Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kabonde: Ahsante kwa mchango wako. Hivi ndivyo dunia ilivyo si wakati wote ukweli utakubalika. Usinisome sawa lakini baada ya kusoma haya ulosoma ukumbini nakushauri kasome "Historia ya TANU 1954 - 1977" kitabu kilichoandikwa na Chuo Cha Kivukoni. Jasho litakumwagika jepesi. Kama mimi unaniona ni "mdini" basi hao wenzangu ni "wanyerere." Kitabu chao ni kisa cha "Superman" mbabe aliekuwa na uwezo wa kuibeba gorofa nzima akarukanayo angani. Mwanzo wa kurasa hadi mwisho ni Nyerere tu kiasi kitabu kinakuwa sawa na mchuzi ulochujuka. Ila nakushauri kisome kitabu changu ndipo utakuwa katika hali ya kunijua na kuujua upande mwingine wa mwezi.
Waziri wa Mambo ya Ndani kwa kuamriwa na Rais anatangaza kuwa tawi la Tanzania la East African Muslim Welfare Society na Baraza la Tanzania la la East African Muslim Welfare Society ni jumuiya zisizotambulika kisheria chini ya kifungu 6 (i) cha Sheria ya Vyama. Kwa tangazo hilo la Rais wa Tanzania, Julus Nyerere, Waislam walinyimwa nafasi ya kukutana na kuzungumza kuhusu tatizo ambalo kwa kweli liliwahisu Waislam peke yao. Kwa ajili hii basi Waislam walinyimwa nafasi ya kujadili na kulitolea uamuzi tatizo
hilo.
Tarehe 27 Aprili, 1985 Julius Kambarage Nyerere, sasa akijulikana kama Baba wa Taifa, katika sherehe kubwa katika viwanja vya Ikulu, alitoa jumla ya medali 3979 kwa Watanzania waliochangia katika maendeleo ya taifa. Kati ya wale ambao walipewa medali hizo alikuwa Sheikh Abdallah Chaurembo.
Wazalendo waliotajwa ndani ya kitabu hiki ambao walipigania uhuru wa Tanganyika, hakuna hata mmoja wao aliyekuwa katika orodha ile ya heshima. Baada ya siku chache kupita, Nyerere kama mtu aliyegutuka alimualika Dossa Aziz Ikulu. Dossa Aziz, wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alikuwa mtu maarufu, mwenye nafasi, na kujiweza sana. Sasa Dossa baada ya miaka kupita hakuwa akifahamika tena na ule umaarufu na utajiri wake ulikuwa umetoweka. Alikuwa akiishi maisha ya kawaida kijijini Mlandege, maili chache nje ya Dar es Salaam. Katika sherehe ya faragha Nyerere alimtunukia medali Dossa Aziz, rafiki yake wa zamani.
Mkuu wangu muda wote sikutaka kabisa kuandika haya lakini maadam umeyaweka bayana nadhani Mohamed Said atanielewa vizuri nilichokuwa nikisisitiza toka huko nyuma kwani haya yote sikuyasoma mahala isipokuwa niliambiwa na mtu wa Uhakika, kiongozi wa dini ambaye maisha yake alishindwa kuelewa Unafiki wa Waislaam inapofikia issues zinazowahusu Waislaam.....Ndio wa kwanza kubomoa kisha hutafuta mchawi.Mimi ndiyo maana nakuita mchochezi. Kwa mtu anayedai kuwa alifanya utafiti wa kina, unashindwaje kutaja jina la huyo waziri ya mambo ya ndani? Au kwa vile aliitwa Omari Muhaji, muislamu mwenzako, ndiyo ugumu unaingia? Ugumu ambao haunao inapokuja kwa Julius Nyerere. Unadai kuwa Mwalimu kama rais alitoa tangazo wakati hapo hapo unasema kuwa alimuagiza waziri muislamu atoe tangazo hilo, sasa tuamini lipi? Kuwa tangazo lilitoka kwenye ofisi ya Rais au kwa waziri wa mambo ya ndani? Tangazo hilo, ingawa lilisema limefuata maagizo ya rais lakini halikuwa la Rais. Ungetaka kuwa sahihi, ungesema tangazo lillilotolewa na Omari muhaji kwa niaba ya Julius Nyerere.
