Ukweli mchungu kuhusu KINANA

Ukweli mchungu kuhusu KINANA

Mleta uzi umetumwa kuja kumsafisha JANGILI ila kumbuka Chama Cha Majangili hamkubaliki tena ktk jamii.
Hata mfanye nini hakunj anayeweza kukubali Majangili na Chama chenu
 
mojawapo ya ukomavu wa kisiasa ni kuwa mtulivu,ustahimilivu,maono,kuthubutu na kuwa na maamuzi sahihi.sifa hizi kinana naona mungu amemjalia.
 
Siasa za kuchafuana zilizoibuka hivi karibuni hapa nchini zinazofanywa na vyama vya upinzani hazitaufikisha mbali upinzani

Hata mume wako mr dhaifu alisema kuwa ni vyama vya msimu lakini akisikia chadema anatetemeka ndio ukawe wewe mkewe?
 
Nadhani kwa bahati mbaya hujamwelewa mtoa mada. Kama wewe ni mchambuzi utaona kuwa anaijenga CDM kwa njia tofauti

Huku ni kujenga cdm bila kudhamiria. Inaingia akilini kulinganisha upinzani enzi za Mrema na huu wa sasa kweli?
 
Bado sijaelewa lengo la mleta uzi huu
Kwamba kinana ni mtu makini, hodari, ametumika na marais wote
Je, sifa hizo ndizo tunazotakiwa kuzizingatia na kuacha kuhoji kama kweli amehusika na ujangili wa tembo?

Hata hivyo nadhani kuna sifa moja mleta uzi ameisahau. Kinana ameongozoza kampeni za urais ambazo zote kura ziliibiwa kupindukia, wapiga kura walichakachuliwa sana, na matokeo mengi yalitangazwa kwa nguvu. Kampeni zote za uchaguzi alizoongoza alitekeleza mikakati yake iliyogawa wapiga kura kwa dini na makabila yao. Mtu wa sifa hizi mimi simuoni kama ni mtu makini.

Unaweza kuwa na akili sana kichwani lakini usiwe na utu moyoni. Pima vyote viwili, utu na akili
 
Tufike mahali tufikirie kama taifa, vizazi vijavyo vinategemea fikara zetu na namna ya kuyaendea mambo.
 
Tunachohitaji Watanzania ni mtu ambaye ataweza kuilinda katiba yetu na rasilimali zetu kwa manufaa yetu . Unadhani Kinana kwa nafasi yake anaweza kuisaidia Tanzania ikafikia hiyo ndoto ? Basi na atuonyeshe kwa muda huu mfupi uliobaki
 
Ni mtu asiyejali au mpuuzi asiyezijua vyema siasa za Tanzania anayeweza akasimama na kuudharau uteuzi uliofanywa na Rais Kikwete ambaye baada ya kushindwa mara kadhaa hatimaye amefanikiwa kumshawishi, mmoja wa wanasiasa makini na wakongwe, mtumishi wa umma wa muda mrefu, mwanadiplomasia na Kanali Mstaafu wa Jeshi, Abdulrahaman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

Kwa muktadha huo na kwa kuzingatia nafasi kuu ya utendaji aliyopewa, nitazungumzia kwa sehemu tu wasifu wa Kinana, mtu ambaye naamini anapaswa kuangaliwa kwa jicho la karibu na wakati mwingine kudhibitiwa ili kasi yake ya kukijenga chama alichopewa dhamana ya kukinusuru isije ikasababisha kuyumba kama si mauti ya kisiasa kwa baadhi ya vyama vya upinzani.

Ni wazi kwamba, kuteuliwa kwa Kinana kuwa Mtendaji Mkuu wa CCM Taifa, akirithi mikoba iliyomshinda, Wilson Mukama, kumetutia ganzi baadhi yetu ambao kwa muda mrefu tumekuwa ‘mashabiki’ au waumini wa kuchagiza kwa njia ya kalamu na wakati mwingine katika mijadala ya wazi kwamba, taifa lilikuwa na haja ya kutafuta mabadiliko ya uongozi kutoka nje ya chama tawala.

