Ukweli mchungu kuhusu KINANA

Ukweli mchungu kuhusu KINANA

Huna hoja, kinana ni very smart katika utendaji na ni hatari kubwa kwa survival ya upinzani ndio mana wanajaribu kumtungia uongo na uzushi

Njoo udake buku 7 Lumumba hapa muda si mredu mtaongezewa dau kwa kazi nzuri mnavyo ponda upinzani
 
Yap hatutakiwi kumbeza tembo wetu wanateketea
 
Huu uzi wa vilaza wa Lumumba, haunihusu, am out!!!
 
F...ck you .what about our elphant. Kinana is the greatest poacher
 
Kinana ni mwanajeshi amelitumikia jeshi kwa kipindi kirefu kwa cheo cha kanali...si mtu wa kupuuzwa
Vile vile JK ni alikuwa mwanajeshi amelitumikia jeshi kwa nafasi yake lakini hajui kwanini tanzania ni maskini, mauji ya albino yameshamiri akiwa kiongozi, deni la taifa linetripple, wanafunzi wamefeli kuliko wakati wowote kwenye historia ya taifa hili. Si hivyo tu, serikali yake ina waliokuwa wanajeshi kama mkuchika lakini hali ni mbaya kuliko kawaida. Kawaweka wanajeshi wastaafu wengi kama wasaidizi wake huko mikoani kama machibya, aliyekuwepo pia kalembo, etc lakini hakuna uafadhali. Hitimisho: kuwa mwanajeshi haimaanishi una leseni ya kuweza kila kitu. Uongozi unahitaji dhamira safi, nia ya kutumikia unaowaongoza, uwezo wa kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati sahihi na kufuata sheria na taratibu.
 
Kinana ni mwanajeshi amelitumikia jeshi kwa kipindi kirefu kwa cheo cha kanali...si mtu wa kupuuzwa

Kwani kuna vita vya kijeshi? au ni imapambano ya matabaka kati ya walionacho na wasionacho?

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Aisee. Kutokana na uwezomhuo wa kinana, ndo maana chadema wanaweweseka na kutafuta kila mbinu chafu kumchafua
Msipende kusema vitu visivyo na uhalisia kama Kinana ni Mzoefu na anakubalika katika jamii katika mikutano yake kule Morogoro alifanya pia Ruaha na matokeo yake katika uchaguzi wa kijiji na kitongoji CCM imeshindwa, kushindwa huko kwa CCM kunamaanisha nini kwa huyo kinana wenu?
 
Tatizo la wanaCCM wengi ni kupenda kuzunguka saaana. Je unadhani tatizo la CCM lilikua Mukama? Ona mwendo wa chama tangu mwaka 2005 hadi leo. Acheni ujinga na unafiki wa kuanza kupambana kwa sifa zisizokua na kichwa wala miguu.

Tatizo la CCM ni mwenyekiti na wala sio kiongozi mwingine yeyote, na bahati mbaya sana hakuna mwanaCCM yeyote mwenye ujasiri wa kulisema hili hadharani au kwenye vikao vyenu vya chama.
 
Wakati unahangaika kuleta utumbo wako hapa kuhusu Kinana, kuna habari kuwa shehena yake nyingine ya pembe za ndovu imekamatwa huko Hongkong jana>>>> Hebu soma habari hii>>>>>>

[TABLE="class: cms_table_contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: cms_table_contentheading"]Hong Kong seizes $400,000 ivory from Tanzania, Kenya [/TD]
[TD="class: cms_table_buttonheading, align: right"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: cms_table_contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: cms_table_createdate"] Thursday, 02 May 2013 10:16
The Citizen
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]

Upon X-ray image analysis, the consignment was detected to contain elephant tusks instead of spare parts, a statement said Hong Kong.

Hong Kong customs officers have seized 113 elephant tusks worth nearly $400,000 on the Chinese ivory market, officials said yesterday. The smuggled ivory was seized at the airport on Tuesday in a container marked “spare parts” from Burundi which was bound for Singapore, said an official statement.

The total seizure, weighing 300 kilograms (660 pounds), was worth an estimated HK$3 million ($390,000). “Upon X-ray image analysis, the consignment was detected to contain ivory tusks instead of spare parts,” the statement said.

