Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Ukweli kuhusu waasisi wa TANU na harakati za kupigania uhuru

Status
Not open for further replies.
Mohamed said hodari wa kujieleza laiti ungeandika kitabu chako nje ya box la udini wallah ningekuwa wa kwanza kukisoma lakini baada ya kusoma hoja zako nakwambia hamu ya kukisoma imetoweka kabisa.
 
Yaya: Ahsante kwa kutuwekea hiyo nukuu kutoka tafasiri ya Kiswahili ya kitabu cha Abdu Sykes. Nakuwekea hapa chini kwa faida ya wanaukumbi mwisho wa EAMWS na siku za mwanzo za BAKWATA:

Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kuamriwa na Rais anatangaza kuwa tawi la Tanzania la East African Muslim Welfare Society na Baraza la Tanzania la la East African Muslim Welfare Society ni jumuiya zisizotambulika kisheria chini ya kifungu 6 (i) cha Sheria ya Vyama. Kwa tangazo hilo la Rais wa Tanzania, Julus Nyerere, Waislam walinyimwa nafasi ya kukutana na kuzungumza kuhusu tatizo ambalo kwa kweli liliwahisu Waislam peke yao. Kwa ajili hii basi Waislam walinyimwa nafasi ya kujadili na kulitolea uamuzi tatizo
hilo.

Viongozi wa EAMWS waliitwa mbele ya Kabidhi Wasii ambae ndiye alikuwa amekabidhiwa na serikali jukumu la kusimamia shughuli za kufunga rasmi shughuli za EAMWS. Viongozi walifahamishwa kuwa chini ya sheria ya vyama mali zote za EAMWS zitauzwa na madeni yatalipwa kutokana na fedha hizo na fedha zitakazobaki watapewa wanachama. Serikali ilikuwa haiwezi kufanya kama sheria ilivyokuwa imeelekeza. Ilikuwa jambo zito sana kwa serikali ya Nyerere kuonekana anasimamia kuuzwa kwa mali za Waislam. Viongozi wa EAMWS walipoitwa kwa Kabidhi Wasii mara ya pili walifahamishwa kuwa serikali imebadilisha mawazo yake kutekeleza amri kama sheria inavyosema kwa ajili hiyo basi imefanya mabadiliko ya sheria ya vyama ambayo yanaiwezesha sasa kutoa mali ya EAMWS na kukabidhi BAKWATA. Hivi ndivyo mali za EAMWS zilivyochukuliwa na kupewa BAKWATA bila ya ridhaa ya Waislam wenyewe. Hivi ndivyo shule zote zilizojengwa na EAMWS pamoja na mradi wa Chuo Kikuu cha Kiislam kilipoanguka katika mikono ya kundi la Adam Nasibu. BAKWATA haikuwa na uwezo wa kuendesha mipango yoyote na taratibu shule na miradi yote ya elimu ikafifia na mwishowe kufa kabisa. Hivi ndivyo halikadhalika moto wa Waislam uliowashwa kwa kupatikana kwa uhuru waliopigania hadi ukapatikana ulivyokufa. Moto huu ulikuja ukawaka tena, lakini hiki ni kisa kingine. Insha Allah Mwenyezi Mungu akipenda tutakuja kukieleza.

