Ukweli Mchungu: Serikali Haiwezi Kuendesha SGR Kwa Watanzania Tuliopo. Tujifunze Kutoka Kwenye Mwendokasi

Ukweli Mchungu: Serikali Haiwezi Kuendesha SGR Kwa Watanzania Tuliopo. Tujifunze Kutoka Kwenye Mwendokasi

Huihui2

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
7,021
Reaction score
11,475
IMG-20240614-WA0104.jpg

Mbona barabarani kuna makampuni kibao,
Makampuni kwenye SGR yawe mengi, yalipe tu kiwango fulani serikalini kisha yapige kazi.

Tumeona kinachoendelea kwenye Mwendokasi ni aibu tu na mateso kwa abiria. Tusikubali SGR ifike huko. BINAFSISHA mara MOJA kama anavyosema Waziri Mbarawa
 
ALIEKWAMBIA MWENDO KASI INAENDESHWA NA SERIKALI 100% NI NANI? UDART SIO SERIKALI NDUGU NI KAMPUNI TANZU, NDIO MAANA MABASI YAO HAYANA PLATE NUMBER YA SU, NA KODI YA IMPORTATION WANALIPA
 
View attachment 3017687
Mbona barabarani kuna makampuni kibao,
Makampuni kwenye SGR yawe mengi, yalipe tu kiwango fulani serikalini kisha yapige kazi.

View attachment 3017688

Tumeona kinachoendelea kwenye Mwendokasi ni aibu tu na mateso kwa abiria. Tusikubali SGR ifike huko. BINAFSISHA mara MOJA kama anavyosema Waziri Mbarawa
Kumbe nguvu ya soda tu Seikali haiwezi kuendeleza mradi mkubwa kama huo sio rahisi. Bora wametoa fursa kwa wawekezaji Wananchi waje nao kuwekeza katika huo mradi. Kazi Iendelee Mama Samia.
 
Watu weusi tuna matatizo sana. Wakati treni hii inafanya majaribio ya miundombinu mlianza kuponda ile speed eti treni gani ina speed ndogo kuliko Bus, mkaambiwa hii ni Test ya miundombinu tu. Leo hii treni imefanya safari kwa dakika 114 hamjasifia ila mmekuja na ukosoaji ambao ni unforeseen.
 
ALIEKWAMBIA MWENDO KASI INAENDESHWA NA SERIKALI 100% NI NANI? UDART SIO SERIKALI NDUGU NI KAMPUNI TANZU, NDIO MAANA MABASI YAO HAYANA PLATE NUMBER YA SU, NA KODI YA IMPORTATION WANALIPA
Umeishia darasa la ngapi wewe!!!
 
Watu weusi tuna matatizo sana. Wakati treni hii inafanya majaribio ya miundombinu mlianza kuponda ile speed eti treni gani ina speed ndogo kuliko Bus, mkaambiwa hii ni Test ya miundombinu tu. Leo hii treni imefanya safari kwa dakika 114 hamjasifia ila mmekuja na ukosoaji ambao ni unforeseen.
Ni kitu kinachotukwamisha, upigaji, ufisadi, wizi na ujambazi kwenye mali za umma.

Mendokasi wamepewa monopoly kwa route zote muhimu bado wanashindwa tatizo ni uongozi, usimamizi, msimamiaji.

Mtu mweusi hakuna anachoweza, labda pombe na ngono!
 
😄😄😄 sawa sawa
 
SGR inatakiwa kufika Mwanza na Kigoma haraka na kusafirisha mizigo ya nchi jirani kwa haraka na tuanze kuchota pesa za majirani na kuua uchumi wa Kenya hizo ndio zilikuwa ndoto za Magu , hii ya kutubeba abiria ni ziada tu ya SGR sasa mwenyewe kaenda mbwembwe kama zote.

Inapaswa mkubwa aambiwe tukope bila hofu SGR imalizwe haraka kujengwa ifike Mwanza na Kigoma kwakuwa ni reli ya kimkakati kubeba mizigo ndio lengo mama na kuifanya bongo kama Ulaya yaani donor country. Yule mwamba hakunaga!he had royal dreams ambazo Mama amezielewa,amezibeba na anazitekeleza kwa nguvu zote !

Mbwembwe za kubeba abiria kwa buku teni hazitalipa mkopo na kwa maana hiyo tozo tulizochoka za mwanayanga zitaendelea kutudidimiza kwenye umaskini. Wakumbuke duniani tunapita tu

Mama ameweza, maua mengi kwake, Mama mitano mingine!
 
Serikali haijawahi kufanikiwa kwenye mradi wowote kuanzia ndege,mwendokasi,madini,gesi,treni,meli,uvuvi,utalii nk. nk.

Huu niuthibitisho kuwa viongozi wajuu serikalini hawana uwezo,ujuzi wala maarifa katika kusimamia miradi na kuipeleka nchi mbele.

Kimsingi serikali yetu inatumia pesa nyingi mmmno kutufanyia kazi ndooogo sana ndomana ikipewa miradi yoote inafilisika!!

Mfano Ikulu ingepewa mradi uuendeshe ili kupata mapato ya kujihudumia ninauhakika ikulu ingegeuka gofu chakavu na watumishi wake wangelala njaa...
Nivile inajiendesha Kwa kodizetu na wanazila bila kujali maana hawana uchungu nazo
Tizama raisi anasafiri kilaleo Tena saanyingine anasafiri na wasanii ughaibuni bila kujali gharama kuubwa bila tija kwakuwa hawazitafuti pesa wanazichota tuu!!!

Kila taasisi(wizara) ya serikali ingekabidhiwa mradi mmoja kama chanzochake pekee cha pesa za matumizi na kodizetu zikatumika tuu kwa huduma nyingine kunaviongozi/mawaziri wangekondeana, wangevaa viraka na kuendesha baiskeli chakavuu.
Narudia Tena "Hatuna viongozi wenye uhodari wowote labda wakuvaa masuti na kumsifu alowapa kulayao".
TURUDI KWENYE ELIMU YETU...
 
View attachment 3017687
Mbona barabarani kuna makampuni kibao,
Makampuni kwenye SGR yawe mengi, yalipe tu kiwango fulani serikalini kisha yapige kazi.

View attachment 3017688

Tumeona kinachoendelea kwenye Mwendokasi ni aibu tu na mateso kwa abiria. Tusikubali SGR ifike huko. BINAFSISHA mara MOJA kama anavyosema Waziri Mbarawa
Hakuna tunachoweza,majibu kamili mtapata baada ya uchaguzi wa 2025 yaani ripoti ya CAG #2026.

Hii ni miradi cosmetics ya kufurahisha wajinga ila itaendelea kula Kodi na Kodi kuiendesha.
 
Kwa kifupi serikali ya CCM inaajiri vilaza sifa wanayoangalia zaidi ni uwe chawa.
Swala sio vilaza Bali Mwendazake Alikurupuka,wrong timing and decion na mara nyingi watu wasio na akili hukombilia hizi structures Ili kuwapumbaza mbulula.

Reli zote Duniani hujengwa kuliwa na uhitaji wa kiuchumi na sio vinginevyo

Mwisho tunaenda kujenga expressway ya kulipia Dom-Dar kabla ya 2030 itakuwa tayari nani atapanda hiyo treni yenu hususani VIP? Mtu ataona Bora alipie toll kwenye Barabara ajiachie na km 120-200/hr.
 
Back
Top Bottom