Ukweli mchungu, Tanzania bado Hatuna chama pinzani thabiti na imara kinachoweza kupambana na dola!

kitalembwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2014
Posts
8,216
Reaction score
21,914
Wasalaam!


Moja kwa moja kwenye mada, Tanganyika baada ya kupata Uhuru, tulikuwa kwenye mfumo wa chama kimoja (TANU) , baadae ikazaliwa CCM, kadri siku zilivyokwenda mwaka 1992 tukaingia rasmi kwenye mfumo wa vyama vingi ,,, hapa vikazaliwa vyama kadhaa ikiwemo NCCR-MAGEUZI, TLP, CHADEMA nakadhalika!

Mwaka 1995 rasmi tukashiriki kwa Mara ya kwanza uchaguzi kwa mfumo wa vyama vingi ,,, kuanzia hapo mpaka Leo.,, Tumeshuhudia viongozi wengi wa vyama vya upinzani wakitokea huku na kule kunadi, kugombea vyeo mbali mbali kupitia vyama vyao !!!

Miaka hiyo tunaanza mfumo wa vyama vingi NCCR ndio ilikuwa tishio chini ya kiongozi wake Augustino Lyatonga Mrema , baadae CHADEMA kikachukua hatamu Kama chama chenye nguvu upande wa upinzani !

Twende kwenye hoja ya msingi, bado Tanzania Hatuna chama makini ambacho viongozi wake wapo tayari kukipigania kudai haki ! Tumeona sarakasi nyingi Sana za Hawa viongozi, kuanzia kwa kina Mrema (huyu Ni Kama ccm B tu wengi wanamjua), Lipumba , wakaja kina Dr Slaa na wengineo, Hawa wote Ni wachumia tumbo,,,,

Kidogo lissu anaonekana ana uchungu na nchi yake , nae haaminiki , Kuna namna flani anatumika na watu fulani kwa malengo fulani ,
Mbowe sijamgusa, huyu anawezekana ana chembe chembe za demokrasia na mabadiliko kuliko hao wengine lakini nae Ni mchumia tumbo(rejea kilichotokea back then 2015) , Sina ushahidi, inasemekana alipokea mkwanja mrefu kutoka kwa bwana mvi , akampa nafasi ya kupeperusha bendera ya chama ,,, !

Hii awamu iliyoisha (2015-2020) yalitokea mengi Sana kwa upande wa upinzani, Hama Hama zile , Mara watu kununuliwa n.k ,, Hawa ndio viongozi tunaotegemea wachukue nchi waongoze ? Wasioweza ustahimilivu ? Hapana Ni ngumu Sana !

Uchaguzi ulioisha juzi hapa October, kila mtu aliona wazi kilichotokea , sihitaji kuelezea, chadema wakaambulia mmbunge mmoja ,, baadae wakatakiwa kupeleka majina ya viti maalumu, taarifa ya chama ikasema haitopeleka majina, kina bulaya, mdee na wengineo naskia walifanya vikao vya siri chama dola then wakaunda majina yao wakapeleka kibabe ,,, Hawa Hawa kina mdee na bulaya tuliwaona wafia chama nao wamegeuka ? Ndio tuliotegemea viongozi wa demokrasia makini ? Hapana nakataa!

Kwa mtindo huu , Tanzania Ni wazi Hakuna chama kinachoweza kuja kuchukua dola kwa miaka ya hivi karibuni, tuhitaji watu walitayari/waliojizatiti! Tuendelee kupambana tu na chama tawala CCM ! Na niseme kuwa , licha ya kutaka mabadiliko, sisi wananchi wenyewe hatuka tayari kwa mabadiliko, itachukua miongo kadhaa ama karne kabisa ili tuwe tayari !

Wacha tuendelee kuzisoma tarakimu !!!
 
Ndo muwe mnatuelewa wenye akili tunavyowambia Tanzania hakuna vyama vya Upinzani Bali magenge ya Wahuni tu.

CDM ni mfano hai tosha kabisa.
 
Chadema chini ya Mbowe msakatonge ndo chama makini kabisa kuwai kutokea Tanzania.
 
Haya ni mawazo ya kipumbavu sana. Ni mawazo ya kipumbavu kwa sababu wewe unadhani chama ni ''dude'' litakalotumika kukupigania wewe/kuwapigania watanzania wakati wewe/watanzania wamekaa miguu juu na wanaangalia kama movie! Upumbavu wa kiwango cha juu.

Wanaopambana na dola ovu kama hii ya Magufuli ni wewe/watanzania wote wapenda maendeleo na haki. Sehemu zote zilizopata mabadiliko ni wananchi walijitokeza kwa wingi kupigania haki zao.

Unajua historia ya kupagania ubanguzi wa rangi Afrika Kusini? Kama wewe/watanzania wataendelea kukaa kinyonge na kutegemea kuwa kuna siku litatokea dude linaloitwa ''chama'' kuwapigania haki zao basi utaishia kujiharishia kwa tabu za maisha. Hili ni kwa watanzania wote bila kujali wanatoka chama gani.
 
Waruhusu wagombea binafsi wasio na chama hata kimoja halafu uone

jinsi watu walivyochoka vyama vyote vilivyopo madarakani
Hawawezi kuruhusu kwa sababu wanajua ndiyo mauti yao. Nachoweza kukuambia ni kuwa ukisubiri eti kuna siku wataruhusu basi siku hiyo haitatokea. Haki haitolewi bali hudaiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…