Huu ndiyo ukawa mwisho wa kile kilichokuwa kikijulikana kama mgogoro wa Waislam ulivyomalizika. Mgogoro ambao ulianza pale mwalimu wa shule ya msingi asiyefahamika na yeyote alipofanya maandamano katika mitaa ya Bukoba akimuunga mkono Julius Nyerere na Azimio lake la Arusha na ukaishia kwa mwalimu huyu akiwa na nafasi juu katika jumuiya ya Kiislam ambayo ilikuwa ikichukiza machoni mwa Waislam. Mwalimu huyu ambae sasa amekuwa Makamu Katibu Mkuu wa BAKWATA alianza kazi yake kwa kuwashutua Waislam. Katika mkutano wa waandishi wa habari Adam Nasibu aliiomba TANU na ASP kujikinga na watu wanaohujumu umoja wa nchi kupitia dini. Akaendelea na kusema kuwa BAKWATA ni sawa na Baraza la Kikristo la Tanzania. Kwa kuwa Waislam walinyimwa fursa ya kujadili ìmgogoroí hivi sasa kilichobaki na dhana tu, kuwa nini kingelitokea endapo wangeliruhusiwa kufanya mkutano ule ulioitishwa na EAMWS. Waislam wa Bukoba ambao ilitaarifiwa kuwa walifanya maandamano kuunga mkono Azimio la Arusha hawakutayarisha maandamano ya kuunga mkono BAKWATA. Dar es Salaam na katika miji mingi ya Tanzania, neno BAKWATA halina tofauti na tusi. Kumuita Muislam kuwa yeye ni mwanachama wa BAKWATA ni sawa na kumuita Mkristo mfuasi wa Yuda Iscariot, aliyemsaliti Yesu kwa vipande thelathini vya fedha.

Kilichobakia baada ya kuvunjika kwa EAMWS ilikuwa ni kujaribu kuiweka BAKWATA katika mikoa kama jumuiya inayowakilisha Waislam wote wa Tanzania Bara. Mwaka mzima wa 1969 Adam Nasibu na kamati ya watu wanne walitembea katika mikoa wakiahidi msaada wa fedha kwa katibu yeyote wa zamani wa EAMWS ambae atashirikiana na BAKWATA makao makuu kuisaidia kufungua ofisi katika mkoa wake. Waislam waliipuuza BAKWATA.

Tabora ambayo haikujitoa katika EAMWS, serikali iliwaruhusu Adam Nasibu na kikundi chake kufanya mkutano wa hadhara. Kabla Adam Nasibu hajahutubia Waislam, Maulid Kivuruga mmoja wa wakongwe wa African Association na muasisi wa TANU Tabora, alipanda jukwaani kwa niaba ya Waislam wa Tabora na kuweka sharti kuwa Waislam watakuwa tayari kumsikiliza Adam Nasibu endapo Waikela mjumbe wa Tume ya Waislam iliyokuwa ikitafuta sulhu na yeye ataruhusiwa na serikali kuwahutubia Waislam ili aeleze upande wa pili wa kisa kile. Kivuruga alisema kuwa Waislam wanaomba sharti hili likubaliwe kwa sababu katika Uislam panapotokea mgogoro basi mpatanishi ni lazima asikilize pande zote mbili. Sharti hili lilikataliwa na BAKWATA na serikali. Palepale mbele ya waheshimiwa wa serikali na viongozi wa BAKWATA, Waislam wakaanza kuzomea huku wakitawanyika wakipiga takbir na wengine wakiitikia Allahu Akbar.

Siku chache baada ya tukio hili Waikela aliitwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai kusailiwa kwa nini anaipinga BAKWATA. Wakiwa ndani ya chumba cha Tabora Hotel, Geoffrey Sawaya, Mkurugenzi wa C.I.D, alimpiga maswali Waikela na kutaka kujua kwa nini yeye hayuko tayari kushirikiana na serikali kuipa nguvu na kuieneza BAKWATA. Sawaya akatoa hongo ya shilingi elfu arobaini kwa Waikela ili asaidie kuimarisha BAKWATA. Waikela kama istizai alimuuliza Sawaya kama fedha zile zilikuwa zimetoka bait mal. Waikela alikataa kupokea hongo ile. Sawaya akamtisha lakini Waikela hakutishika. Waikela aliwekwa ndani ya chumba kile akiulizwa maswali kwa kiasi cha saa nne na kisha akaamrishwa kuweka sahihi yake katika makaratasi fulani. Hili alilifanya. Waikela hakufuatwa tena na serikali. Ingawa kulikuwepo na juhudi za chinichini za kuipinga BAKWATA, juhudi hizi hazikushinda kwa kuwa BAKWATA iliweza kufungua matawi yake nchi nzima pamoja na Tabora. Wapo baadhi ya viongozi ambao hawakuweza kuhimili vishawishi vya kupokea ile hongo ya serikali na kwa ajili hii walishirikiana na serikali hivyo kuwezesha ofisi za BAKWATA kufunguliwa, hata kama zipo pale kwa jina tu.
 
