Ukweli mchungu kuhusu KINANA

Ukweli mchungu kuhusu KINANA

ni kinana gani unae mzungumzia wewe....ni huyu wa magamba au yule wa tembo......

ni huyu huyu aliefanya ziara mkoano morogoro akawapasha machadema hadi yakaamua kumchafua kwa uzushi na uongo..ni huyu huyu ambaye kibanda alimsifia ndipo magaidi akina lwakatare wakamteka na kumtesa
 
Akiwa katika ziara ya kikazi mkoani morogoro, kinana aliingiza wanachama wapya 4000 kutoka vyama mbalimbali vya siasa na katika kuhitimisha ziara hiyo alitoa hotuba kali na ya kusisimua huku akiwananga machadema kuwa waache utoto na siasa za visasi na zaidi waache kupanga mauaji.kitendo hicho kiliwaudhi na kuwaghadhibisha chadema na hivyo kuamua kumuundia zengwe la kashfa
 
Watanzania wana akili nyepesi sana!

Binafsi naamini ni tatizo la upungufu wa mlo kamili ndio chanzo cha upeo mdogo wa watanzania wengi, mfano ni mleta mada.

Kwa akili ya kawaida kabisa, utagundua huyo mnafiki Msigwa kushadadia suala la Kinana kuwa ana husika na ujangili ni kutaka umaarufu wa bei rahisi.

Wenzake wakina Zitto na makamanda wengine walikuwa wakiibua masuala ya siri mno ya kulihujumu taifa yanayo fanywa na watendaji wasio waadilifu. Ndio maana mchango wa Zitto katika kukomboa raslimali za nchi hauwezi kubezwa na yeyote yule.

Hili suala la Kinana ni la tangu 2008 huko, na INTERPOL walichunguza wakabaini kuwa Kinana ahusiki, sasa kelele za Msigwa za nini hapa? Kwenye ili Msigwa asahau kuwa atatambulika miongoni mwa wabunge machachali kwenye medani za siasa hapa nchini.

Inabidi watanzania mshtuke nia ya huyu Msigwa kupeleka hotuba iliyojaa masimango, kashfa na uongo wa kupitiliza pale bungeni, nia kubwa ya Msigwa ni kumchafua Katibu Mkuu wa CCM taifa, wala hakuwa na maslahi mengine zaidi ya ili.

Ila kama ilivyo ada, njia ya muongo ni fupi, watanzania wazalendo na wafatiliaji wameujua ukweli, na malengo ya Msigwa hayajatimia katika juhudi zake za kumchafua Kinana.

We ni raia wa nchi gani unaposema Watanzania wana akili nyepesi sana? Vp kuhusu rais wako JK na mumeo Kinana?...ZINDUKA DADA..!
 
issue ya tembo haiwezi kumrudisha kinana nyuma,ni bora mngeacha nayo tu,ni kama issue ya slaa kukwiba mke wa mtu haiwezi kumrudisha nyuma!thats just the politics of character assasination a.k.a. siasa za maji chuki yaliyo na taka

weka mbali na Tembo
 
Kwa hiyo mtu akilitumikia jeshi kwa kipindi kirefu kwa cheo cha kanali basi huyo mtu si wa kupuuzwa?, hivi nyie watu wanawatoa wapi? maana hamuwezi kabisa kujenga hoja, Binafsi ninachokihofia kwa huyo kinana ni tembo wetu tu, na wala si kingine, kasi ya jamaa kwenye ujangili inatisha, fikiria meli nzima imejaza meno ya tembo, ni tembo wangapi wameuawa?, ni meli ngapi zimepita bila kugundulika?, huyu jamaa ni hatari, hatareee!, weka mbali na tembo.

weka mbali na wake za watu, weka mbali zaidi na ndoa za watu....kinana ni mwiba mchungu sana kwa chadema na mtasambaratika tu..take it from me. Kwa kipindi kifupi alichokaa madarakani chadema imeyumba, vp akikaa mwaka mmoja? Huo uzushi wenu ndio ugaidi wenyewe unaoongozwa na lwakatare kwa maelekezo ya slaa
 
