Ukweli Mchungu: Haji Manara ni mkubwa kuliko TFF

Ukweli Mchungu: Haji Manara ni mkubwa kuliko TFF

Boss la DP World

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2021
Posts
2,318
Reaction score
8,464
Huu ndiyo ukweli Mchungu
1. Watanzania wengi wanamjua Haji Manara na hawaijui TFF wala viongozi wake.

2. Haji Manara amechangia uhamasishaji wa watu kupenda soka, nakumbuka kipindi kile akiwa Simba na Jerry Muro akiwa Yanga ilikuwa burudani murua sana.

3. Japo Haji amefungiwa lakini namsihi aendelee kujihusisha na soka kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii na afungue channel ya michezo ya YouTube.

4. Taasisi kama TFF ingekuwa na ushawishi tungeona Ina followers wengi online lakini followers wa kurasa zote za TFF ukizijumlisha hazifikii hata robo ya followers wa Haji kwenye mtandao wa Instagram sasa hapo Kuna ukubwa gani?

5. Siku ya Mwananchi MC wa tukio ni Haji Manara na hapangiwi chakusema na wapuuzi wapuuzi. Siku hiyo ndo utaona ukubwa wa Haji ukilinganisha na tiefuefu.

6. Ndugu yangu Majaliwa wewe ndiye uliyemwingiza Karia madarakani hapo TFF, si unakumbuka simu ile ya sikuile? Unamkumbuka aliyekupa hayo maelekezo? Sasa umpigie simu Karia leo mwambie mambo yamebadilika.

7. Haji Manara usifuate uamuzi huu wa wahuni, endelea kutupa raha bila kutetereka, nyuma yako kuna ulinzi mkubwa wa wananchi.

NB: Baada ya uamuzi huu, Followers zaidi ya 40,000 wameongezeka kwa Haji Manara, hapo Kuna watu wanatanani kuwa unfolisha wote😂😂😂
 
Bro Bei Elekezi huyu Haji Manara haijapita hata miaka miwili (2yrs) toka alipishwe ile faini ya 5m mwaka 2020 akiwa Simba SC Tanzania.

Yeye na Hassan Bumbuli kama wakumbuka walitakiwa wasiwe watovu wa nidhamu in 2yrs.

Je, miaka hyo miwili imepita? Hongera @Tanfootball kwa kusimamia nidhamu
 
Bro Bei Elekezi huyu Haji Manara haijapita hata miaka miwili (2yrs) toka alipishwe ile faini ya 5m mwaka 2020 akiwa Simba SC Tanzania. Yeye na Hassan Bumbuli kama wakumbuka walitakiwa wasiwe watovu wa nidhamu in 2yrs. Je miaka hyo miwili imepita? Hongera @Tanfootball kwa kusimamia nidhamu
Sasa kwani safari hii kafanya kosa gani?
 
Sisi huku Pwani hata ukinitukana au kunivunjia heshma naweza kukuomba radhi bila shida yoyote

si ajabu msaidizi wako ofisin sometime kumuita 'Mkuu'


wahenga husema 'hewallah si utumwa'
Kama alikwenda kuomba msamaha nyumbani kwa Karia na Eng Hersi Ina maana analijuwa kisa lake. Huwezi kuomba kusamehewa kama hujakosa
 
Wewe na manara wote ni punguani wahedi mtu timamu hawezi kesha mitandaoni kama manara kupost utumbo badala ya kupost content za maana kwa siku anapost mara 30 halafu post zote utumbo yaani 30×30=900 hakuna mtu mwenye akili anafanya hvyo sema kwa vile watanzania tunapenda ujinga kuliko nchi yoyote africa ndo maana tunamuona manara wa maana sana.
 
Haji amezaliwa na roho ya kukubaliwa, hatuwezi kushindana na karama ya mtu
 
Back
Top Bottom