Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 15,460
- 24,233
Nenda popote zao la immigrants second generation au first generation huwa linafanya vizuri..., sababu wazazi wamepata shida wana-instill kujituma kwa watoto wao hivyo wenzao wakitembea wao wanakimbia.., trust me ubaguzi waliofanyiwa na kubaniwa opportunities watu weusi huko USA inachukua muda kuondoka..., na mentality ndio hio kwamba hata wakijitahidi hawatapata opportunities same as whites (ndio maana wengi walijikita kwenye michezo n.k.), sababu their role models ndio walifanya vyema / kufanikiwa huko....Fact ila hao Black America nimewatolea mfano kwa kushindwa kubadili mindset zao na kuchukua advantage ya kufanya mambo makubwa kulinganisha na eneo walilopo tofauti na Mazingira yetu ndio maana napata hitimisho la race kama race na Sio Mazingira nj some na sisi tuna Rasilimali chungu nzima ila sasa kuzitumia kwa manufaa ni mtihani mkuu!
Sio rangi inayomfanya mtu afanikiwe au adumae ni culture / utamaduni..., kwahio hata sisi huku mambo ya kuamini vitu vimepangwa na mungu, kushikana uchawi na kutegemea mwanasiasa ndio atutoe hapa kutupeleka pale inatudumaza..., kizazi kikizaliwa na watu kama kina Diamond wote watataka kuwa kama Diamond na kuingia kwenye usanii..., Kizazi kikizaliwa na kujiuliza na kujaribu kuboresha (age of enlightenment) utapata thinkers na watu wanaotaka kuboresha....
Kizazi kikizaliwa kwamba wale HAMAS ni wabaya au hawa Israel ni wabaya n.k. utapata kizazi cha chuki na kulipizana visasi...
Kizazi kikizaliwa kwa kuona kwamba wizi / ufisadi ndio ujanja na siasa ni biashara ya kupata kura ili kwenda kula utapata kizazi cha watu walaghai..., kizazi kikizaliwa kwamba tunahitaji wawekezaji na sisi hatuna akili kitu atafanya ajaye utapata watu tegemezi....
Yote hayo ni utamaduni (the way we do things around here) na kutoka kwenye mentality moja mpaka nyingine itachukua generations na in black americans case mabadiliko ya leo huenda matokea yake ni generation nne zijazo....