We ni raia wa nchi gani unaposema Watanzania wana akili nyepesi sana? Vp kuhusu rais wako JK na mumeo Kinana?...ZINDUKA DADA..!

taratibu mama, msamehe bure kwa kuusema ukweli unaokuumiza...say no to ugaidi wa lwakatare
 
Umetumwa? Kwahiyo kama ni mzuri kama ulivyojaribu kumwelezea, unaonaje kama angegombea urais 2015? Nakushauri kuwa uwe mwelewa, TUMEICHOKA ccm na Kama una jipya kuhusu Kinana ungelisema hilo kuwa Kampeni Meneja wa Mkapa na Kikwete kumeleta tija gani? Amemfanyia Kampeni Kikwete, Kikwete amekuwa rais sawa! Lakini muhimu tunaangalia Kikwete ametufanyia nini? Hakuna zaidi ya udini, watu kung'olewa kucha, meno, macho na au kuuawa! Hilo ndo tusifie Kinana kuwa alituingizia kiongozi Mzuri?
 
weka mbali na wake za watu, weka mbali zaidi na ndoa za watu....kinana ni mwiba mchungu sana kwa chadema na mtasambaratika tu..take it from me. Kwa kipindi kifupi alichokaa madarakani chadema imeyumba, vp akikaa mwaka mmoja? Huo uzushi wenu ndio ugaidi wenyewe unaoongozwa na lwakatare kwa maelekezo ya slaa
Mkuu, sijakupata vizuri hapo, kwamba tukiachana la suala la ujangili pia tunatakiwa tumuweke mbali na wake za watu?. Hilo kwangu sio la muhimu kwa sababu hayo ni maisha binafsi, na hayawezi kuathiri uchumi wa nchi ama kuleta madhara yeyote kwa taifa kwa ujumla, tatizo kubwa ni la ujangili, masuala ya ndoa za watu hayana maana sana katika maslahi mapana ya taifa.
 
Kaka najua umejiita "mchambuzi". Sitaki nikubeze wala kuyakataa mawazo yako.Sijui kama kuna uchambuzi ambao unazungumzia upande mmoja wa silingi na kuacha upande mwingine. Kama mwanazuoni ulitakiwa uzungumzie strength and weakness of the guy. Hainingii akilini kumpamba Kinana kuwa ni silaha kwa wapinzani. Possibly inaweza kuwa ni mtazamo wako ambao una maslahi binafsi kuliko huo uchambuzi unaong'ang'ania!

Ni kweli kuwa Kinana amapewa jukumu la kuwa mtendaji mkuu wa CCM,ila kama wewe una akili na ni mchambuzi kweli tena mzalendo, tuzungumzie uhusika wa Kinana katika kuishauri CCM na serikali yake kutekeleza ilani zake ambazo kila siku zipo majukwaani. Mi nilitigemea mchango wa Kinana kuisaidia CCM itekeleze ahadi zake ili sisi Watanzania tuweze kurudisha imani zetu kwa chama, ila bila aibu na kwa masikitiko makubwa unazungumzia vita ya Kinana na wapinzani!!!!!
And funny enough, you are calling yourself an "analyist". Unachambua nini mkuu wakati uanonekana wazi kuwa una mpango wa kusafisha Kinana na kashfa zake z ujangili.

Nisingependa kuzungumzia swala lake la ujangili anaotuhumiwa nao kwani hapa Tanzania hakuna kiongozi yeyote aliewahi kukumbwa na kashfa akawajibika zaidi ya watu kama wewe na akina Nchimbi, AG na wengine mnakuja na kutoa maelezo ambayo wakuwaamini ni wale tu wasioelewa.

Uchambuzi wako ambao ni subjective kwa asilimia mia utakusaidia baadae, we endelea nao. Wenye akili tutaendelea kuchambua pumba na ngano.
 
