Ukweli Mchungu: Haji Manara ni mkubwa kuliko TFF

Haji Manara ni mkubwa kuliko Yanga ndiyo maana licha ya matusi yote aliyowatukana bado mnamnyenyekea hata kwenye mambo yake ya kipumbavu bado mnamuunga mkono. Kweli nyie ni wapuuzi
 
Hilo ni kweli. Lakini Je umaarufu wake ni kinga dhidi ya uvunjaji sheria!? Sheria ya kubagua hadhi ya mtu haipo Duniani. Kama anaamini hakustahili hiyo adhabu basi akate rufaa.
 
Kosa gani kafanya?? Kukibishana na karia ndo apigwe nyundo mbili na mil 20?? Huoni kuwa ni adhabu ya kukomoa??
 
Kwa hiyo unamfuatilia?? Ndege wafananao
 
Watz tunapenda udaku sana ndo maana ana follow wengi.

Unataka kusema raisi samia, JK kuna mtu hamjui lakini kazidiwa follower na wengi sana.
 
Nakazia 🤣🤣🤣
 
Nashauri Sisiemu iwe makini sana hapa; usikute ukawa mkakati wa Hajj Manara kutafuta kuigawa makundi kama yale ya 2015.
 
Huu ndiyo ukweli Mchungu
1. Watanzania wengi wanamjua Haji Manara na hawaijui TFF wala viongozi wake.
Aisee, kumbe kipimo cha ukubwa ni kujulikana na watu wengi? Hapa mtaani kuna kichaa mmoja, sidhani kama kuna kaya yoyote haina walau mtu mmoja anayemjua. Lakini Mkuu wa wilaya hata mimi simjui! Labda kwa mtazamo wako huu, huyo kichaa ni mkubwa kuliko DC !

NB: post ya mleta uzi inazidi kudhihirisha kuwa ni wawili tu, JK na Baba yake Haji tu
 
Wenye akili husoma andiko lote
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…