Ukweli mchungu kwa Walokole wote duniani, hamtamuweza Shetani, mtazaliwa kuzeeka na kuondoka hamtamuweza na dunia itabaki

Wakala wa Shetani katika ubora wake...
 
Shetani na mungu ni marafiki huwa wanakutana mara kibao wanapiga story, mda mwingine huwa wanabet kabisa wanaweza kumchukua binadamu mmoja wakampa mateso ya kutosha ili waangalie nani mkeka wake utatiki
 
Mpaka hapo tu ushampiga hat trick uyo kondoo wa bwana hapo juu.

Kwa kifupi tu huyo mungu mwenyewe alimshindwa shetani huko mbinguni akamtupa duniani, na duniani pia kamshindwa ndo maana aliwapa adhabu adam na Eva ila alishindwa kumpa adhabu shetani
Kuna kitu hakipo sawa kwenye haya mafundisho na ukijaribu kuhoji unatishiwa ziwa la moto ndo maana nasema tukiondoa moto wafia dini wengi wanaleft sababu wapo pale kiunafiki, uhalisia ni kuwa wanapenda maisha ya raha na starehe za hii dunia ila tatizo ni moto. Walokole wanapenda Mwanamke mzuri, minyama nyama, kinywaji n.k
 
Watu wengi wanajitungua tu nani aliyemuona huyo shetani?

nani aliyempa jina la sheitani?

anafanya mambo machafu kwa sababu gani kwa nini ashindane na binadamu wakat yeye wa milele?

eti mungu kamshindwa shetan yaan mungu hatengeneze kitu kilicho juu ya uwezo wake?

hivi wewe mleta mada una akili kweli au ndo wakala wake na sheitan?
 
Mpaka hapo tu ushampiga hat trick uyo kondoo wa bwana hapo juu.

Kwa kifupi tu huyo mungu mwenyewe alimshindwa shetani huko mbinguni akamtupa duniani, na duniani pia kamshindwa ndo maana aliwapa adhabu adam na Eva ila alishindwa kumpa adhabu shetani
Baba yake anampenda sana kilichomfanya amwelewe ni umaridadi wake wa kuzichapa mwisho akaona kweli nina kidume
 
Nakupa za ndani hakuna sehemu niliyomchonganisha baba yake nimesema baba yake anajivunia kuwa na kidume ndo mana anampenda na usijidanganye kuwa kuna siku baba yake atamfanyia baya hilo sahau
 
Shetani ni roho ila wewe ni roho iliyofichwa ndani ya mwili wenye damu na nyama... Dunia asili yake imeundwa kuufavour ulimwengu wa damu na nyama kuliko ulimwengu wa kiroho, na kitu kibaya pindi tu unapozaliwa mambo yote unayoanza kuyazoea ni yale ya kuufurahisha na kuuburudisha mwili ili kukufanya uweze kuwa comfortable na huu ulimwengu, kwa hiyo kutokana na hilo watu wengi wanaishi pasipokujua kwa nini wapo hapa duniani kwasababu mambo ya ulimwengu yanatupambaza hadi tunashindwa kukonekti mwili na ule ulimwengu wa kiroho ili tuweze kuwa bora zaidi ya huyo Shetani.

Ndio maana kuna msemo unasema dunia sio ya watu wadhaifu, hii haina maana yoyote katika ulimwengu wa mwili ila unamaana kubwa katika ulimwengu wa kiroho.

Ni kweli Shetani hana shida na watu kama wewe ila kuna watu wako na hatima za kiuungu ndani ya roho zao ndio watu ambao Shetani anashida nao sana.

Hao vibwengo uliowataja wapo katika safu ya utawala wa Shetani ni sawa na waamini wanaposema malaika.

Shetani ni yuko very powerful kama ulivyosema na ako na himaya yake hapa duniani na huu ulimwengu uko na watu wanaobeba hatima za kutimiza malengo ya Shetani ambao hawa ndio watu wenye nguvu na ni watu wenye ushawishi mkubwa na ndio watu wanaoogopwa kwenye kila ngazi ambayo wanaiwakilisha.

Lakini agenda zao wanazozitimiza huwa hazina faida wala muunganiko wowote na roho ila agenda zao zimekaa kwa namna ya kimwili lengo ni kukufanya wewe uliyebeba agenda za kiuungu ndani yako upumbazike hadi ushindwe kufikia lile lengo lililofanya Mungu wako akulete kwenye hili eneo la majaribio (roho zote zilizopo duniani zipo kwenye majaribio) kwahiyo dunia sio sehemu ya maisha ndio maana kuna deadline, ila wengi wanajua ingawa si kwauhakika kabisa kwamba kinachokufa ni mwili na sio roho, hiyo ni kweli na baada ya pale ndio maisha huanza rasmi kwa zile roho zote ambazo zimefanikiwa kutimiza yale malengo yaliyowafanya wawe hapa duniani na ndio huko mnaita paradise.

Wale waliobeba maono ya kiungu wengi wao wanaishi hadi wanakufa hawafanikiwi kama ulivyosema ndugu muandishi kwasababu duniani ili ushinde lazima uwe na nguvu.

Kwahiyo hatuko hapa kwaajiri ya kushindana na shetani ila tuko hapa kwaajiri ya kutimiza hatima zilizotufanya tuwe katika ulimwengu huu mgumu upande wa kiroho ila mrahisi upande wa kimwili.

Ndugu muandishi, usimuogope shetani ila ogopa deadline ikifika ukiwa bado hujamaliza kazi uliyopewa uifanye. Asante.
 
Nimekuelewa vuzuri sana kiongozi, wapo watu wanaojindanganya watamuangusha Shetani ndiyo maana nikawambia wasipoteze muda wao hakuna watakachoweza na kama wapo tayari kupoteza muda waingie kwenye 18 zake mwisho watamuona mshindi ni nani kati yao na yeye
 
Kwanza kabisa, thibitisha Shetani yupo kweli na habari za kuwepo kwake si hadithi za kutungwa na watu tu.

Cc Fine Wine
 
Sio hadithi za kutungwa ni kweli yupo, watu wengi wanakosa uhakika kwasababu ya kukosa sifa za kumfikia

Acha longolongo nyingi.

Kwanza kabisa, thibitisha Shetani yupo kweli na habari za kuwepo kwake si hadithi za kutungwa na watu tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…