Ni mtu asiyejali au mpuuzi asiyezijua vyema siasa za Tanzania anayeweza akasimama na kuudharau uteuzi uliofanywa na Rais Kikwete ambaye baada ya kushindwa mara kadhaa hatimaye amefanikiwa kumshawishi, mmoja wa wanasiasa makini na wakongwe, mtumishi wa umma wa muda mrefu, mwanadiplomasia na Kanali Mstaafu wa Jeshi, Abdulrahaman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

Kwa muktadha huo na kwa kuzingatia nafasi kuu ya utendaji aliyopewa, nitazungumzia kwa sehemu tu wasifu wa Kinana, mtu ambaye naamini anapaswa kuangaliwa kwa jicho la karibu na wakati mwingine kudhibitiwa ili kasi yake ya kukijenga chama alichopewa dhamana ya kukinusuru isije ikasababisha kuyumba kama si mauti ya kisiasa kwa baadhi ya vyama vya upinzani.

Ni wazi kwamba, kuteuliwa kwa Kinana kuwa Mtendaji Mkuu wa CCM Taifa, akirithi mikoba iliyomshinda, Wilson Mukama, kumetutia ganzi baadhi yetu ambao kwa muda mrefu tumekuwa ‘mashabiki’ au waumini wa kuchagiza kwa njia ya kalamu na wakati mwingine katika mijadala ya wazi kwamba, taifa lilikuwa na haja ya kutafuta mabadiliko ya uongozi kutoka nje ya chama tawala.

Sitaki kuwa miongoni mwa wapenda mabadiliko ambao kwa njia za kujifariji au za kujipa matumaini hewa wameingia katika mkumbo wa jumla jumla wa kumbeza Kinana kwa namna wanayotaka kuuaminisha umma wa Watanzania kwamba, mtu huyo anaweza akasukumwa kirahisi kwa namna ile ile ilivyopata kuwa kwa watangulizi wake kadhaa waliopata kushika wadhifa huo.

siku zote nilikuwa nikiamini kwamba, ukatibu mkuu kwa Kinana ilikuwa ni silaha moja ya maangamizi kwa vyama vya upinzani ambavyo naamini vinapaswa kuendelea kupewa fursa ya kuaminiwa na kukomaa.

Kinana anaendelea kubakia kuwa tishio kubwa kwa ustawi wa upinzani ambao ni rutuba muhimu kwa maendeleo ya demokrasia na misingi ya utawala bora.

Hili ndilo ambalo naamini wapinzani wanapaswa kulitazama na kulitafakari nyakati hizi wanapoendesha harakati zao za kukabiliana na maguvu ya dola na haya mapya ya hoja ambazo aghalab zitaongozwa na Kinana nyakati hizi taifa linapojiandaa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa miaka mitatu ijayo.

Haitoshi kwa kina Freeman Mbowe, Profesa Ibrahim Lipumba, James Mbatia, Dk. Willibrod Slaa na Zitto Kabwe kumbeza Kinana na timu ya watendaji wake eti kwa hoja nyepesi na zisizo na mashiko za ufisadi au uchafu wa jumla jumla wa CCM.

Wapinzani na wachambuzi wa mambo wanapaswa kujua na kutambua kwamba, Kinana ni mwanasiasa wa vitendo, msomaji mzuri wa vitabu, ripoti, taarifa, magazeti, msikilizaji na msikivu mzuri wa mambo mepesi na mazito kuliko alivyokuwa ‘utopia’ Mukama anayeamini na kuzitetea nadharia zisizotekelezeka.

Si hilo tu, wapinzani wanapaswa kutambua kwamba, historia yake ya uaskari alioutumikia miaka 20 hadi mwaka 1972 akifikia cheo halisi cha jeshi cha Kanali ikimhusisha na mafunzo mahususi ya kimkakati ni sehemu ya mambo ambayo yanatawala nidhamu ya kazi ya aina ya kipekee iliyomfanya Kinana akawa jemedari wa mapambano ya CCM tangu mwaka 1995 hadi leo.

