Ukweli mchungu kwa Wana CHADEMA; MBOWE anapaswa kupumzika

Mimi si mwanachadema na wala sina chama lakini kwa hilo nakuunga mkono. Msigwa kasema mengi ambayo ukweli wake wanaujua wanachadema na viongoxi wenzake lakini kwa uzito wa hizo shutuma ingekuwa jambo la kingwana kwa Mbowe kukaa pembeni na kupisha uongozi mwingine na ikiwezekana uchunguzi ufanyike ili kubaini ukweli na kurudisha imani ya wanachama. Mahala ilipofika CHADEMA Sasa hivi kuna wengi tuna matumini nayo ili kuleta mabadiliko ya kweli nchini hususan. Shutuma anazotoa Msigwa inarudisha nyuma juhudi na mafanikio yote yaliyopatikana Hadi sasa. Kwa bahati mbaya mambo haya yanatokea wakati tumekaribia sana uchaguzi na kwa kikosa muda wa kurekebisha. Namdihi sana bwana Mbowe na viongozi wenzake wazingatie jambo hili tusije tukakatishwa tamaa wote tuliokuwa na matumini na chama hili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…