Ukweli Mchungu: Halima Mdee hawezi kukubalika kwa wanachama wa CCM ndani ya CCM

Atakubalika sana na kupewa UENYEKITI wa UWT Taifa
 
Kwani akihamia ccm,kiti cha ubunge viti maalumu kwa tiketi ya chadema atakipata?
 
Chadema ina hazina kubwa Sana ya wanawake kwa hiyo usitegemee Halima ameacha pengo lolote. Waliondoka akina Dr Slaa, Zitto, Kitila, N.k lakini Chadema bado imekuwa tishio
Sasa kama chadema inahazina nyingi, kwa nini bado munawaota hawa wamama wasio na chama chochote??
 
Wampokee tu, kwasasa she is no longer the same.
 
Ameshajimaliza.
 
Tofauti yake ni nini?
Mwanasiasa lengo lake kuu ni kushinda uchaguzi ili akatekeleze sera za itikadi ya chama chake wakati mwanaharakati lengo lake kuu ni kupigania kubadili sera za kitaifa kwa ujumla na mara nyingi anatakiwa asiwe na itikadi ya chama chochote, lkn kwa hali ya sasa ni vigumu sana kuwatenganisha.

Mwanaharakati yuko tayari kufa kwa anachokitetea wakati mwanasiasa hayuko tayari kufa kwa anachokitetea anaweza kubadilika au kubadili itikadi.
 
Kama mliweza kumpokea LIJUALIKALI basi mnaweza kupokea chochote. Tetesi zinadai huyo anayejiita mwendawazimu bado ana nafasi nne za viti maalum. Hivyo katika COVID19 wane wataambulia hivyo viti Mzee Halima, Bulaya, Matiko na mwingine. Tetesi pia zinadai Bashite mfoji vyeti anachukua nafasi ya Chakubanga.
 
Hiyo option ya kwanza ndo nzuri zaidi.

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
Sasa tupe mfano wa mwanasiasa wa Upinzani aliyehamia CCM na akakubalika hadi kugombea Uraisi.

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
Halima ameweka kuiimarisha Bawacha kuwa jumuia bora ya kinamama, ukizingatia pesa za Chadema si kama za CCM. Iwapo atakabidhiwa UWT chama chenye matawi mpaka vitongojini Tanzania nzima. Ataleta mabadiliko makubwa.

Wasichana wengi vyuoni watajiunga na CCM kupitia UWT. Halima ni mbunifu, mtekelezaji na anajitambua.
 
Ndivyo unavyojidanganya.

Sent from my TECNO WX3 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…