Unainsinuate kuwa chanzo cha uhasama wote dhidi ya EAMWS ni Mwalimu na unashindwa kabisa kukiri kuwa mamlaka ya kwanza kufungia shule za EAMWS ilikuwa ni serikali ya Mapinduzi Zanzibar, iliyojaa waislamu watupu. Hautaki kuzungumzia mchango wa Abeid Aman Karume katika kifo cha EAMWS. Haumzungumzii Adam Nasibu, kiongozi wa tawi la EAMWS, Bukoba aliyetangaza mkoa wake kujitoa kutoka EAMWS mwezi Oktoba 1968, akifuatiwa na tamko la Sheikh Juma Jambia wa Tanga kujitoa na hatimaye mikoa 9 kati ya 17 kujitoa EAMWS ilipofika Desemba 1968. Hautuambii kuwa kikao kilichoanzisha bakwata ni kile kilichofanyika Iringa tarehe 13 Desemba 1968, ambacho kilifunguliwa na kufungwa na Abeid Aman Karume na Rashid Kawawa. Hautuambii kuhusu mchango na uhasama wa Sheikh Abdallah Chaurembodhidi ya EAMWS. Hautuambii kuwa Sheikh Hassan hakuwa Khalifa na hakutambuliwa kama sehemu ya Tariq na viongozi wa Sufi wakati Sheikh Abdallah Chaurembo alikuwa kiongozi katika order ya Shadhili. Maana yake Sheikh Chaurembo hakuwa zezeta wa kuburuzwa ovyo ovyo na mkatoliki Julius Nyerere. Yeye na wenzake waliipinga EAMWS kwa misingi ya uzalendo, walikiona kama chombo cha mabepari wa kihindi na kiarabu. Hawa ndio waliouwa EAMWS na sio mkatoliki Julius Nyerere.
Amandla......
Mohammed,Safari: Ahsante kwa mchango wako lakini mbona una hamaki nimekuudhi kitu gani ndugu yangu? Hiyo lugha ya kutuniza "limejaa" lugha ya mtu aliyeghadhibika. Lugha ya kiungwana ingekuwa "kimejaa."
Kitabu changu kinaitwa: "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 -1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika." Hiki ni kitabu kinachoelezea maisha ya Abdulwahid Sykes na zile nyakati alizoishi yaani miaka ya 1920 hadi miaka ya 1960. Sasa hapa kama sikueleza maisha yake ningeeleza kitu gani? Kisha kitabu kinachambua mchango ambao ulikuwa haujaelezwa wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Sasa kama singeeleza habari za Uislam na Waislam ningeandika kitu gani? Ni hivyo tu. Nadhani umenielewa. "Historia ya TANU" ni kitabu kinachoeleza habari za TANU na jinsi chama kilivyoanzishwa. Kichekesho ni kuwa waandishi wa Chuo cha Kivukoni "wakamsahau" Abdulwahid Sykes ambae hicho chama chenyewe mikutano yake ya siri kuanzia 1950 hadi siku wanakianzisha rasmi tarehe 7 Julai 1954 ilikuwa ikifanyika nyumbani kwake na yeye akiwa kiongozi. Acha hilo hata hiyo nyumba yenyewe iliyoasisiwa chama chenyewe ilijengwa na baba yake. Kitabu kinamtaja Nyerere peke yake kama ndiye muaisisi. Kwa bahati mbaya au nzuri Nyerere nae hakuwakumbusha au kuwaeleza kuwa TANU nimeikuta nilipokuja Dar es Salaam 1952. Hapa ndipo nikaona iko haja ya kuandika kitabu na kueleza kisa kizima cha historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Ntakuongezea kitu kingine. Nimeandika kitabu kingine "Torch on Kilimanjaro" Oxford University Press, Nairobi 2006. Humo kajaa Mwalimu Nyerere.
