Ukweli mchungu kuhusu KINANA

ni kinana gani unae mzungumzia wewe....ni huyu wa magamba au yule wa tembo......

ni huyu huyu aliefanya ziara mkoano morogoro akawapasha machadema hadi yakaamua kumchafua kwa uzushi na uongo..ni huyu huyu ambaye kibanda alimsifia ndipo magaidi akina lwakatare wakamteka na kumtesa
 
Akiwa katika ziara ya kikazi mkoani morogoro, kinana aliingiza wanachama wapya 4000 kutoka vyama mbalimbali vya siasa na katika kuhitimisha ziara hiyo alitoa hotuba kali na ya kusisimua huku akiwananga machadema kuwa waache utoto na siasa za visasi na zaidi waache kupanga mauaji.kitendo hicho kiliwaudhi na kuwaghadhibisha chadema na hivyo kuamua kumuundia zengwe la kashfa
 

We ni raia wa nchi gani unaposema Watanzania wana akili nyepesi sana? Vp kuhusu rais wako JK na mumeo Kinana?...ZINDUKA DADA..!
 
issue ya tembo haiwezi kumrudisha kinana nyuma,ni bora mngeacha nayo tu,ni kama issue ya slaa kukwiba mke wa mtu haiwezi kumrudisha nyuma!thats just the politics of character assasination a.k.a. siasa za maji chuki yaliyo na taka

weka mbali na Tembo
 

weka mbali na wake za watu, weka mbali zaidi na ndoa za watu....kinana ni mwiba mchungu sana kwa chadema na mtasambaratika tu..take it from me. Kwa kipindi kifupi alichokaa madarakani chadema imeyumba, vp akikaa mwaka mmoja? Huo uzushi wenu ndio ugaidi wenyewe unaoongozwa na lwakatare kwa maelekezo ya slaa
 
We ni raia wa nchi gani unaposema Watanzania wana akili nyepesi sana? Vp kuhusu rais wako JK na mumeo Kinana?...ZINDUKA DADA..!

taratibu mama, msamehe bure kwa kuusema ukweli unaokuumiza...say no to ugaidi wa lwakatare
 
Umetumwa? Kwahiyo kama ni mzuri kama ulivyojaribu kumwelezea, unaonaje kama angegombea urais 2015? Nakushauri kuwa uwe mwelewa, TUMEICHOKA ccm na Kama una jipya kuhusu Kinana ungelisema hilo kuwa Kampeni Meneja wa Mkapa na Kikwete kumeleta tija gani? Amemfanyia Kampeni Kikwete, Kikwete amekuwa rais sawa! Lakini muhimu tunaangalia Kikwete ametufanyia nini? Hakuna zaidi ya udini, watu kung'olewa kucha, meno, macho na au kuuawa! Hilo ndo tusifie Kinana kuwa alituingizia kiongozi Mzuri?
 
Mkuu, sijakupata vizuri hapo, kwamba tukiachana la suala la ujangili pia tunatakiwa tumuweke mbali na wake za watu?. Hilo kwangu sio la muhimu kwa sababu hayo ni maisha binafsi, na hayawezi kuathiri uchumi wa nchi ama kuleta madhara yeyote kwa taifa kwa ujumla, tatizo kubwa ni la ujangili, masuala ya ndoa za watu hayana maana sana katika maslahi mapana ya taifa.
 
Kaka najua umejiita "mchambuzi". Sitaki nikubeze wala kuyakataa mawazo yako.Sijui kama kuna uchambuzi ambao unazungumzia upande mmoja wa silingi na kuacha upande mwingine. Kama mwanazuoni ulitakiwa uzungumzie strength and weakness of the guy. Hainingii akilini kumpamba Kinana kuwa ni silaha kwa wapinzani. Possibly inaweza kuwa ni mtazamo wako ambao una maslahi binafsi kuliko huo uchambuzi unaong'ang'ania!

