Muisraeli
Member
- Aug 25, 2020
- 45
- 82
Haisaidii mkuu, hata msigwa kuna watu hawakuamini hivyohivyoMe ntakuwa mtu wa mwisho kuamini mtu kama Lissu au Heche kuwa wanaweza wakaenda CCM……Haiwezekani kabisa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Haisaidii mkuu, hata msigwa kuna watu hawakuamini hivyohivyoMe ntakuwa mtu wa mwisho kuamini mtu kama Lissu au Heche kuwa wanaweza wakaenda CCM……Haiwezekani kabisa
Mimi si mwanachadema na wala sina chama lakini kwa hilo nakuunga mkono. Msigwa kasema mengi ambayo ukweli wake wanaujua wanachadema na viongoxi wenzake lakini kwa uzito wa hizo shutuma ingekuwa jambo la kingwana kwa Mbowe kukaa pembeni na kupisha uongozi mwingine na ikiwezekana uchunguzi ufanyike ili kubaini ukweli na kurudisha imani ya wanachama. Mahala ilipofika CHADEMA Sasa hivi kuna wengi tuna matumini nayo ili kuleta mabadiliko ya kweli nchini hususan. Shutuma anazotoa Msigwa inarudisha nyuma juhudi na mafanikio yote yaliyopatikana Hadi sasa. Kwa bahati mbaya mambo haya yanatokea wakati tumekaribia sana uchaguzi na kwa kikosa muda wa kurekebisha. Namdihi sana bwana Mbowe na viongozi wenzake wazingatie jambo hili tusije tukakatishwa tamaa wote tuliokuwa na matumini na chama hili.Asalaam ndugu zangu!!!
Ifahamike;Mimi ni Mwana CHADEMA tena sio Mwana CHADEMA wa kuhamia lahasha!!! Bali ni Mwana CHADEMA wa kuzaliwa…….nimezaliwa nikamkuta mzazi wangu mmoja ni Mwana mageuzi,hivyo nami nikawa Mwana Chama wa hiki Chama kwa kwa Kurithi kutoka kwa Bi’Mkubwa wangu…………Nikienda kujenga hoja msinichukulie Kama Chawa wengine kutoka CCM,Mimi ni kamanda kweli kweli✊🏿✊🏿
Kwanini nasema Mbowe apumzike au asigombee kabisa Muhula huu;
•Mbinu za kuendeshea Chama kwa sasa zimemuishia,Amekaa kwenye Uenyekiti wa Chama kwa zaidi ya miaka 20 na kila siku mbinu za harakati za Siasa zinabadilika ila yeye bado anaamini kwenye Siasa za kiungwana yaani bado anafikiri CCM anaweza kutoka kwa kuombwa aachie nchi😂😂😂………..CHADEMA inawahitaji watu majasiri kama Tundu LISSU,John Heche,Ezekiel Wenje etc
•Kiongozi anaposhindwa kuleta ushindi,anapaswa kupumzika ili kuachia mtu mwenye mawazo mbadala asongeshe gurudumu mbele la harakati………Mbowe kashindwa kwa sasa na anapaswa kuachia ngazi
•Aking’atuka atakiwezesha Chama kutoka kile zile tuhuma kuwa Chama kinaendeshwa kama Mali ya familia na ukoo wa kina Mbowe……….kwa hapa atakuwa amewafunga mdogo Ma-CCM pamoja na vibaraka wao ACT-Wazalendo
Ni hayo tu kwa Leo ila kiukweli,nitamshangaa sana tena sana kama huyu Kamanda Mkuu atachukua fomu ya kugombea wadhifa wowote ndani ya chama……anapaswa kuwa Mshauri tu kama walivyo kina Mabere Marando,Jakaya Kikwete, au Zitto Kabwe (japo huyu ameachia Chama kwa wapemba coz huku bara Chama hakina mvuto kabisa)
Akiendelea ipo siku Wanachama tunao jielewa tutampindua Kama alivyofanywa James Mbatia
Aluta continua,victory ascalerta✊🏿