Mimi nilidhani Julius Nyerere alikuwa na usongo na waislamu peke yao. Sasa huyu Kasella Bantu naye alikuwa muislamu?Kasella Bantu ndiyo mtu aliyempeleka Julius Nyerere kwa Abdulwahid kumtambulisha. Hii ilikuwa mwaka wa 1952. Bantu na Nyerere walifahamiana toka huko nyuma walipokuwa wakifundisha Tabora. Chama hakiwezi kupinga ukweli kwamba Kasella Bantu alikuwa miongoni mwa wale wanachama 17 waasisi wa TANU. Hali kadhalika chama hakiwezi, kupinga ule ukweli wa historia kuwa Kasella Bantu alishiriki katika ìkuandikaî ile katiba ya TANU. Kasella Bantu anakerwa sana na kupotoshwa kwa historia. Kila alipopata fursa kuanzia alipokuwa ng'ambo uhamishoni na hata baada ya kurudi nyumbani kutoka uhamishoni, Kasella Bantu ameeleza kuhusu mambo haya mawili ya kihistoria, kuwa aliandika katiba ya TANU na ni mmoja wa waasisi wa TANU. Bantu kama waanzilishi wengine wengi anahisi kwamba mchango wake katika harakati za uhuru wa Tanganyika haujathaminiwa.
Aliyepiga marufuku kitabu cha Hamza Njozi ni Benjamin Mkapa. Lakini huyu hajaitwa mnafiki na waislamu kwa kuwapa lile jengo la Tanesco Morogoro wakajenge chuo chao. Nimekisoma pia kitabu cha Njozi kwenye internet.Jasusi: Nimekisoma kitabu cha Mbogoni na wakati anafanya utafiti alikujanihoji na akanipiga picha mbele ya Msikiti wa Manyema. Kitu kilichotustaajabisha ni kuwa kitabu cha Mbogoni kiliruhusiwa kuingia nchini lakini cha Hamza Njozi "Mwembechai Killings" kikapigwa marufuku.
FM: Ahsane kwa mchango wako. Waziri wa Mambo ya Ndani alikuwa Said Maswanya. Naheshimu fikra zako teundelee na mjadala.
Mohammed,Jasusi: Ahsante kwa mchango wako. Nakuwekea kipande hiki hapa chini:
It was at Imphal towards the end of the war that Abdulwahid and the rest of the Burma infantry sat down to reflect on their own war experience and the future of Tanganyika. It was decided that the Burma infantry from Tanganyika forming the 6th Battalion should form the base for a future political party to fight for independence. This was agreed. The Burma infantry from Tanganyika should form the base for a future political party to free the country through popular mass action. The name of the political party was to be Tanganyika African National Union (TANU). Ally Sykes remembers that Abdulwahid wrote the name of the proposed party in his diary. The Burma infantry was also aware that back home there was the African Association fighting for African rights. Abdulwahid knew a great deal about the association because his own father was its founding secretary. How the intended party was to be incorporated in the African Association, was not, however, discussed.
TANU as a political movement had always existed in Abdulwahid's mind and he persistently and constantly worked for its realisation. A party to unite all the people of Tanganyika irrespective of their ethnic identity or religious affiliation was now a reality. Abdulwahid and the TAA leadership had planted the seeds of unity in Tanzania. If that unity was to be destroyed soon after independence the founding fathers are not to blame. The TANU inaugural meeting was attended by a small crowd of about twenty people, among them Julius Nyerere, Abdulwahid and Ally Sykes, Dossa Aziz, Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajab Diwani, Schneider Plantan, Marsha Bilali, Rashidi Ally Meli, Frederick Njiliwa Idd Faiz Mafongo, Idd Tulio, Denis Phombeah and others. Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz and Rupia were the main financiers of the movement in Dar es Salaam.