Customs officers made the city’s largest ivory seizure last October when they intercepted almost four tonnes worth about $3.4 million, hidden in shipments from Kenya and Tanzania. In January, customs officers intercepted another container from Kenya carrying 779 pieces of ivory weighing 1.3 tonnes.

Anyone found guilty of importing ivory into Hong Kong faces up to two years in jail and a maximum HK$5 million fine. Even so, the city remains a major trading centre for processed ivory goods such as carvings and jewellery.

The international trade in elephant ivory, with rare exceptions, has been outlawed since 1989 after elephant populations in Africa dropped rapidly from millions in the mid-20th century to around 600,000 by the end of the 1980s.

However, a rise in the illegal trade in ivory has been fuelled by demand in Asia and the Middle East, where elephant tusks are used in traditional medicines and to make ornaments.

Africa is home to an estimated 472,000 elephants whose survival is threatened by poaching, illegal game hunting and habitat loss. (AFP)
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Kama Kinana ni mtu makini na mwenye busara, basi naamini hiyo busara na umakini utamuongoza kutafuta (m)wanasheria kutafuta haki baada ya kuchafuliwa jina lake kwa kutuhumiwa kuwa JANGILI...ndiyo nimesema JANGILI. Kama angekuwa makini angekuwa ameshatafakari (Just to think about it) hata kurudisha zile mashine za kufulia zilizokuwa zimetolewa kwa ajili ya Mount Meru Hosp.

Hatutaki kusikia porojo za Kigwangalla eti Marando alimshauri awasamehe waliomtuhumu au ile list ya mafisadi aliyoitoa Slaa na wengi wao wakasema wataenda mahakamani...F%&#@k that. Kama yeye ni mtu makini akiamini kuwa ana makende mawili aende mahakamani kufungua kesi ya madai. Wanasheria wako tu hata wa bure (Lamwai). Kutuma watu mahususi tena wengine wageni hapa JF (Mnakaribishwa though) kuja kumtetea kwenye social media haitasaidia lolote zaidi ya kuongeza maswali juu ya umakini wa KINANA.

Mkuu uliyeleta huu uzi, unakaribishwa maana nimeona una kamba mguuni. Mpelekee salamu na ushauri wa bure kuwa anatakiwa kutafuta haki yake mahakamani na si kwenye social media, hata Ndugulile anajua hilo. Kwa msemo wa Mwanakijiji, anatakiwa kuchora mstari na si kukimbilia kwenye social media.
 
Ni mtu asiyejali au mpuuzi asiyezijua vyema siasa za Tanzania anayeweza akasimama na kuudharau uteuzi uliofanywa na Rais Kikwete ambaye baada ya kushindwa mara kadhaa hatimaye amefanikiwa kumshawishi, mmoja wa wanasiasa makini na wakongwe, mtumishi wa umma wa muda mrefu, mwanadiplomasia na Kanali Mstaafu wa Jeshi, Abdulrahaman Kinana kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

Kwa muktadha huo na kwa kuzingatia nafasi kuu ya utendaji aliyopewa, nitazungumzia kwa sehemu tu wasifu wa Kinana, mtu ambaye naamini anapaswa kuangaliwa kwa jicho la karibu na wakati mwingine kudhibitiwa ili kasi yake ya kukijenga chama alichopewa dhamana ya kukinusuru isije ikasababisha kuyumba kama si mauti ya kisiasa kwa baadhi ya vyama vya upinzani.

Ni wazi kwamba, kuteuliwa kwa Kinana kuwa Mtendaji Mkuu wa CCM Taifa, akirithi mikoba iliyomshinda, Wilson Mukama, kumetutia ganzi baadhi yetu ambao kwa muda mrefu tumekuwa ‘mashabiki’ au waumini wa kuchagiza kwa njia ya kalamu na wakati mwingine katika mijadala ya wazi kwamba, taifa lilikuwa na haja ya kutafuta mabadiliko ya uongozi kutoka nje ya chama tawala.