Kabonde: Ahsante kwa mchango wako. Hivi ndivyo dunia ilivyo si wakati wote ukweli utakubalika. Usinisome sawa lakini baada ya kusoma haya ulosoma ukumbini nakushauri kasome "Historia ya TANU 1954 - 1977" kitabu kilichoandikwa na Chuo Cha Kivukoni. Jasho litakumwagika jepesi. Kama mimi unaniona ni "mdini" basi hao wenzangu ni "wanyerere." Kitabu chao ni kisa cha "Superman" mbabe aliekuwa na uwezo wa kuibeba gorofa nzima akarukanayo angani. Mwanzo wa kurasa hadi mwisho ni Nyerere tu kiasi kitabu kinakuwa sawa na mchuzi ulochujuka. Ila nakushauri kisome kitabu changu ndipo utakuwa katika hali ya kunijua na kuujua upande mwingine wa mwezi.
 
Mohamed Said,

..mimi sina tatizo na kutokuwepo kwa Wakristo ktk jamii za Warufiji,Wamanyema, etc etc.

..ziko jamii nyingi tu hapa Tanzania ambapo dini moja ndiyo dominant. suala hilo ni la kawaida kabisa hapa Tanzania.

..tatizo nililoliona mimi ni ile lugha uliyotumia kuielezea fact hiyo. uliielezea fact hiyo kama jambo la kushukuriwa, na zaidi kama vile ni jambo la kujivunia.

..tunaishi ktk jamii ambayo iko diverse na information zinasambaa kwa kasi mno. i dont think, a sensitive and responsible person, one who knows for a fact that our country is diverse, would make such a statement.

..binafsi nadhani ungeweka pembeni conclusions zako za UDINI-UDINI watu wangeweza kuipokea kazi yako kwa umakini unaostahili.

NB:

..sasa kwa hapa tulipofikia, je unaweza kutueleza mchango wa Mwalimu ktk kupigania uhuru ulikuwa ni nini?

..pia kwanini hukutafuta wasaa wa kumhoji, ukiwa na facts ulizokuwa nazo, na kusikiliza upande wake wa hadithi?

..je, huoni kwamba na wewe umetumbukia ktk kosa lilelile unalojaribu kurekebisha, ambalo ni kufuta na kupuuza michango ya baadhi ya watu ktk kupigania uhuru wa Tanganyika??
 
Ili kuweka mizani sawa na kuondoa miwani ya udini nawashaurini nyote mliosoma kitabu cha Mohammed Said, kama mimi, pia msome kitabu cha Lawrence E.Y. Mbogoni "The Cross versus The Crescent" Religion and Politics in Tanzania from the 1880s to the 1990s. Hiki kimeandikwa kisomi vile vile bila miwani ya udini. Kwa walioko Tanzania kimechapishwa na Mkuki na Nyota Publishers.
 
Kabonde: Ahsante kwa mchango wako. Hivi ndivyo dunia ilivyo si wakati wote ukweli utakubalika. Usinisome sawa lakini baada ya kusoma haya ulosoma ukumbini nakushauri kasome "Historia ya TANU 1954 - 1977" kitabu kilichoandikwa na Chuo Cha Kivukoni. Jasho litakumwagika jepesi. Kama mimi unaniona ni "mdini" basi hao wenzangu ni "wanyerere." Kitabu chao ni kisa cha "Superman" mbabe aliekuwa na uwezo wa kuibeba gorofa nzima akarukanayo angani. Mwanzo wa kurasa hadi mwisho ni Nyerere tu kiasi kitabu kinakuwa sawa na mchuzi ulochujuka. Ila nakushauri kisome kitabu changu ndipo utakuwa katika hali ya kunijua na kuujua upande mwingine wa mwezi.

