Ukweli mchungu ni kuwa Yanga havuki hatua ya makundi

Ndugu zangu WAna yanga pamoja ya kuwa tumemfunga geita gold goli tatu baada ya mapumziko na simu nyingi kwa viongozi WA geita ila bado ukweli kazima usemwe ya kuwa kuwa timu yetu itaishia MAKUNDI tu na Sio vinginevyo...
Hii post yako inatusaidia nini?

Ni sawa na kusema umeota shule fulani haitafaulisha wakati wanafunzi wapo wanaendelea na masomo.

Sioni jipya sana sana utakuwa umewakatisha tamaa!
 
Ningependa kuona Yanga na Simba zote zinaingia robo itakuwa ushindi kwa soka letu na ukweli tunahitaji sana kufanya hivyo.

Taratibu tuchukue nafasi ya Kongo kwenye ukanda huu wa afrika mashariki na kati,tukienda na nusu hii Sasa ni bonus.

NB: Mimi shabiki wa yanga
 
Ukimaliza kujifariji, kaa chini urudie kusoma uzi kwa makini
 
Ndugu zangu WAna yanga pamoja ya kuwa tumemfunga geita gold goli tatu baada ya mapumziko na simu nyingi kwa viongozi WA geita ila bado ukweli kazima usemwe ya kuwa kuwa timu yetu itaishia MAKUNDI tu na Sio vinginevyo...
Pole kwa frustration baada ya yanga kurudisha goli na kushinda tatu
Ndo game lilivyo
 
yanga anaongoza hili kundi,huo ndo ukweli mchungu.
 
Kipindi msimu unaanza

"Yanga msahau kuhusu ubingwa kabisa" sasa hivi gape ni point 8

" Yanga inabebwa ngoja mechi za kimataifa zianze " zilipoanza sasa michuano hiyo ni myepesi.

" Mazembe hawezi fungwa na Yanga " baada ya mechi
mazembe hii sio mazembe Ile.

" Bamako anakuja kumpiga Yanga hapa kwa mkapa" baada ya mechi Bamako hana tofauti na ruvu shooting.

Wana Simba tutaacha kujifariji lini? Mpira ni uwanjani na sio mapambio .
 
Yule Kiongozi wao mstaafu aliyewaita mbumbumbu mashabiki wa aina hii, hakika aliwaza mbali sana.
 
Kuna yule jamaa anajiita sijui itobo au itobe alileta utabiri kabla ya mechi na baada ya mechi jamaa alipotea mazina😂😂
 
Madunduka mnapitia katika wakati mgumu ubora Yanga unawafanya muifuatilie zaidi kuliko timu yenu
 
yote kheri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…