Sitaki kuwa miongoni mwa wapenda mabadiliko ambao kwa njia za kujifariji au za kujipa matumaini hewa wameingia katika mkumbo wa jumla jumla wa kumbeza Kinana kwa namna wanayotaka kuuaminisha umma wa Watanzania kwamba, mtu huyo anaweza akasukumwa kirahisi kwa namna ile ile ilivyopata kuwa kwa watangulizi wake kadhaa waliopata kushika wadhifa huo.

siku zote nilikuwa nikiamini kwamba, ukatibu mkuu kwa Kinana ilikuwa ni silaha moja ya maangamizi kwa vyama vya upinzani ambavyo naamini vinapaswa kuendelea kupewa fursa ya kuaminiwa na kukomaa.

Kinana anaendelea kubakia kuwa tishio kubwa kwa ustawi wa upinzani ambao ni rutuba muhimu kwa maendeleo ya demokrasia na misingi ya utawala bora.

Hili ndilo ambalo naamini wapinzani wanapaswa kulitazama na kulitafakari nyakati hizi wanapoendesha harakati zao za kukabiliana na maguvu ya dola na haya mapya ya hoja ambazo aghalab zitaongozwa na Kinana nyakati hizi taifa linapojiandaa kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa miaka mitatu ijayo.

Haitoshi kwa kina Freeman Mbowe, Profesa Ibrahim Lipumba, James Mbatia, Dk. Willibrod Slaa na Zitto Kabwe kumbeza Kinana na timu ya watendaji wake eti kwa hoja nyepesi na zisizo na mashiko za ufisadi au uchafu wa jumla jumla wa CCM.

Wapinzani na wachambuzi wa mambo wanapaswa kujua na kutambua kwamba, Kinana ni mwanasiasa wa vitendo, msomaji mzuri wa vitabu, ripoti, taarifa, magazeti, msikilizaji na msikivu mzuri wa mambo mepesi na mazito kuliko alivyokuwa ‘utopia’ Mukama anayeamini na kuzitetea nadharia zisizotekelezeka.

Si hilo tu, wapinzani wanapaswa kutambua kwamba, historia yake ya uaskari alioutumikia miaka 20 hadi mwaka 1972 akifikia cheo halisi cha jeshi cha Kanali ikimhusisha na mafunzo mahususi ya kimkakati ni sehemu ya mambo ambayo yanatawala nidhamu ya kazi ya aina ya kipekee iliyomfanya Kinana akawa jemedari wa mapambano ya CCM tangu mwaka 1995 hadi leo.

Wachambuzi wa mambo, nikiwamo mimi mwenyewe ambao siku zote tumekuwa tukiiona CCM kuwa chama kinachokufa kwa maana ya kuchungulia kaburi, tunapaswa kuanza kutafakari upya mawazo yetu hayo, nyakati hizi Kinana alipopewa dhamana ya kuwa mtendaji wake mkuu.

Tutakuwa wendawazimu iwapo tutamlinganisha Kinana na Mukama na kusahau kwamba huyu aliye kilingeni leo ndiye aliyemuongoza Benjamin Mkapa katika mapambano makali ya kisiasa mwaka 1995, zama Augustine Mrema alipokuwa tishio la kwanza la kweli dhidi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu.

Alikuwa ni Kinana aliyefanya kazi kubwa katika kipindi chote cha kampeni akiratibu na kuongoza kampeni zote za Mkapa zilizomjumuisha pia Mwalimu Nyerere katika mazingira ambayo wengi walikuwa wakiamini CCM ilikuwa katika mwelekeo wa anguko la kihistoria.

Kinana ambaye kabla ya mwaka 1995 alikuwa tayari amepata kuwa Naibu Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Waziri wa Ulinzi alitumia vyema mbinu za medani na zile za kidemokrasia na kidiplomasia kumjengea uhalali Mkapa ambaye wakati huo alikuwa mwanasiasa ambaye hakuwa akijulikana sana.

Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba, siku chache tu baada ya kuingia Ikulu kwa mara ya kwanza mwaka 1995, kwa sababu ama ya ulevi wa madaraka au kwa kutingwa na kazi za kimamlaka, Mkapa alisahau kazi kubwa aliyofanyiwa na Kinana.

Ni katika kipindi hicho cha kati ya mwaka 1995 na 2000 ndipo nilipokutana kwa mara ya kwanza na mara kadhaa na Kinana nyumbani kwake Masaki, jijini Dar es Salaam ambako nilipata fursa ya kumsikiliza na kuufahamu upeo mkubwa wa kuona mambo aliokuwa nao mwanasiasa huyo.

