Haya ni mawazo ya kipumbavu sana. Ni mawazo ya kipumbavu kwa sababu wewe unadhani chama ni ''dude'' litakalotumika kukupigania wewe/kuwapigania watanzania wakati wewe/watanzania wamekaa miguu juu na wanaangalia kama movie! Upumbavu wa kiwango cha juu. Wanaopambana na dola ovu kama hii ya Magufuli ni wewe/watanzania wote wapenda maendeleo na haki. Sehemu zote zilizopata mabadiliko ni wananchi walijitokeza kwa wingi kupigania haki zao. Unajua historia ya kupagania ubanguzi wa rangi Afrika Kusini? Kama wewe/watanzania wataendelea kukaa kinyonge na kutegemea kuwa kuna siku litatokea dude linaloitwa ''chama'' kuwapigania haki zao basi utaishia kujiharishia kwa tabu za maisha. Hili ni kwa watanzania wote bila kujali wanatoka chama gani.