Ukweli mchungu, Tanzania bado Hatuna chama pinzani thabiti na imara kinachoweza kupambana na dola!

Ukweli mchungu, Tanzania bado Hatuna chama pinzani thabiti na imara kinachoweza kupambana na dola!

Siku zote angalia Ugali wako na familia yako, haya mambo ya Siasa sio ya kuyatolea msuli hata kidogo.

Watu wanaweka mbele Maslahi kuliko Uzalendo
 
Watanzania ndio walioisaliti Chadema hivyo acheni kuwalaumu kina Halima na wenzake.
 
But this was obvious from the beginning. Hata zile slogan za #NiYeye ilikuwa kujipa faraja ya muda mfupi
 
Ndivyo inavyosemwa siku zote kwa maneno lakini CCM ambao wanajua kuwa CHADEMA haijafa na haifi leo pamoja na upinzani wote kwa ujumla hawakubali kufanya uchaguzi huru na wenye haki kila uchaguzi unapofika wana weka mpira kwapani na kupiga kura kabla ya siku ya uchaguzi ili iwe rahisi kuzibeba kwenye mifuko ya viroba wakati wa kuzitumbukiza kwenye sanduku la kura.
Point yako Ni ipi mkuu ! Tz bado Kuna upinzani wenye tija ?
 
Toa huo ujinga kichwani wakuamini katika watu tena binadamu aina hii ya watanzania.Watanzania ndo hawa hawa wanaopatikana kwenye hivi vyama.kwahiyo linapokuja swala la mabadiliko kama kweli wewe ni mfuasi wa mabadiliko piga vita kuhusu mabadiliko popote ulipo.Lakini kama utakaa usubiri hadi waliokwenye chama fulani wakupiganie utakua hufikiri sawasawa.Jiunge timu mabadiliko bila kujali wakina nani wanashukia njiani.kwasababu sio lazima wewe ndo uone kile unachokiamini nakukipigania.it takes times kufikia mabadiliko kwahiyo pambana ata kwa vizazi vijavyo.
Nyuma ya keyboard
 
Tatizo sio Chama au Wapinzani. Tatizo liko kwa Watanzania ambao robo tatu yao hawajui wanataka nini.

Waliompa misukosuko mwalimu Nyerere walikuwa vijana wachache ambao ni "radicalised" kama akina Eugene Maganga na Kapteni Mohamed Tamimu na wala sio Wapinzani!!!
Damu/mioyo ya Aina hiyo haipo cku hz
 
Siku zote angalia Ugali wako na familia yako, haya mambo ya Siasa sio ya kuyatolea msuli hata kidogo.

Watu wanaweka mbele Maslahi kuliko Uzalendo
Hawana uzalendo hata robo
 
Watanzania ndio walioisaliti Chadema hivyo acheni kuwalaumu kina Halima na wenzake.
CHADEMA yenyewe inaeleweka ndo watanzania waiunge mkono ? Viongozi sio wazalendo
 
nilipWasalaam!


Moja kwa moja kwenye mada, Tanganyika baada ya kupata Uhuru, tulikuwa kwenye mfumo wa chama kimoja (TANU) , baadae ikazaliwa CCM, kadri siku zilivyokwenda mwaka 1992 tukaingia rasmi kwenye mfumo wa vyama vingi ,,, hapa vikazaliwa vyama kadhaa ikiwemo NCCR-MAGEUZI, TLP, CHADEMA nakadhalika!

Mwaka 1995 rasmi tukashiriki kwa Mara ya kwanza uchaguzi kwa mfumo wa vyama vingi ,,, kuanzia hapo mpaka Leo.,, Tumeshuhudia viongozi wengi wa vyama vya upinzani wakitokea huku na kule kunadi, kugombea vyeo mbali mbali kupitia vyama vyao !!!

Miaka hiyo tunaanza mfumo wa vyama vingi NCCR ndio ilikuwa tishio chini ya kiongozi wake Augustino Lyatonga Mrema , baadae CHADEMA kikachukua hatamu Kama chama chenye nguvu upande wa upinzani !

Twende kwenye hoja ya msingi, bado Tanzania Hatuna chama makini ambacho viongozi wake wapo tayari kukipigania kudai haki ! Tumeona sarakasi nyingi Sana za Hawa viongozi, kuanzia kwa kina Mrema (huyu Ni Kama ccm B tu wengi wanamjua), Lipumba , wakaja kina Dr Slaa na wengineo, Hawa wote Ni wachumia tumbo,,,,

Kidogo lissu anaonekana ana uchungu na nchi yake , nae haaminiki , Kuna namna flani anatumika na watu fulani kwa malengo fulani ,
Mbowe sijamgusa, huyu anawezekana ana chembe chembe za demokrasia na mabadiliko kuliko hao wengine lakini nae Ni mchumia tumbo(rejea kilichotokea back then 2015) , Sina ushahidi, inasemekana alipokea mkwanja mrefu kutoka kwa bwana mvi , akampa nafasi ya kupeperusha bendera ya chama ,,, !

Hii awamu iliyoisha (2015-2020) yalitokea mengi Sana kwa upande wa upinzani, Hama Hama zile , Mara watu kununuliwa n.k ,, Hawa ndio viongozi tunaotegemea wachukue nchi waongoze ? Wasioweza ustahimilivu ? Hapana Ni ngumu Sana !

Uchaguzi ulioisha juzi hapa October, kila mtu aliona wazi kilichotokea , sihitaji kuelezea, chadema wakaambulia mmbunge mmoja ,, baadae wakatakiwa kupeleka majina ya viti maalumu, taarifa ya chama ikasema haitopeleka majina, kina bulaya, mdee na wengineo naskia walifanya vikao vya siri chama dola then wakaunda majina yao wakapeleka kibabe ,,, Hawa Hawa kina mdee na bulaya tuliwaona wafia chama nao wamegeuka ? Ndio tuliotegemea viongozi wa demokrasia makini ? Hapana nakataa!

Kwa mtindo huu , Tanzania Ni wazi Hakuna chama kinachoweza kuja kuchukua dola kwa miaka ya hivi karibuni, tuhitaji watu walitayari/waliojizatiti! Tuendelee kupambana tu na chama tawala CCM ! Na niseme kuwa , licha ya kutaka mabadiliko, sisi wananchi wenyewe hatuka tayari kwa mabadiliko, itachukua miongo kadhaa ama karne kabisa ili tuwe tayari !

Wacha tuendelee kuzisoma tarakimu !!!
Duhh ni nomaa
 
Sio hatuna chama pinzani thabiti. Hakuna wananchi wapinzani thabiti. Walipodhulumiwa kila mmoja hewala bwana! Watizameni Wa nigeria walivoingia barabarani walivopambana. Huku eti watu wanataka mabeberu waingilie kati ilhali aliedhulumiwa kakalia sofa anakula bisi akitizama youtube akitoka youtbe JF, akitoka hapo porno 😀
 
Sio hatuna chama pinzani thabiti. Hakuna wananchi wapinzani thabiti. Walipodhulumiwa kila mmoja hewala bwana! Watizameni Wa nigeria walivoingia barabarani walivopambana. Huku eti watu wanataka mabeberu waingilie kati ilhali aliedhulumiwa kakalia sofa anakula bisi akitizama youtube akitoka youtbe JF, akitoka hapo porno 😀
Mkuu nimecheka ! Hadi porno ?
 
Back
Top Bottom