Tangu wakati huo hadi wakati wa kampeni za mwisho za mwaka 2010, niliendelea kukutana kwa nyakati fupi fupi na Kinana na mara kadhaa nikawa mtu wa kufuatilia na kuzisikiliza kwa makini, habari zake kutoka ama kwa marafiki au maadui zake wa kisiasa.

Sikushangazwa hata kidogo niliposikia tena kwamba, Mkapa alilazimika kumuangukia tena Kinana na kumuomba aongoze tena kampeni zake mwaka 2000 kabla ya Kikwete naye hajafanya kile alichofanya mtangulizi wake alipomuomba mwanasiasa huyo adhibiti joto la kiti cha urais mwaka 2010.

Uwezo wake mkubwa wa kisiasa, umakini wake na upeo mkubwa alionao katika kuona na kuchambua masuala ya siasa, uchumi na jamii ndivyo vitu ambavyo kwanza kwa nyakati tofauti vimepata kumfanya Kinana awe Mbunge wa Jimbo la Arusha kwa miaka 10, Mbunge wa Afrika Mashariki na Spika wa Bunge hilo.

Si ajabu hata kidogo kwamba, hata kabla ya kufikia huko, ni Kinana huyo huyo ambaye alipata kuwa Mwakilishi wa Kidiplomasia wa Rais wa Tanzania katika eneo la Maziwa Makuu na kabla ya hapo akiwa Mwenyekiti wa Mawaziri wa Ulinzi wa Nchi za Kusini Mwa Afrika (SADC) zama akiwa Waziri wa Ulinzi katika Serikali ya Awamu ya Pili iliyokuwa ikiongozwa Rais Ali Hassan Mwinyi.

Uzoefu wake katika siasa za kiraia unaanzia mwaka 1972 wakati alipostaafu jeshi akiwa Kanali baada ya kulitumikia kwa miaka 20 ndiyo ambao amekuwa akiutumia kama silaha kubwa ya kukijua chama chake na pengine kumfanya awe mmoja kati ya watu wachache ambao wamepata kuwafanyia kazi marais wote wane wa Tanzania.

Anarithi mikoba ya Mukama akiwa mmoja wa wanasiasa wachache wa CCM wa rika ile ile la kina Kikwete ambaye alilikimbia na kulikana kundi la mtandao mwaka 2005 ambalo baadhi yetu tunaamini kuwa, ndilo lilisababisha kuzaliwa kwa siasa mpya za kupakana matope, kuzushiana na kuhujumiana ndani na nje ya CCM.

Lakini pengine kubwa katika yote hayo anaingia madarakani huku akiwa na hazina ya uzoefu mkubwa wa kuongoza mapambano dhidi ya vyama vya upinzani na kushinda katika mazingira ambayo aghalab yamekuwa yakiacha vidonda visivyopona kwa wapinzani tangu mwaka 1995. Huyu si mtu wa kumpuuza au kumbeza hata kidogo.

Angalia huyu ana post ngapi ?
 
Kweli Kinana ni Jemedari...ni Kiongozi shupavu....Mpiga kampeni mzuri wa CCM...Sijui kanali na mengineyo....ila tatizo sio mzalendo
Ametumia CV yake hiyo na umaarufu wake huo kufanya ujangili....Tanzania tuna mpango wa kuufanya utalii kuwa ndio source kubwa ya mapato nchini...wakati Kinana anapambana kumaliza kile kinachowaleta watalii.....
Hapa ndio nataka kuamini Kinana ni msomali!
 
Kibanda aliwahi kuandika kua Kinana ataleta tabu...watu hatukumuelewa
 
Wewe ni Absolom Kibamba?... Umempamba kweli, nilidhani hujapona bado uko hospitalini!!
 
Watu wengine bana wakilewa kahawa na kashata wakati wanacheza dhumna pale Saigon basi hujiamuliatu kutoa uzi hapa JF,kisa naye ajulikane eti anamuelewa sana Kinana,mbona ya Loliondo na pembe za ndovu huyaandiki?
 
Back
Top Bottom