao wanachukua hadi passport yako ya kusafiria na kukufanyisha kazi masaa 30 hadi 36 wasikupe hata muda wa kusali na huna mahala pa kwenda kuomba haki yako. Sana sana utafukuzwa nchini mwao
Uchambuzi wa AMI
Kule Saudia wewe Mkandara ni mgeni na mambo ya kule inabidi uvumilie.Hushangai ubaguzi na chuki vya hapa kwetu vinavyofanywa na wakristo kwa wananchi wenzao waislamu?.Juzi tu hakimu mkristo kamfunga muislamu kwa kukataa kuvua kofia mahakamani ambalo ndilo vazi lake.Soma mkasa wenyewe hapa unaotaka kufanywa sheria.

5.
Muhammed Said
......Kwao wao nimepokea heshima, na mialiko. Ajabu naiona kwenu kila mkisoma hoja zangu hamaki zinapanda.
Uchambuzi wa Ami
Hii ajabu ya hawa wachangiaji hapa ndiyo ajabu ya wakristo wa Tanzania.Utashangaa vitu vinavyoonekana ni vya maana na hata wakristo nchi nyengine hapa kwetu pindi inapokuwa vinawahusu waislamu basi inakuwa ni nongwa.Hivyo usishangae kwamba utafiti wako umethaminiwa na wasomi mbali mbali lakini unabezwa na akina mie hapa JF,na wala hawaoni aibu kupinga suala la kielimu huku wenyewe wakijidai kuthamini elimu.
Hii yote ni kiburi iliyojengwa na Nyerere kwa mafanikio dhidi ya waislamu,kwa kuvunja nguvu zao na hata kufuta historia yao katika kudai uhuru.
Mimi ningekuwa ni muamuzi ningesitisha pambano kuokoa maisha ya wanaogaragara sakafuni.Kwa hapa JF ningekuwa moderator ningeufunga mjadala na kumwambia Muhammed Said "Muhammed nenda zako hawakuwezi hawa na hawana hoja!."

Amiii!
Wanichekesha sana weye!
Nafikiri kama mwalimu wangu mmoja,Mwalimu Mohammed-masikini marehemu, alivyowahi kusema, subsumers hazipandi!
IQ yako nafikiri ina walakin.
Unaconclude issue wakati mjadala uko upenuni mwako.
Issue mnayoitetea wewe na watu wa aina yako ni kama tunawachezea quarter ground na katika quarter yenu eneo la penalty.Magoli tusha wafunga na bado wala hamjaingia mduara wa kati.
Mada mlioitoa doesn't wash, na haiwasaidii wale mnaotaka kuwatetea maana haina mantiki ya Utaifa.
Sasa hapa tutaendelea kuwachezea shere na kuwa tia doba, zile asizozipenda Mohammed Said.Na ndio maana akifungwa goli la akili anakimbilia shajara za Abdul Sykes kwa mwongozo!!!
Pale mtakapoelewa kwamba maisha ya mtanzania pamoja na imani yake , ni umoja ,utaifa na maendeleo kwa kwenda mbele.
Mimi nawaona kwa utetezi wenu na hali mliyonayo ninyi ni wadandiaji tu wa mustakabali wa nchi hii.
 
galileo sms.jpg
 
Mohamed said,tumekusoma tumekuelewa,tunakubali some historical mistakes were made,though makosa mengi yalitokana na past masters wa tanganyika notably waarabu na waingereza and unfortunately leveling the playing field after independence has been hard.
But reading between the lines na hiki kiswahili chako cha Kariakoo,mission quarter and gerezani axis it seems you are by any means necessary advocating a "FINAL SOLUTION",a crusade by which the books with one swoop will be balanced.As a scholar of repute you will have noticed,historically this modus operandi has never worked apart from fragmanting a nation.please do the needfull and tell me i have read you wrong
 
Spot on Son of A
These guys are incorrigible villains scampering for A FINAL SOLUTION.
That is the alarm I have been raising all along.
This man Mohammed Said has absolutely no other remedy to the hue and cry he is raising, and that is despite several reminders from various contributors.
In that I have the opinion tat he will fail in whatever they aree scheming,with MS being the soft face of the scheme.
Wihout other Tanzanians support this issue will just smack on their faces.
 
Son of Alaska: Thanks for your contribution. I am uncomfortable with English language as I can not be as eloquent as I would like to so I will respond in my Kariakoo parlance. I hope you dont mind. Umekosea si kama nataka final solution. Hitler alijaribu hiyo na matokeo yake sote tunayajua. Kwanza kabisa nia yangu ni kurejesha heshima ya wazee wangu iliyokuwa imeporwa kwa kipindi kirefu. Pili nataka serikali ijue kuwa Waislam tunajuwa na tuko katika juhudi za kubadilisha hali hiyo kwa msaada wao au nje ya msaada wao. Taifa litashikana pale patakapokuwa hakuna mabwana na watwana na hii ndiyo itakayojenga amani ya kweli. Hali jinsi ilivyo sasa tumekalia kuti kavu kuanguka si ajabu.
 
Ahsante Yaya: Naomba kufanya sahihisho moja ni "Mlandizi" sio "Mlandege" kosa liko katika kitabu tafasiri ya Kiswahili.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom