Ukweli mchungu Ni kuwa Tundu Lisu Hawezi Kuwa Rais Wa Nchi Hii, Hana sifa za kiuongozi za kuwa Mkuu Wa nchi

Ukweli mchungu Ni kuwa Tundu Lisu Hawezi Kuwa Rais Wa Nchi Hii, Hana sifa za kiuongozi za kuwa Mkuu Wa nchi

Hivi kwenye kaghetto kako utakuwa umeandika CHADEMA makenchini.Unaipenda sana.
Nitakipendaje chama Kama hicho kilicho kosa Sera na ajenda za kueleweka? Mtu mwenye Akili Timamu utaanzaje kujiunga mkono au kushabikia chama Kama Chadema? CCM ndio Tumaini la wanyonge na Tegemeo letu vijana tunaojitambua
 
Ndugu zangu huo ndio ukweli kuwa Tundu Lisu Hawezi Kuwa Rais Wa Nchi Hii ya Tanzania, Hata Kama angezaliwa kabla ya Uhuru na kuwepo wakati huo na ikatokea uchaguzi, bado Lisu asingepewa nafasi ya kuwa Mkuu Wa nchi Hii ya Tanzania, kwa kuwa anakosa sifa za kiuongozi anazopaswa kuwa nazo Mkuu Wa nchi

Tundu Lisu Ni Mtu asiye na kifua, busara, Wala hekima za kiuongozi, Hana Subira Wala uvumilivu wa Jambo lililo katika kifua chake, Amejaa mihemuko na jazba kubwa Sana, Amejaa ujana ambao tunasema anawaka Kama Moto wa petroli mahali panapohitaji busara na hekima za kiuongozi, Ni mtu ambaye Hawezi kuwaunganisha watu wa makundi yote, Rika zote, vyama vyote na wenye mitizamo na mielekeo tofauti ya kisera na kiitikadi katika ujenzi wa Taifa letu, kwake yeyote atakayetofautiana Naye Basi huyo mtu ataitwa Hana akili au Ni mpumbavu, Ndio maana ya kauli zake za kusema hayo Ni Maccm au policcm

Lisu amenyimwa kipawa na uwezo wa kuweza kuwaunganisha watu hata anaotofautiana nao maana asio elewana nao kimtizamo au kisera au kiitikadi anawaona akili hazipo kichwani, Ni mtu anayeweza kutoa hata Siri za Taifa letu kwa kujuwa kuwa hiyo ndio demokrasia yenyewe au uwazi bila kujari kuwa Kuna Mambo yanapaswa kubaki Siri za Taifa kwa usalama wa Taifa letu,Ndio maana Lisu anaweza kutoka kufanya mazungumzo na Mtu ambayo yanapaswa kufanywa Siri kwa muda fulani wakati baadhi ya mambo yanasubiliwa kukamilika lakini yeye akitoka hapo akabanwa kidogo utakuta anaanza kuyaongea yote hadharani ili kuwafurahisha watu wake.

Lisu Ni Mtu ambaye Hana sifa ya kuviongoza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama Kama Amiri Jeshi mkuu ,maana Hana busara Wala hekima ya kuweza kuviunganisha na kuviweka pamoja na kuvijengea morali kutokana na kauli zake za dharau na kianaharakati harakati kwa kila Jambo

Lisu Hawezi kutujengea umoja na mshikamano wa kitaifa zaidi anaweza kulisambalatisha Taifa letu ndani ya muda mfupi Sana, maana kwake yeye anahisi anajuwa na kufahamu kila kitu na haupaswi Wala hapaswi kupingwaa Wala kukosolewa maamuzi yake au kauli zake au mtizamo wake , Ni Rahisi Sana kupandikiza chuki ndani ya Taifa letu kwa kujenga Hisia za sisi na wao yaani Hawa Ni wenzetu na wale siyo wenzetu na hawana akili

Lisu Hawezi utatuzi wa migogoro Wala kuwa mfariji wa Taifa letu kwa kuwa Hana kauli Nzuri afunguapo mdomo wake au kinywa chake,

Lisu hajuwi Ni wakati gani wakuongea na wakati gani wakukaa kimya, hajuwi wakati gani wakujibu na wakati gani wakukaa kimya, hajuwi aongee maneno gani na wakati gani, hajuwi kuwa ukiwa kiongozi mkubwa hupaswi kujibu kila swali la mwandishi au mtu unalojuwa litaleta hisia tofauti au migogoro au chuki fulani au kuhatarisha usalama wa Taifa au kufichua Siri fulani yenye maslahi ya Taifa

Hajuwa Kama kiongozi Kuna wakati wa kukaa kimya kuvuta Subira kuwa mvumilivu kujishusha kusubiri taarifa sahihi , kusema subiri kwanza Hilo Jambo litatolewa ufafanuzi Baadaye kidogo, yeye Lisu anataka ajibu kila kitu hata ambacho hakipaswi kujibiwa na kufahamika kwa wakati huo kwa maslahi mapana ya Taifa letu, Lisu anaweza akataja hata idadi na aina ya silaha zetu, mizinga au ndege Vita na Hadi zinakokaa Kama akiulizwa na waandishi wazungu huko ulaya

