Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kumbe Mkuu haukujua kuwa huko walikotokea wakina Dr. William Mwanjisi, Mzee John Mwakangale, Mzee Japhet Kirilo aliyesimamia kidete kesi ya mgogoro wa adhi wa wameru. Na wengine waliotoka nje ya mikoa unayoijua wewe ni wakina Mzee Joseph Kimalando kutoka Moshi ambaye amehusika katika harakati za kupinga ukoloni toka miaka ya 1930s akiwa ameajiriwa kwenye shirika la reli Tanganyika, mhehe Julius Mwasanyaji, mhindi Amir Jamal kutoka Morogoro, Frank Humplick na dada zake Mary na Regina ambao nyimbo zao ndizo zilitumika kuhamasisha wana TANU. Hata huko Tanga kwenye waislamu wengi, mchango wa Stephen Mhando na mdogo wake Peter Mhando katika kuhamasisha wabondei hauwezi kudharauliwa! ( kutoka " Nyerere and Africa: End of an era cha Godfrey Mwakikagile"). Na hawa ni sehemu ndogo tu ya waliohusika katika mapambano hayo. Ukweli nikuwa sehemu za pwani bila kuungwa mkono na sehemu nyingine za Tanganyika zisingefua dafu mbele ya mkoloni. Wote walihusika, tofauti na unavyotaka kutuaminisha.
Amandla.........
MOHAMME SAID AKAJIBU HIVI:
FM: Pole sana ndugu yangu. Mwakikagile amenakili kazi yangu. Ungesoma kitabu changu ungestaajabu na kusema mbona hii kama inatoka kitabu cha Mohamed Said? Ndiyo maana nikikusisitizia kuwa soma kwanza kitabu ndipo utakuwa katika hali nzuri ya kufanya majadiliano. Mwakikagile si wa kwanza kufanya hivyo watu wengi sana wanatumia kazi zangu kama zao na mimi ninafuata mila ya Kiislam kuwa elimu na taalamu haviuzwi kwa hiyo hata mtu akichukua kazi yangu akaitumia huwa kwangu si kitu hata kama hakunitaja.
NA WEWE FUNDI NCHUNDO UKAJIBU HIVI:
Cha msingi hapa ni je anayosema ni uongo? Kuwa hao wote hawakuhusika katika jitihada za kugombea uhuru? Kama Mwakikagile amenakili kazi yako na yote alioyaandika yamo kwenye kitabu chako basi huu si ushahidi tosha kuwa hata wewe unajua kuwa walihusika wengi katika kudai uhuru na sio waislamu au wakina Sykes au wazee wako peke yako? Kama ukweli huu unaujua na umeuandika kwenye kitabu chako kwa nini basi kwenye mihadhara yako hausemi hivyo bali unashikilia kuwa ni waislamu PEKE YAO ndio waliohusika katika mpambano huo na wakristu walibebwa tu? Na kama Mwakikagile amenakili kazi yako bila kukutaja kwa nini basi usimpleke kwa Pilato maana plagiarism ni kosa kubwa sana!! Lakini kama amekunukuu na kukutaja, hiyo ni kawaida katika uandishi kama wewe mwenyewe jinsi ulivyonukuu kazi za wengine. Mimi nimekuambia tangu mwanzo kuwa maandishi yako yanakushitaki maana humo humo una-refute haya unayoyasema hadharani kwa wale ambao ni wavivu wa kufikiri.
Amandla.......
UCHAMBUZI WANGU-AMI
Pamoja na kwamba hutaki kukiri makosa yako katika huu mjadala,kwamba kwa kutokukisoma kitabu cha Mohammed kwanza kama ambavyo amekusisitiza mara nyingi halafu ndio ukaja kuchangia,umekuwa ukichanganya sana.
Mimi nililoliona hapa katika majibu yako ni kuwa wewe na Lole mumekubali kuwa si kweli kwamba Mohammed Said katika utafiti wake amekuwa akiwataja waislamu pekee.
Kumbuka,hapa hukuwa na jibu kuonesha kinyume chake Mohammed aliposema kuwa Mwakikagile amenakili kazi yake.Badala yake umerukia jee hayo yaliyosemwa na Mwakikagile ni uongo?.
Jibu ni kuwa ni kweli ndio maana Mohammed akaandika kama alivyoona kuwahusu wao na kuwahusu waislamu walio wengi.