Sitaki kuwa miongoni mwa wapenda mabadiliko ambao kwa njia za kujifariji au za kujipa matumaini hewa wameingia katika mkumbo wa jumla jumla wa kumbeza Kinana kwa namna wanayotaka kuuaminisha umma wa Watanzania kwamba, mtu huyo anaweza akasukumwa kirahisi kwa namna ile ile ilivyopata kuwa kwa watangulizi wake kadhaa waliopata kushika wadhifa huo.

siku zote nilikuwa nikiamini kwamba, ukatibu mkuu kwa Kinana ilikuwa ni silaha moja ya maangamizi kwa vyama vya upinzani ambavyo naamini vinapaswa kuendelea kupewa fursa ya kuaminiwa na kukomaa.

Kinana anaendelea kubakia kuwa tishio kubwa kwa ustawi wa upinzani ambao ni rutuba muhimu kwa maendeleo ya demokrasia na misingi ya utawala bora.

Hili ndilo ambalo naamini wapinzani wanapaswa kulitazama na kulitafakari nyakati hizi wanapoendesha harakati zao za kukabiliana na maguvu ya dola na haya mapya ya hoja ambazo aghalab zitaongozwa na Kinana nyakati hizi taifa linapojiandaa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa miaka mitatu ijayo.

Haitoshi kwa kina Freeman Mbowe, Profesa Ibrahim Lipumba, James Mbatia, Dk. Willibrod Slaa na Zitto Kabwe kumbeza Kinana na timu ya watendaji wake eti kwa hoja nyepesi na zisizo na mashiko za ufisadi au uchafu wa jumla jumla wa CCM.

Wapinzani na wachambuzi wa mambo wanapaswa kujua na kutambua kwamba, Kinana ni mwanasiasa wa vitendo, msomaji mzuri wa vitabu, ripoti, taarifa, magazeti, msikilizaji na msikivu mzuri wa mambo mepesi na mazito kuliko alivyokuwa ‘utopia’ Mukama anayeamini na kuzitetea nadharia zisizotekelezeka.

Si hilo tu, wapinzani wanapaswa kutambua kwamba, historia yake ya uaskari alioutumikia miaka 20 hadi mwaka 1972 akifikia cheo halisi cha jeshi cha Kanali ikimhusisha na mafunzo mahususi ya kimkakati ni sehemu ya mambo ambayo yanatawala nidhamu ya kazi ya aina ya kipekee iliyomfanya Kinana akawa jemedari wa mapambano ya CCM tangu mwaka 1995 hadi leo.

Wachambuzi wa mambo, nikiwamo mimi mwenyewe ambao siku zote tumekuwa tukiiona CCM kuwa chama kinachokufa kwa maana ya kuchungulia kaburi, tunapaswa kuanza kutafakari upya mawazo yetu hayo, nyakati hizi Kinana alipopewa dhamana ya kuwa mtendaji wake mkuu.

Tutakuwa wendawazimu iwapo tutamlinganisha Kinana na Mukama na kusahau kwamba huyu aliye kilingeni leo ndiye aliyemuongoza Benjamin Mkapa katika mapambano makali ya kisiasa mwaka 1995, zama Augustine Mrema alipokuwa tishio la kwanza la kweli dhidi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu.

Alikuwa ni Kinana aliyefanya kazi kubwa katika kipindi chote cha kampeni akiratibu na kuongoza kampeni zote za Mkapa zilizomjumuisha pia Mwalimu Nyerere katika mazingira ambayo wengi walikuwa wakiamini CCM ilikuwa katika mwelekeo wa anguko la kihistoria.

Kinana ambaye kabla ya mwaka 1995 alikuwa tayari amepata kuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri wa Ulinzi alitumia vyema mbinu za medani na zile za kidemokrasia na kidiplomasia kumjengea uhalali Mkapa ambaye wakati huo alikuwa mwanasiasa ambaye hakuwa akijulikana sana.

Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, siku chache tu baada ya kuingia Ikulu kwa mara ya kwanza mwaka 1995, kwa sababu ama ya ulevi wa madaraka au kwa kutingwa na kazi za kimamlaka, Mkapa alisahau kazi kubwa aliyofanyiwa na Kinana.

Ni katika kipindi hicho cha kati ya mwaka 1995 na 2000 ndipo nilipokutana kwa mara ya kwanza na mara kadhaa na Kinana nyumbani kwake Masaki, jijini Dar es Salaam ambako nilipata fursa ya kumsikiliza na kuufahamu upeo mkubwa wa kuona mambo aliokuwa nao mwanasiasa huyo.

Tangu wakati huo hadi wakati wa kampeni za mwisho za mwaka 2010, niliendelea kukutana kwa nyakati fupi fupi na Kinana na mara kadhaa nikawa mtu wa kufuatilia na kuzisikiliza kwa makini, habari zake kutoka ama kwa marafiki au maadui zake wa kisiasa.

Sikushangazwa hata kidogo niliposikia tena kwamba, Mkapa alilazimika kumuangukia tena Kinana na kumuomba aongoze tena kampeni zake mwaka 2000 kabla ya Kikwete naye hajafanya kile alichofanya mtangulizi wake alipomuomba mwanasiasa huyo adhibiti joto la kiti cha urais mwaka 2010.

Uwezo wake mkubwa wa kisiasa, umakini wake na upeo mkubwa alionao katika kuona na kuchambua masuala ya siasa, uchumi na jamii ndivyo vitu ambavyo kwanza kwa nyakati tofauti vimepata kumfanya Kinana awe Mbunge wa Jimbo la Arusha kwa miaka 10, Mbunge wa Afrika Mashariki na Spika wa Bunge hilo.

Si ajabu hata kidogo kwamba, hata kabla ya kufikia huko, ni Kinana huyo huyo ambaye alipata kuwa Mwakilishi wa Kidiplomasia wa Rais wa Tanzania katika eneo la Maziwa Makuu na kabla ya hapo akiwa Mwenyekiti wa Mawaziri wa Ulinzi wa Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) zama akiwa Waziri wa Ulinzi katika Serikali ya Awamu ya Pili iliyokuwa ikiongozwa Rais Ali Hassan Mwinyi.

Uzoefu wake katika siasa za kiraia unaanzia mwaka 1972 wakati alipostaafu jeshi akiwa Kanali baada ya kulitumikia kwa miaka 20 ndiyo ambao amekuwa akiutumia kama silaha kubwa ya kukijua chama chake na pengine kumfanya awe mmoja kati ya watu wachache ambao wamepata kuwafanyia kazi marais wote wane wa Tanzania.

Anarithi mikoba ya Mukama akiwa mmoja wa wanasiasa wachache wa CCM wa rika ile ile la kina Kikwete ambaye alilikimbia na kulikana kundi la mtandao mwaka 2005 ambalo baadhi yetu tunaamini kuwa, ndilo lilisababisha kuzaliwa kwa siasa mpya za kupakana matope, kuzushiana na kuhujumiana ndani na nje ya CCM.

Lakini pengine kubwa katika yote hayo anaingia madarakani huku akiwa na hazina ya uzoefu mkubwa wa kuongoza mapambano dhidi ya vyama vya upinzani na kushinda katika mazingira ambayo aghalab yamekuwa yakiacha vidonda visivyopona kwa wapinzani tangu mwaka 1995. Huyu si mtu wa kumpuuza au kumbeza hata kidogo.
Mleta uzi amekopy makala ya Kibanda wakati anaelekea kuondoka tanzania daima
 
Namkubali Mh Kinana, lakini Nape na Mwigulu wanamwaribia sana katika discipline ndani ya CCM.
 