Mbona cha kwako limejaa Sykes na Uislam tuu? :eyebrows:
 
Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kuamriwa na Rais anatangaza kuwa tawi la Tanzania la East African Muslim Welfare Society na Baraza la Tanzania la la East African Muslim Welfare Society ni jumuiya zisizotambulika kisheria chini ya kifungu 6 (i) cha Sheria ya Vyama. Kwa tangazo hilo la Rais wa Tanzania, Julus Nyerere, Waislam walinyimwa nafasi ya kukutana na kuzungumza kuhusu tatizo ambalo kwa kweli liliwahisu Waislam peke yao. Kwa ajili hii basi Waislam walinyimwa nafasi ya kujadili na kulitolea uamuzi tatizo
hilo.

Mimi ndiyo maana nakuita mchochezi. Kwa mtu anayedai kuwa alifanya utafiti wa kina, unashindwaje kutaja jina la huyo waziri ya mambo ya ndani? Au kwa vile aliitwa Omari Muhaji, muislamu mwenzako, ndiyo ugumu unaingia? Ugumu ambao haunao inapokuja kwa Julius Nyerere. Unadai kuwa Mwalimu kama rais alitoa tangazo wakati hapo hapo unasema kuwa alimuagiza waziri muislamu atoe tangazo hilo, sasa tuamini lipi? Kuwa tangazo lilitoka kwenye ofisi ya Rais au kwa waziri wa mambo ya ndani? Tangazo hilo, ingawa lilisema limefuata maagizo ya rais lakini halikuwa la Rais. Ungetaka kuwa sahihi, ungesema tangazo lillilotolewa na Omari muhaji kwa niaba ya Julius Nyerere.

Unainsinuate kuwa chanzo cha uhasama wote dhidi ya EAMWS ni Mwalimu na unashindwa kabisa kukiri kuwa mamlaka ya kwanza kufungia shule za EAMWS ilikuwa ni serikali ya Mapinduzi Zanzibar, iliyojaa waislamu watupu. Hautaki kuzungumzia mchango wa Abeid Aman Karume katika kifo cha EAMWS. Haumzungumzii Adam Nasibu, kiongozi wa tawi la EAMWS, Bukoba aliyetangaza mkoa wake kujitoa kutoka EAMWS mwezi Oktoba 1968, akifuatiwa na tamko la Sheikh Juma Jambia wa Tanga kujitoa na hatimaye mikoa 9 kati ya 17 kujitoa EAMWS ilipofika Desemba 1968. Hautuambii kuwa kikao kilichoanzisha bakwata ni kile kilichofanyika Iringa tarehe 13 Desemba 1968, ambacho kilifunguliwa na kufungwa na Abeid Aman Karume na Rashid Kawawa. Hautuambii kuhusu mchango na uhasama wa Sheikh Abdallah Chaurembodhidi ya EAMWS. Hautuambii kuwa Sheikh Hassan hakuwa Khalifa na hakutambuliwa kama sehemu ya Tariq na viongozi wa Sufi wakati Sheikh Abdallah Chaurembo alikuwa kiongozi katika order ya Shadhili. Maana yake Sheikh Chaurembo hakuwa zezeta wa kuburuzwa ovyo ovyo na mkatoliki Julius Nyerere. Yeye na wenzake waliipinga EAMWS kwa misingi ya uzalendo, walikiona kama chombo cha mabepari wa kihindi na kiarabu. Hawa ndio waliouwa EAMWS na sio mkatoliki Julius Nyerere.

