Ukweli mchungu: Je, ni kila mtu anayestahili kusaidiwa?

Ukweli mchungu: Je, ni kila mtu anayestahili kusaidiwa?

Joined
Oct 5, 2026
Posts
31
Reaction score
51
Katika jamii zetu, tumefundishwa kusaidiana tunapokuwa na uwezo. Lakini kuna swali ambalo watu wengi hawapendi kulijadili: Je, ni kila mtu anapaswa kusaidiwa?

Wapo watu wanaosaidiwa mara nyingi lakini hawajifunzi kujitegemea. Wengine wanapewa mitaji, wanaharibu, kisha wanarudi kuomba msaada mwingine. Wapo pia wanaokataa kubadilika licha ya kupewa nafasi nyingi za kufanya hivyo.

Kwa upande mwingine, kuna watu wanaopitia magumu si kwa sababu ya uvivu, bali kwa kukosa fursa, mitaji au mazingira mazuri.

Sasa, je, tunapomsaidia mtu ambaye hataki kujisaidia, tunakuwa tunamsaidia kweli au tunamfundisha kutegemea wengine?

Na je, kuna wakati ambapo kumkatalia mtu msaada ndiyo njia bora ya kumfanya ajifunze kuwajibika?

Ningependa kupata maoni yenu kwa hoja, si kwa hisia.

Maswali ya mjadala:

  • Je, msaada unapaswa kutolewa kwa kila mwenye uhitaji au kwa wale wanaoonyesha juhudi za kujikwamua?
  • Unapaswa kuendelea kumsaidia mtu anayekosea mambo yale yale kila unapomsaidia?
  • Kuna tofauti gani kati ya mtu anayeshindwa kujisaidia na mtu ambaye hataki kujisaidia?
  • Je, kukataa kumsaidia mtu ni ubinafsi au ni kuweka mipaka?
 
Baba aliwahi nambia usikubali kuomba msaada kwa mtu yupo kama wewe, jifunze kutafuta vyako sio kusubiri kupatiwa na mwenzako.

Msaada unaopewa leo utakuja kudhalilishwa kesho, maneno ya mzee yalikuwa 100%
 
Back
Top Bottom