Kama unafahamu na kutofautisha matendo ya Mbowe na Lissu, hapo ni rahisi kuona mwanasiasa na mwanaharakati katika siasa.
Wate hao ni viongozi wakuu wa CHADEMA, ila mmoja ametulia anajibu hoja kwa hoja, bila ya jaziba na anakuwa na msisitizo kwa kile anacho kiamini - pia anatumia ushawishi kusudi wale ambao hawaoni kama yeye nao wafumbuke macho wamfuate. Wakati huo huo mwingine analazimisha watu wamfuate yeye - la sivyo ataitisha mgomo, atawashitaki kwenye vyombo vya kimataifa, ataswaga watu barabarani! Ukikataa maoni yake anakutukana matusi kibao! Akishindwa kumconvice mtu anazira, anasaga meno na kukimbilie nje! Anatumia mbinu za ulaghai na hasa anapenda kufadhiliwa na kutumia hela za wanaomtuma!
Ukiwaelewa hao watu wawili mashuhuri wa CHADEMA, utakuwa umeelewa tofauti kati ya mwanasiasa na mwanaharakati!
Mbowe = mwanasiasa
Lissu = mwanaharakati