Mkuu unawezaje kuamini Swala la bahati, ikiws huamini uwepo wa Mungu,
Labda nikuulize bahati ni nini, unawezaje kuthibitisha mambo ya bahati ,
Swali zuri.
Bahati ni jambo kutokea bila kupanga, bila kulifanyia kazi. Randomly. Na bahati haihitaji uwepo wa Mungu.
In fact, bahati/ randomness inaonesha kuwa Mungu hayupo. Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote angekuwepo, bahati isingewezekana kuwapo. Kwa sababu bahati inaweza kumpa kitu kizuri mtu mbaya na kumpa kitu kibaya mtu mzuri.
Mungu wa haki angekuwepo, asingeruhusu bahati iwepo.
Kwa hivyo, hakuna contradiction kusema Mungu hayupo na bahati ipo.
Kuna mambo katika maisha yanatokea kwa bahati tu.
Yule Hasheem Tahabit unafikiri asingezaliwa na bahati ya kuwa mrefu angefika NBA?
Huchagui wala hufanyii kazi kuzaliwa, unajikuta tu umezaliwa kwa bahati tu.
Nchi unayozaliwa, huchagui wala huifanyii kazi, inatokea kwa bahati tu.
Vinasaba unavyozaliwa navyo huvipati kwa kufanyia kazi, unavipata kwa bahati tu.
Wazazi waliokuzaa huwachagui, unajikuta umezaliwa na wazazi hao kwa bahati tu.
Socio economic class unayozaliwa hujaipanga wewe, unajikuta tu umezaliwa familia ya Kifalme ya Uingereza au mtoto wa Kapuku.
Sasa Prince William wa Uingereza akiwa anafurahia maisha mazuri sana kuliko mtoto wa kapuku wa Nangurukulu utasema hakuna bahati ya kuzaliwa iliyosababisha hivyo?