Simjui, hanijui. Simtetei bali natoa maoni yangu katika hiyo situation. Suala la uzinifu wewe ni nani wa kulizungumzia? Wewe ni msafi kiasi gani mpaka uwe hakimu wa suala la 'uzinifu'? Btw, nani alikuambia kuwa 'wazinifu' hawaruhusiwi kuwazika wanaume au wanawake waliokuwa wakizini nao? kwanini mnaacha kujadili mambo ya msingi mnakimbilia kujadili masuala ambayo hata hamuwezi kuyathibitisha? Kwa hiyo mke wa Madoda alimwacha mumewe awe anazini na Catherine, halafu akasubiri afe ili amwadhibu mwanamke mwenzake kwa kujaribu kumzuia kuja kumzika na kutupa shada lake la maua? Mnaangalia historia ya Catherine, nani aliwadanganya kuwa Mungu huwa anajihangaisha na historia? Hovyoo!