Amandla......
 
Tarehe 27 Aprili, 1985 Julius Kambarage Nyerere, sasa akijulikana kama Baba wa Taifa, katika sherehe kubwa katika viwanja vya Ikulu, alitoa jumla ya medali 3979 kwa Watanzania waliochangia katika maendeleo ya taifa. Kati ya wale ambao walipewa medali hizo alikuwa Sheikh Abdallah Chaurembo.
Wazalendo waliotajwa ndani ya kitabu hiki ambao walipigania uhuru wa Tanganyika, hakuna hata mmoja wao aliyekuwa katika orodha ile ya heshima. Baada ya siku chache kupita, Nyerere kama mtu aliyegutuka alimualika Dossa Aziz Ikulu. Dossa Aziz, wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alikuwa mtu maarufu, mwenye nafasi, na kujiweza sana. Sasa Dossa baada ya miaka kupita hakuwa akifahamika tena na ule umaarufu na utajiri wake ulikuwa umetoweka. Alikuwa akiishi maisha ya kawaida kijijini Mlandege, maili chache nje ya Dar es Salaam. Katika sherehe ya faragha Nyerere alimtunukia medali Dossa Aziz, rafiki yake wa zamani.

Sasa kama ni mbaya kiasi ambacho mnasema, kwa nini asingekausha tuu na kutomtunuku nishani yeyote! Orodha ya watu wanaostahili medali huwa haiandikwi na rais peke yake bali jopo la watu. badala ya kutambua utu wa mtu anayekubali kurekebisha makosa yake, nyinyi mnambeza!

Amandla.....
 
Safari: Ahsante kwa mchango wako lakini mbona una hamaki nimekuudhi kitu gani ndugu yangu? Hiyo lugha ya kutuniza "limejaa" lugha ya mtu aliyeghadhibika. Lugha ya kiungwana ingekuwa "kimejaa."

Kitabu changu kinaitwa: "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 -1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika." Hiki ni kitabu kinachoelezea maisha ya Abdulwahid Sykes na zile nyakati alizoishi yaani miaka ya 1920 hadi miaka ya 1960. Sasa hapa kama sikueleza maisha yake ningeeleza kitu gani? Kisha kitabu kinachambua mchango ambao ulikuwa haujaelezwa wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Sasa kama singeeleza habari za Uislam na Waislam ningeandika kitu gani? Ni hivyo tu. Nadhani umenielewa. "Historia ya TANU" ni kitabu kinachoeleza habari za TANU na jinsi chama kilivyoanzishwa. Kichekesho ni kuwa waandishi wa Chuo cha Kivukoni "wakamsahau" Abdulwahid Sykes ambae hicho chama chenyewe mikutano yake ya siri kuanzia 1950 hadi siku wanakianzisha rasmi tarehe 7 Julai 1954 ilikuwa ikifanyika nyumbani kwake na yeye akiwa kiongozi. Acha hilo hata hiyo nyumba yenyewe iliyoasisiwa chama chenyewe ilijengwa na baba yake. Kitabu kinamtaja Nyerere peke yake kama ndiye muaisisi. Kwa bahati mbaya au nzuri Nyerere nae hakuwakumbusha au kuwaeleza kuwa TANU nimeikuta nilipokuja Dar es Salaam 1952. Hapa ndipo nikaona iko haja ya kuandika kitabu na kueleza kisa kizima cha historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ntakuongezea kitu kingine. Nimeandika kitabu kingine "Torch on Kilimanjaro" Oxford University Press, Nairobi 2006. Humo kajaa Mwalimu Nyerere.
 