Ni kweli kuwa Kinana amapewa jukumu la kuwa mtendaji mkuu wa CCM,ila kama wewe una akili na ni mchambuzi kweli tena mzalendo, tuzungumzie uhusika wa Kinana katika kuishauri CCM na serikali yake kutekeleza ilani zake ambazo kila siku zipo majukwaani. Mi nilitigemea mchango wa Kinana kuisaidia CCM itekeleze ahadi zake ili sisi Watanzania tuweze kurudisha imani zetu kwa chama, ila bila aibu na kwa masikitiko makubwa unazungumzia vita ya Kinana na wapinzani!!!!!
And funny enough, you are calling yourself an "analyist". Unachambua nini mkuu wakati uanonekana wazi kuwa una mpango wa kusafisha Kinana na kashfa zake z ujangili.

Nisingependa kuzungumzia swala lake la ujangili anaotuhumiwa nao kwani hapa Tanzania hakuna kiongozi yeyote aliewahi kukumbwa na kashfa akawajibika zaidi ya watu kama wewe na akina Nchimbi, AG na wengine mnakuja na kutoa maelezo ambayo wakuwaamini ni wale tu wasioelewa.

Uchambuzi wako ambao ni subjective kwa asilimia mia utakusaidia baadae, we endelea nao. Wenye akili tutaendelea kuchambua pumba na ngano.
 
hivi huyu si walim'goa meno hivi karibuni? bado anamsifia tu msomali?
 
hili gazeti lote la udaku nani ana muda wa kusoma, fanya samari, okoa muda wetu, kuna uzi mwingi sijapitia

wewe soma heading ondoka acha wenye akili timamu waumize vichwa kutambua ukweli juu ya mchapakazi kinana
 

Alistaafu jeshi mwaka 1972 akiwa ametumikia jeshi miaka 20 ! Cheo cha mwisho 'Kanali'. Kwa mantiki hiyo alipata ofisa kadeti (Luteni)1952 ! Hili lilikuwa jeshi gani ? .......KAR ? ...TPDF !? JWTZ !?
 
Ccm ilipofikia hata akija malaika hawezi kuinusuru

tatizo la ccm sio kukosa watu makini ila ni wizi, ufisadi na ubadhirifu,ambao kinana ni sehemu ya hao mafisadi
 
mkuu jamaa asafishiki ata kidogo amechafuka na ameshachafuka kumsafisha ni sawa na mtu anaezuiwa ndevu kama huwezi zuiwa ndevu ata siku moja kwanza huyu ni msomali sidhani kama ana ndui mkononi?
 
eti kwa hoja nyepesi na zisizo na mashiko za ufisadi au uchafu wa jumla jumla wa CCM.

unatuaminisha ya kuwa, ufisadi kwako na kinana ni hoja nyepesi? ebu ucpende kufanya mawazo yako ndo yawe yetu CCM is going to die soooooooooooon

 
Kuna machache nataka kujua hapa. Mchungaji Msigwa alisema mbona ccm hawaombi ushahidi dhidi ya tuhuma kwa Kinana kuhusu ujangili wa meno ya tembo? Ni mara ngapi wabunge wameagizwa kuleta ushahidi dhidi ya kauli zao Bungeni? Lema ni mfano mzuri sana. Kaagizwa alete ushahidi juu ya kauli yake kwamba Kikwete ni mdini. Mbona huyu anayeomba kuleta ushahidi Spika amekuwa kimya? Lukuvi amekuwa kimya?

Mleta mada umeandika wasifu wa Kinana weee. Wasifu ni kinga dhidi ya mapungufu ya mtu? Hujagusia tuhuma za ujangili. Inawezekana kabisa, na ndivyo ilivyo kwamba Kinana ni jangili. Yeye kuwa kanali, waziri, mbunge, balozi, katibu ccm, havimzuii kufanya uhalifu aliofanya na anaoendelea kuufanya.

Kinana kastaafu jeshi 1972 baada ya kulitumikia kwa miaka 20. Ana miaka mingapi sasa? Kwa mahesabu ya haraka alianza kulitumikia jeshi mwaka 1952. Alizaliwa lini huyu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…