Wachambuzi wa mambo, nikiwamo mimi mwenyewe ambao siku zote tumekuwa tukiiona CCM kuwa chama kinachokufa kwa maana ya kuchungulia kaburi, tunapaswa kuanza kutafakari upya mawazo yetu hayo, nyakati hizi Kinana alipopewa dhamana ya kuwa mtendaji wake mkuu.

Tutakuwa wendawazimu iwapo tutamlinganisha Kinana na Mukama na kusahau kwamba huyu aliye kilingeni leo ndiye aliyemuongoza Benjamin Mkapa katika mapambano makali ya kisiasa mwaka 1995, zama Augustine Mrema alipokuwa tishio la kwanza la kweli dhidi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu.

Alikuwa ni Kinana aliyefanya kazi kubwa katika kipindi chote cha kampeni akiratibu na kuongoza kampeni zote za Mkapa zilizomjumuisha pia Mwalimu Nyerere katika mazingira ambayo wengi walikuwa wakiamini CCM ilikuwa katika mwelekeo wa anguko la kihistoria.

Kinana ambaye kabla ya mwaka 1995 alikuwa tayari amepata kuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri wa Ulinzi alitumia vyema mbinu za medani na zile za kidemokrasia na kidiplomasia kumjengea uhalali Mkapa ambaye wakati huo alikuwa mwanasiasa ambaye hakuwa akijulikana sana.

Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, siku chache tu baada ya kuingia Ikulu kwa mara ya kwanza mwaka 1995, kwa sababu ama ya ulevi wa madaraka au kwa kutingwa na kazi za kimamlaka, Mkapa alisahau kazi kubwa aliyofanyiwa na Kinana.

Ni katika kipindi hicho cha kati ya mwaka 1995 na 2000 ndipo nilipokutana kwa mara ya kwanza na mara kadhaa na Kinana nyumbani kwake Masaki, jijini Dar es Salaam ambako nilipata fursa ya kumsikiliza na kuufahamu upeo mkubwa wa kuona mambo aliokuwa nao mwanasiasa huyo.

Tangu wakati huo hadi wakati wa kampeni za mwisho za mwaka 2010, niliendelea kukutana kwa nyakati fupi fupi na Kinana na mara kadhaa nikawa mtu wa kufuatilia na kuzisikiliza kwa makini, habari zake kutoka ama kwa marafiki au maadui zake wa kisiasa.

Sikushangazwa hata kidogo niliposikia tena kwamba, Mkapa alilazimika kumuangukia tena Kinana na kumuomba aongoze tena kampeni zake mwaka 2000 kabla ya Kikwete naye hajafanya kile alichofanya mtangulizi wake alipomuomba mwanasiasa huyo adhibiti joto la kiti cha urais mwaka 2010.

Uwezo wake mkubwa wa kisiasa, umakini wake na upeo mkubwa alionao katika kuona na kuchambua masuala ya siasa, uchumi na jamii ndivyo vitu ambavyo kwanza kwa nyakati tofauti vimepata kumfanya Kinana awe Mbunge wa Jimbo la Arusha kwa miaka 10, Mbunge wa Afrika Mashariki na Spika wa Bunge hilo.

Si ajabu hata kidogo kwamba, hata kabla ya kufikia huko, ni Kinana huyo huyo ambaye alipata kuwa Mwakilishi wa Kidiplomasia wa Rais wa Tanzania katika eneo la Maziwa Makuu na kabla ya hapo akiwa Mwenyekiti wa Mawaziri wa Ulinzi wa Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) zama akiwa Waziri wa Ulinzi katika Serikali ya Awamu ya Pili iliyokuwa ikiongozwa Rais Ali Hassan Mwinyi.

