Swala sio vilaza Bali Mwendazake Alikurupuka,wrong timing and decion na mara nyingi watu wasio na akili hukombilia hizi structures Ili kuwapumbaza mbulula.
Reli zote Duniani hujengwa kuliwa na uhitaji wa kiuchumi na sio vinginevyo
Mwisho tunaenda kujenga expressway ya kulipia Dom-Dar kabla ya 2030 itakuwa tayari nani atapanda hiyo treni yenu hususani VIP? Mtu ataona Bora alipie toll kwenye Barabara ajiachie na km 120-200/hr.
Inasikitisha sana. Ina maana sasa imeshakubalika kuwa serikali haitakuwa tena na uwiano katika mipango ya kitaifa maendeleo (
national integrated development planning)? Serikali ya CCM imejenga SGR kwa gharama kubwa sana inayojumuisha
mass passenger transportation component. Halafu serikali hiyo hiyo inapanga kutumia gharama kubwa tena kujenga expressway kwenye corridor hiyo hiyo kama vile hii ni nchi yenye uchumi wa dunia ya kwanza! Inahitaji miundombinu shindani kuwapa raia wake “
wide choice”! Tena kwa mikopo zaidi!
What’s going on? Umuhimu wa kugawa pesa za umma za maendeleo kwa sekta mbali mbali kwa uwiano sahihi umetupiliwa mbali? Sasa kila Rais anataka kufanya “miradi yake” kuwapiku wenzake wa awamu zingine? Yaani, tunakubaliana na wajinga/wapumbavu waliozuka na kutamalaki miaka hii wanaofikiri Rais bora ni yule “mwenye maono; anayebuni miradi ya ‘kimkakati’”?
Halafu hayo mahangaiko ya kutaka SGR ionekane ikisafirisha abiria ni ujinga mwingine usioelezeka. Taaluma zimetupiliwa mbali enzi hizi! Watu hawajiulizi ilikuwaje reli zetu za awali za TRC na TAZARA zikafikia hapo zilipo? Bahati mbaya hakuna documentary clip ya TAZARA watu waone ilivyokuwa wakati TAZARA inazinduliwa ikiwa brand new na kila kitu kimekamilika.
Kiuchumi, gharama ya kuendesha treni ni kubwa sana inaweza kufidiwa tu na kiwango kikubwa cha usafirishaji mizigo mizito (
bulky) kwa umbali mrefu (=>1000km). Vinginevyo, inabidi abiria watozwe nauli kubwa sana kufidia gharama za uendeshaji na faida kidogo. Tanzania miaka yote gharama za safari za treni ya abiria (TRC/TZR) zimekuwa zikifidiwa (
subsidised) na safari za treni ya mizigo. Ulaya waliachana na mchezo wa
cross-subsidisation miaka mingi tu. Nauli za abiria katika treni ni ghali kuliko za mabasi.
Baada ya mageuzi makubwa ya kiuchumi yaliyochagizwa na IMF na Benki ya Dunia, makampuni binafsi ya malori yalivamia soko ndio ikawa mwanzo wa kudorora kwa TRC na TZR. Hakuna hatua za kisera zilizochukuliwa kubadilisha hali hiyo. Lakini viongozi wetu wamekimbilia kumwaga matrilioni ya mikopo kujenga SGR. (Sijui kama
feasibility study ilifanyika). Sasa hao wanasiasa na wananchi wanaona raha kuanza kupanda treni kwenda Morogoro na Dodoma bila kujiuliza hatma ya huo mradi!
Ni hasara sana kwa nchi kama Tanzania kutekeleza mipango yake kwa propaganda za kisiasa badala ya uhalisia wa vigezo vya uchumi. It’s just a matter of time, the reality will finally settle on the SGR and ATCL, the most amazing follies that I know and still wondering at.