Huku ni kujenga cdm bila kudhamiria. Inaingia akilini kulinganisha upinzani enzi za Mrema na huu wa sasa kweli?
Ni kosa kubwa maishani kumdharau adui. Hivyo mtoa mada alitaka kutueleza kuwa makini ili CDM kupata ushindi 2015. Kwa mfano mwepesi kabla ya mchezo wa watani wa jadi, Yanga ikitaka ushindi, basi Yanga inatakiwa kuwa makini na lolote lisemwalo hasa zuri kuhusu Simba kama inataka kupata ushindi. Vile vile Yanga inatakiwa kutoa taarifa potofu kuhusu yenyewe ili Simba ijisahau kuwa Yanga si lolote.
 
Tutaendelea kumbeza pamoja na ustaafu wake wa jeshi maana amechafuka, zamani enzi za Nyerere alikuwa mtu makini sana lakini sasa hana umakini wowote na hasa alipoingia kwenye genge la wezi wa rasilimali za nchi. Amepewa ukatibu mkuu kama shukrani za kumpigia kampeni JK na ndiyo maana anafanya anavyotaka kusafirisha nyara za serikali. Atakisaidia sana chama cha mapinduzi maana anachangia pesa nyingi kwenye chama. Ukitaka kujua kwamba Kinana si yule wa 2005 sikiliza hotuba yake ya mkutano wa Morogoro... Huwezi kuwa mtu makini ukiwa ndani ya CCM, muulize Samuel Sitta, Mwakyembe, Mama Kilango, Nape, Mwandosya watakuambia nini kilichomo ndani ya CCM. Hata wale ambao huwadhanii kabisa kwamba wanaweza kufanya madudu ukielezwa mambo wanayofanya hutaamini!! Endeleeni kumsifia Kinana.
Mmesahau mlivyomsifia Mkama kwamba alifanya mambo makubwa Dar akiwa Mkurugenzi wa jiji wengine wakasema sasa chama kimepata Jembe, akatoa na siku 90 wakiwa na Nnauye.... hovyoooo. Leo Kinana!!! poleni wapambe
 
Mleta uzi hata sijakuelewa kwa sababu hujaweza kutuonesha namna ambavyo uadilifu wake huo wa kuanzia miaka ya 1960's unaweza kumsafisha na matendo yake ya sasa ya ujangili kuua na kusafirisha meno ya tembo wetu ambayo sasa ndiyo agenda kuu inayomuhusu yeye kwa muda huu.We are talking about the present,what Kinana is doing now.Hiyo habari ya miaka ile haina maana sana kwetu sasa kwa sababu kama ulitenda mema milioni kadhaa kuanzia jana na ukatenda ovu baya leo hakika hilo baya moja pekee linafuta mema yote uliyotenda miaka milioni uliyoishi.Na hii ndiyo kanuni atakayotumia MUNGU MUUMBA WA BINGU NA NCHI kumhukumu kila aliye kiumbe wake

So, mimi sijaelewa hata kidogo uadilifu wa Kinana wa miaka yote leo unahalalisha kwa namna gani matendo yake maovu ya sasa....UJANGILI WA TEMBO WETU kwa sababu mleta uzi katika kila setensi aliyoandika hapo juu sijaona alipojaribu kusema usafi wa Kinana katika hujuma dhidi ya uchumi wa nchi yetu anazohusishwa nazo sasa zaidi ya hoja nyepesi sana za juujuu za kumtakasa kwa kutumia historia ambayo kwa namna yeyote hakuna mwenye tatizo na hilo hata kama kweli ndivyo alivyo.Nasema kwa sbb ni lazima tufahamu kwamba kwa sasa tuna-deal na kizazi cha dot.com.....vijana wengi wa kuanzia miaka ya 1980 to date ambao hiyo historia kwao si ishu wala hawana haja nayo...na hili maana yake ni kuwa hujaweza kumsaidia Kinana na CCM yake kuwa safi na free na uchafu alioubeba sasa ambao by any means kwa nafasi yake kama mtendaji mkuu wa chama kinachotawala na kinachosimamia serikali inayotekeleza sera ambazo zinamuathiri kila mmoja wetu,hakustahili kuwa na tuhuma kama hizi bila ya hatua za haraka,zilizowazi na zisizotia hata chembe ya shaka kuchukuliwa na chama chake kumsafisha ili aendelee kuaminika na umma!!.