Lisu Hafahamu kuwa mdomo wa kiongozi unapaswa kuwa na breki na kuzungumza pale panapohitajika, hajuwi kuwa mdomo wa kiongozi haupaswi kuongea kila kitu hata Kama shangwe zinaunguluma kila Kona ya jukwaa, Hafahamu kuwa mdomo wa kiongozi unapaswa kuwa Kama chujio na siyo kuwa Kama dodoki linalozoa na kunyonya kila kitu na ukilikamua linatoa Tena yote


Lisu Ni mjuaji Sana anayehisi anajuwa kila kitu, anahisi anaweza kila kitu, anahisi hastahili kujifunza kutoka kwa yeyote, anahisi hapaswi kushauriwa na yeyote, anahisi Hakuna darasa jingine au taaluma nyingine zaidi ya madarasa aliyopita na taaluma aliyonayo, anahisi hata walimu wake hawana akili kwa Sasa ya kumueleza kitu, anahisi yeye ndio katiba itembeayo na maktaba ya kila kitu,hajuwi kuwa uongozi na kiongozi Kuna wakati unapaswa ukubali mawazo ya wenzio kwa kupunguza kidogo kutoka uliyokuwa unayaamini awali na kuyasimamia,

Lisu abaki kuwa mwanaharakati na mtu anayepaswa kuongozwa, Lisu hapaswi kuwa ndio top, Hapaswi kuwa wamwisho kimaamuzi Anapaswa kuwa na mtu juu yake Aliyejaa hekima busara upendo unyenyekevu uvumilivu Subira utu uzima na moyo mkubwa ili kumtuliza muda wote Na kumuelekeza kwa hekima na busara bila mikwaruzano, maana naamini Lisu Hawezi kubadilika hivyo alivyo kwa kuwa ndivyo alivyo zaliwa,

Kazi iendeleee , Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka

Lucas Mwashambwa kijana mzalendo na mpenda nchi yangu

Akili ndogo hujadili watu baadala ya issues.
 
Akili ndogo hujadili watu baadala ya issues.
Issues Ni sifa za mtu anayeweza kuwa kiongozi na vipi mtu anaweza asiwe kiongozi hasa ngazi ya Urais asipokuwa na sifa hizo, mfano ndio huyo Lisu kuwa hawezi Kuwa Rais hapa Tanzania na hata asingezaliwa hapa Tanzania bado asingepata Urais popote na katika nchi yoyote Ile yenye watu wanaojitambu
 
Huyo mtu wenu hata Mbowe hakutaka awe mgombea wenu Ndio maana kwenye kampeni zake alitengwa hata na Mwenyekiti wake,
Nani alikuambia hayo maneno yenye uongo?Ukaacha kumfuatilia "maliyemu" anasemaje ukawa umetega sikio CHADEMA wanasemaje?Huo ni umbeya.Hiyo tabia acha.Ukiendelea nayo hautahama hapo kwa shemeji yako.
 
Nani alikuambia hayo maneno yenye uongo?Ukaacha kufuatilia "maliyemu" ukawa umetega sikio CHADEMA wanasemaje?Huo ni umbeya.Hiyo tabia acha.Ukiendelea nayo hautahama hapo kwa shemeji yako.
uliona Mbowe akiambatana na huyo mtu wenu kwenye kampeni Kama ilivyokuwa uchaguzi wa 2015 wakati wa mh lowasa au 2010 wakati wa Dr Slaa? Kwa ufupi Ni kuwa hata Mbowe mwenyewe hamkubali jamaa maana anajuwa jamaa Hana sifa za Urais Wala hawezi Kuwa Rais Wa Nchi hii
 
Issues Ni sifa za mtu anayeweza kuwa kiongozi na vipi mtu anaweza asiwe kiongozi hasa ngazi ya Urais asipokuwa na sifa hizo, mfano ndio huyo Lisu kuwa hawezi Kuwa Rais hapa Tanzania na hata asingezaliwa hapa Tanzania bado asingepata Urais popote na katika nchi yoyote Ile yenye watu wanaojitambu
Kaa utulie basi.Hadi umechachamaa kama umeambiwa umedokoa kichwa cha samaki kwenye chungu!
 
Kaa utulie basi.Hadi umechachamaa kama umeambiwa umedokoa kichwa cha samaki kwenye chungu!
Mimi sijachachamaa Ila nimewaambia ukweli ambao Ni mchungu kwenu, Najuwa mnachanganyikiwa hasa baada ya kuwa mnajuwa ukweli kuwa huko kwenu mna uhaba mkubwa wa viongozi ndio sababu ya kuokotezana okotezana hasa baada ya wenye akili kuwakimbia na kuwaacha wenyewe mkihangaika
 
Mimi sijachachamaa Ila nimewaambia ukweli ambao Ni mchungu kwenu, Najuwa mnachanganyikiwa hasa baada ya kuwa mnajuwa ukweli kuwa huko kwenu mna uhaba mkubwa wa viongozi ndio sababu ya kuokotezana okotezana hasa baada ya wenye akili kuwakimbia na kuwaacha wenyewe mkihangaika
Na ndiyo maana wakitoka CDM wanapewa uongozi huko jalalani.
 
Back
Top Bottom