Mimi ndiyo maana nakuita mchochezi. Kwa mtu anayedai kuwa alifanya utafiti wa kina, unashindwaje kutaja jina la huyo waziri ya mambo ya ndani? Au kwa vile aliitwa Omari Muhaji, muislamu mwenzako, ndiyo ugumu unaingia? Ugumu ambao haunao inapokuja kwa Julius Nyerere. Unadai kuwa Mwalimu kama rais alitoa tangazo wakati hapo hapo unasema kuwa alimuagiza waziri muislamu atoe tangazo hilo, sasa tuamini lipi? Kuwa tangazo lilitoka kwenye ofisi ya Rais au kwa waziri wa mambo ya ndani? Tangazo hilo, ingawa lilisema limefuata maagizo ya rais lakini halikuwa la Rais. Ungetaka kuwa sahihi, ungesema tangazo lillilotolewa na Omari muhaji kwa niaba ya Julius Nyerere.
Unainsinuate kuwa chanzo cha uhasama wote dhidi ya EAMWS ni Mwalimu na unashindwa kabisa kukiri kuwa mamlaka ya kwanza kufungia shule za EAMWS ilikuwa ni serikali ya Mapinduzi Zanzibar, iliyojaa waislamu watupu. Hautaki kuzungumzia mchango wa Abeid Aman Karume katika kifo cha EAMWS. Haumzungumzii Adam Nasibu, kiongozi wa tawi la EAMWS, Bukoba aliyetangaza mkoa wake kujitoa kutoka EAMWS mwezi Oktoba 1968, akifuatiwa na tamko la Sheikh Juma Jambia wa Tanga kujitoa na hatimaye mikoa 9 kati ya 17 kujitoa EAMWS ilipofika Desemba 1968. Hautuambii kuwa kikao kilichoanzisha bakwata ni kile kilichofanyika Iringa tarehe 13 Desemba 1968, ambacho kilifunguliwa na kufungwa na Abeid Aman Karume na Rashid Kawawa. Hautuambii kuhusu mchango na uhasama wa Sheikh Abdallah Chaurembodhidi ya EAMWS. Hautuambii kuwa Sheikh Hassan hakuwa Khalifa na hakutambuliwa kama sehemu ya Tariq na viongozi wa Sufi wakati Sheikh Abdallah Chaurembo alikuwa kiongozi katika order ya Shadhili. Maana yake Sheikh Chaurembo hakuwa zezeta wa kuburuzwa ovyo ovyo na mkatoliki Julius Nyerere. Yeye na wenzake waliipinga EAMWS kwa misingi ya uzalendo, walikiona kama chombo cha mabepari wa kihindi na kiarabu. Hawa ndio waliouwa EAMWS na sio mkatoliki Julius Nyerere.

Amandla......
Mkuu wangu muda wote sikutaka kabisa kuandika haya lakini maadam umeyaweka bayana nadhani Mohamed Said atanielewa vizuri nilichokuwa nikisisitiza toka huko nyuma kwani haya yote sikuyasoma mahala isipokuwa niliambiwa na mtu wa Uhakika, kiongozi wa dini ambaye maisha yake alishindwa kuelewa Unafiki wa Waislaam inapofikia issues zinazowahusu Waislaam.....Ndio wa kwanza kubomoa kisha hutafuta mchawi.
 
FM: Ahsane kwa mchango wako. Waziri wa Mambo ya Ndani alikuwa Said Maswanya. Naheshimu fikra zako teundelee na mjadala.
 
Safari: Ahsante kwa mchango wako lakini mbona una hamaki nimekuudhi kitu gani ndugu yangu? Hiyo lugha ya kutuniza "limejaa" lugha ya mtu aliyeghadhibika. Lugha ya kiungwana ingekuwa "kimejaa."