Uzoefu wake katika siasa za kiraia unaanzia mwaka 1972 wakati alipostaafu jeshi akiwa Kanali baada ya kulitumikia kwa miaka 20 ndiyo ambao amekuwa akiutumia kama silaha kubwa ya kukijua chama chake na pengine kumfanya awe mmoja kati ya watu wachache ambao wamepata kuwafanyia kazi marais wote wane wa Tanzania.

Anarithi mikoba ya Mukama akiwa mmoja wa wanasiasa wachache wa CCM wa rika ile ile la kina Kikwete ambaye alilikimbia na kulikana kundi la mtandao mwaka 2005 ambalo baadhi yetu tunaamini kuwa, ndilo lilisababisha kuzaliwa kwa siasa mpya za kupakana matope, kuzushiana na kuhujumiana ndani na nje ya CCM.

Lakini pengine kubwa katika yote hayo anaingia madarakani huku akiwa na hazina ya uzoefu mkubwa wa kuongoza mapambano dhidi ya vyama vya upinzani na kushinda katika mazingira ambayo aghalab yamekuwa yakiacha vidonda visivyopona kwa wapinzani tangu mwaka 1995. Huyu si mtu wa kumpuuza au kumbeza hata kidogo.
hivi huyu si walim'goa meno hivi karibuni? bado anamsifia tu msomali?
 
hili gazeti lote la udaku nani ana muda wa kusoma, fanya samari, okoa muda wetu, kuna uzi mwingi sijapitia

wewe soma heading ondoka acha wenye akili timamu waumize vichwa kutambua ukweli juu ya mchapakazi kinana
 
Alistaafu jeshi mwaka 1972 akiwa ametumikia jeshi miaka 20 ! Cheo cha mwisho 'Kanali'. Kwa mantiki hiyo alipata ofisa kadeti (Luteni)1952 ! Hili lilikuwa jeshi gani ? .......KAR ? ...TPDF !? JWTZ !?
 
Ccm ilipofikia hata akija malaika hawezi kuinusuru

tatizo la ccm sio kukosa watu makini ila ni wizi, ufisadi na ubadhirifu,ambao kinana ni sehemu ya hao mafisadi
 
mkuu jamaa asafishiki ata kidogo amechafuka na ameshachafuka kumsafisha ni sawa na mtu anaezuiwa ndevu kama huwezi zuiwa ndevu ata siku moja kwanza huyu ni msomali sidhani kama ana ndui mkononi?
 
eti kwa hoja nyepesi na zisizo na mashiko za ufisadi au uchafu wa jumla jumla wa CCM.

unatuaminisha ya kuwa, ufisadi kwako na kinana ni hoja nyepesi? ebu ucpende kufanya mawazo yako ndo yawe yetu CCM is going to die soooooooooooon

Kuna machache nataka kujua hapa. Mchungaji Msigwa alisema mbona ccm hawaombi ushahidi dhidi ya tuhuma kwa Kinana kuhusu ujangili wa meno ya tembo? Ni mara ngapi wabunge wameagizwa kuleta ushahidi dhidi ya kauli zao Bungeni? Lema ni mfano mzuri sana. Kaagizwa alete ushahidi juu ya kauli yake kwamba Kikwete ni mdini. Mbona huyu anayeomba kuleta ushahidi Spika amekuwa kimya? Lukuvi amekuwa kimya?

Mleta mada umeandika wasifu wa Kinana weee. Wasifu ni kinga dhidi ya mapungufu ya mtu? Hujagusia tuhuma za ujangili. Inawezekana kabisa, na ndivyo ilivyo kwamba Kinana ni jangili. Yeye kuwa kanali, waziri, mbunge, balozi, katibu ccm, havimzuii kufanya uhalifu aliofanya na anaoendelea kuufanya.

Kinana kastaafu jeshi 1972 baada ya kulitumikia kwa miaka 20. Ana miaka mingapi sasa? Kwa mahesabu ya haraka alianza kulitumikia jeshi mwaka 1952. Alizaliwa lini huyu?
 
Back
Top Bottom