Lakini kinachofanyika sasa ni upuuzi na kuwafanya watu wote ni wajinga hawawezi kuchanganua na kupima mambo katika mizani sawia ya weledi wa mambo.Wewe cheki hata kule ambako hili jambo limeibukia(bungeni) hakuna hata mmoja katika serikali au wabunge wa chama chake aliyesimama kwa kutumia kanuni za chombo(bunge) ili kuleta hoja thabiti chao ya kumtetea na kumkinga huyu bwana dhidi ya tuhuma zake ikiwa ni pamoja na kumtaka mtoa tuhuma kuleta ushahidi wa tuhuma.Lakini tulichokiona,tunachokiona sasa na tutakachoendelea kukiona baadaye ni taharuki na kejeli kuelekezwa kwa mtoa hoja na CHADEMA jambo ambalo kwa watu wanaofikiri kwa kutumia vichwa wanatambua mara moja kuwa nyoka kapigwa jiwe la kichwa sasa anatapatapa ili afe tu.
 
Nani ana mpuuza? Kama kauza pembe si kauza tu? Kwani shida iko wapi na huo umaarufu alionao?
 
Umejitahidi kumremba lakini mwisho wa siku mbivu na mbichi zitajulikana, uzoefu wake katika siasa tutaona utatusaidia vipi kujikwamua na umaskini ilionao Tanzania. Pia tutaona ni kwa namna gani atairudisha heshima ya CCM ambayo inaelekea kupotea kabisa hata kwa wanakijiji ambao walikua wanategemewa.
 
Teh teh teeh..! Kweli ukweli mchungu, mtachonga sana mwaka huu ila ukweli utabakia kuwa ukweli daima, Kinana ni jembe na ni pigo takatifu kwa upinzani..!

Nakubaliana na wewe kuwa hili ni pigo takatifu,lakini si kwa wapinzani bali kwa watanzania wote! kwa maliasili zetu zote, ni pigo takatifu kwa tembo wetu.
NAkubali pia kama Kinana ni mtu makini,madhubuti ,jasiri na hodari wa mipango na mikakati lakini je wajuwa kuwa wahalifu wananidhamu ya hali ya juu linapokuja suala la mambo yao?
In short uhodari na umakini unomnasibisha mtu huyu si wa kuijenga nchi yetu bali kuiangamiza usinitake nikupe ushahidi kwani kwa uhodari wao ushahidi sina ,kutokana na umahiri wao k sina uwezo wa kuwazuia,kutokana na umakini wao sina uwezo wa kuwatia hatiani ,kutokana na mikakati yao sina uwezo wa kuondoa ulindanaji wao .
LAKINI kutokana na uwezo mkubwa wa KISANDUKU CHA KURA 2015 UWEZO WANGU UTAKUWA MKUBWA KUYASHINDA YOTE HAYO TUSUBIRI!
 
Jana nilimsikia kijana moja wa Lumumba akilalamika buku saba yake aijaingizwa kwa Mpesa. Wanajitaidi sana kuosha kinyesi Nape hawa vijana walipeni kwa wakati kwani wanaumia sana hasa kwa hili sakata. Hawa vijana wa UVCCM awalali kwa sasa. Usiku mchana wanashinda kwenye mitandao
 
Wanaompuuza kinana ni mambumbu wa kufikiri,na hiyo ndio hulka ya atanzania na kwanini msigwa asipeleke ushahidi huo kwenye vyombo vya dola ni kutaka kujichukulia ujiko kwa wajinga wasio weza kufikiri, apeleke kama ulivyopelekwa wa lwakatare??
 
Back
Top Bottom