Kitabu changu kinaitwa: "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 -1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika." Hiki ni kitabu kinachoelezea maisha ya Abdulwahid Sykes na zile nyakati alizoishi yaani miaka ya 1920 hadi miaka ya 1960. Sasa hapa kama sikueleza maisha yake ningeeleza kitu gani? Kisha kitabu kinachambua mchango ambao ulikuwa haujaelezwa wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Sasa kama singeeleza habari za Uislam na Waislam ningeandika kitu gani? Ni hivyo tu. Nadhani umenielewa. "Historia ya TANU" ni kitabu kinachoeleza habari za TANU na jinsi chama kilivyoanzishwa. Kichekesho ni kuwa waandishi wa Chuo cha Kivukoni "wakamsahau" Abdulwahid Sykes ambae hicho chama chenyewe mikutano yake ya siri kuanzia 1950 hadi siku wanakianzisha rasmi tarehe 7 Julai 1954 ilikuwa ikifanyika nyumbani kwake na yeye akiwa kiongozi. Acha hilo hata hiyo nyumba yenyewe iliyoasisiwa chama chenyewe ilijengwa na baba yake. Kitabu kinamtaja Nyerere peke yake kama ndiye muaisisi. Kwa bahati mbaya au nzuri Nyerere nae hakuwakumbusha au kuwaeleza kuwa TANU nimeikuta nilipokuja Dar es Salaam 1952. Hapa ndipo nikaona iko haja ya kuandika kitabu na kueleza kisa kizima cha historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ntakuongezea kitu kingine. Nimeandika kitabu kingine "Torch on Kilimanjaro" Oxford University Press, Nairobi 2006. Humo kajaa Mwalimu Nyerere.
Mohammed,
Just a point of order. Nyerere hakuikuta TANU Dar-es-Salaam mwaka 1952 kama TANU ilianzishwa 1954.
 
Kasella Bantu ndiyo mtu aliyempeleka Julius Nyerere kwa Abdulwahid kumtambulisha. Hii ilikuwa mwaka wa 1952. Bantu na Nyerere walifahamiana toka huko nyuma walipokuwa wakifundisha Tabora. Chama hakiwezi kupinga ukweli kwamba Kasella Bantu alikuwa miongoni mwa wale wanachama 17 waasisi wa TANU. Hali kadhalika chama hakiwezi, kupinga ule ukweli wa historia kuwa Kasella Bantu alishiriki katika ìkuandikaî ile katiba ya TANU. Kasella Bantu anakerwa sana na kupotoshwa kwa historia. Kila alipopata fursa kuanzia alipokuwa ng'ambo uhamishoni na hata baada ya kurudi nyumbani kutoka uhamishoni, Kasella Bantu ameeleza kuhusu mambo haya mawili ya kihistoria, kuwa aliandika katiba ya TANU na ni mmoja wa waasisi wa TANU. Bantu kama waanzilishi wengine wengi anahisi kwamba mchango wake katika harakati za uhuru wa Tanganyika haujathaminiwa.
Mimi nilidhani Julius Nyerere alikuwa na usongo na waislamu peke yao. Sasa huyu Kasella Bantu naye alikuwa muislamu?

Amandla....
 
Jasusi: Nimekisoma kitabu cha Mbogoni na wakati anafanya utafiti alikujanihoji na akanipiga picha mbele ya Msikiti wa Manyema. Kitu kilichotustaajabisha ni kuwa kitabu cha Mbogoni kiliruhusiwa kuingia nchini lakini cha Hamza Njozi "Mwembechai Killings" kikapigwa marufuku.
 
Na kama Nyerere aliyejaa kwenye "Torch on Kilimanjaro" ni huyu huyu Nyerere unayemzungumzia basi sina hata shauku ya kusoma hicho kitabu.
 
Jasusi: Nimekisoma kitabu cha Mbogoni na wakati anafanya utafiti alikujanihoji na akanipiga picha mbele ya Msikiti wa Manyema. Kitu kilichotustaajabisha ni kuwa kitabu cha Mbogoni kiliruhusiwa kuingia nchini lakini cha Hamza Njozi "Mwembechai Killings" kikapigwa marufuku.
Aliyepiga marufuku kitabu cha Hamza Njozi ni Benjamin Mkapa. Lakini huyu hajaitwa mnafiki na waislamu kwa kuwapa lile jengo la Tanesco Morogoro wakajenge chuo chao. Nimekisoma pia kitabu cha Njozi kwenye internet.
 
FM: Ahsane kwa mchango wako. Waziri wa Mambo ya Ndani alikuwa Said Maswanya. Naheshimu fikra zako teundelee na mjadala.

Kumbe ulikuwa unamjua! Asante kwa kunisahihisha.

Sasa Waziri wa Mambo ya Ndani, Said Maswanya alikuwa mkristu au mkatoliki?

Amandla........
 
Jasusi: Ahsante kwa mchango wako. Nakuwekea kipande hiki hapa chini:

It was at Imphal towards the end of the war that Abdulwahid and the rest of the Burma infantry sat down to reflect on their own war experience and the future of Tanganyika. It was decided that the Burma infantry from Tanganyika forming the 6th Battalion should form the base for a future political party to fight for independence. This was agreed. The Burma infantry from Tanganyika should form the base for a future political party to free the country through popular mass action. The name of the political party was to be Tanganyika African National Union (TANU). Ally Sykes remembers that Abdulwahid wrote the name of the proposed party in his diary. The Burma infantry was also aware that back home there was the African Association fighting for African rights. Abdulwahid knew a great deal about the association because his own father was its founding secretary. How the intended party was to be incorporated in the African Association, was not, however, discussed.

TANU as a political movement had always existed in Abdulwahid's mind and he persistently and constantly worked for its realisation. A party to unite all the people of Tanganyika irrespective of their ethnic identity or religious affiliation was now a reality. Abdulwahid and the TAA leadership had planted the seeds of unity in Tanzania. If that unity was to be destroyed soon after independence the founding fathers are not to blame. The TANU inaugural meeting was attended by a small crowd of about twenty people, among them Julius Nyerere, Abdulwahid and Ally Sykes, Dossa Aziz, Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajab Diwani, Schneider Plantan, Marsha Bilali, Rashidi Ally Meli, Frederick Njiliwa Idd Faiz Mafongo, Idd Tulio, Denis Phombeah and others. Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz and Rupia were the main financiers of the movement in Dar es Salaam.

Sasa ukileta fikra ya kuwa TANU ilianza 1954 na Nyerere tayari ushakaribisha matatizo.
 
Nafurahi umetuwekea kipande hiki. Pale nilipo bold ndio hasa chimbuko la msimamo na mtizamo wa Abdulwahid. Nilipokutana naye mara ya kwanza nikiwa mwanafunzi pale Aga Khan ( leo Tambaza) nilimwambia natoka Musoma alinieleza jinsi alivyomkarimu Mwalimu Nyerere alkipofika Dar-es-Salaam. Akaniambia kuwa walimkaribisha Nyerere na yeye alifurahi kumwachia kiti cha uongozi kwa sababu huyu alionekana kuwa na azma ya kusaidia ukombozi wa Afrika, hasa Afrika kusini. Alisema tulijua Nyerere atasaidia katika harakati za ukombozi wa Afrika kusini. Na kama leo ningeandika kumhbukumbu zangu za marehemu Abdulwahid ningelitaja hilo kwa sababu ni jambo ambalo siwezi kusahau. Na kuna mahali niliwahi kuandika baada ya kifo cha Julius Nyerere, nikasema, kama atakutana na Abdulwahid Sykes huko ahera atamwambia, Abdu, ile kazi mliyonituma, nimeikamilisha.
 
JK: Ahsante kwa mchango wako. Kuna mmoja wa watu wa karibu sana na Mwalimu alijitolea kunifanyika miadi na Nyerere nilipomueleza kuwa naandika kitabu cha Abdu Sykes. Juhudi zake hazikufanikiwa. Mchango wa Nyerere nimeueleza kwa kirefu katika kitabu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom