Ukweli mchungu: Vifurushi vipya vya NHIF vitaumiza wanachama zaidi ya kikokotoo kinavyoumiza wafanyakazi

 
Nakubaliana na concept yako by 60% na uko sahihi ku focus kwenye mgonjwq maana huduma ya hospital ni wito kabisa na short of that utakiwi kuwa kwenye medical profession!! Hili nadhani liko wazi.

40% yangu nataka itambue kuwa wale watu wanaofanya kazi pale wana watoto, mama ,baba, wake na waume wa kutunzwa huko majumbsni kwao. Wanahitqji mishahara kutoka kwa mwajiri mwisho wa mwezi. Sasa kama wewe NHIF unaniletea wagonjwa wengi na wewe hutaki kunilipa onetime ili nami niwe na madaktari na wauguzi wa kutosha kulingana na wingi wa wagonjwa wako then hata mimi nina haki kukataa. Wa kwanza asiyejali ni wewe na lawqmq unakuja kuniangushia mimi. Hunisaidii ku deal na wagonjwa wako na yet ni wengi sana wanahitaji double or three times ya human resources and medicines resources ili kumudu nafanyaje? Obviously nitashindwa na nitafunga hospital na kufanya hata wale wateja wengine wakose huduma!!

Wewe NHIF umeishalipwq na wateja wako ili uwape huduma. Ila wewe hulipi wateja wako(mahospital). Inawezekana vipi uende kulaumu tena hospital? Ungewalipa kwa muda tuone.

Tatu kama unabadilisha modality ya bei basi na wewe NHIF jali wateja wako njoo mezani tujadili mapema na tu conclude siyo kuja kunilazmisha ghafla ukitaka nichukue watu wako.ambao ni wengiiii kwa hela ndogo ili hali na mimi nime engage madaktari wa juu tayari na ambao wana mikataba ya kazi siwezi kurudi kwao kushusha mishahara yao bila wao kuondoka na kugoma maana watadhsni nawaibia huku nalipwa fedha nyingi(coz ya NHIF na private hospital) a consultant doctor hajui yanayoendelea, he is a professional na hayo ni mambo ya administration huko, yeye anataka alipwe na administration issues his/her business!!

Na kumbukeni running a hospital ni sawa na ku run kiwanda ,its a 24hrs nonstop running shift ya employees na vifaa na madawa yawepo kwenye shelf kuwapa wagonjwa otherwise watu watakufia mapokezi na mgonjwa kufia mapokezi au hakupewa huduma ni unyama kwa medical professionals heri wangefunga aende kwingineko kuliko kumuua mlangoni kwao kisa huduma mbovu au dawa au vifaa havipo.

So aliyewaacha hapa watu njia panda ni NHIF na siyo hospitals. Kila jambo lina mwanzilishi na hapa ni NHif. Mimi naamini nhif hawajali. Most likely wanaona gharama ni kubwa kwa hiyo wameacha ku solve tatizo ili watu wahamie huduma za serikali ili wao wafanye savings , sometimes hizi nchi zetu hazijali. Nadhani mentality ni kuwa huduma haijakosq nendeni vituo vya afya au hospital za mikoa, deeper inside wanawaza kisiasa tu kuwa kwqnza wakulima wapiga kura wengi hawaendi huko ma private hospitals so no pressure ni hawa tu wafanyakazi wa serikalini wenye NHIF ndo wanaenda.

Again hapa anayeumia ni most likely ofisa wa serikali. Maana yule ambaye hana anendelea. Na wengi wenye bima binafsi including hao mawaziri wenyewe utakuta wana bima za Jubilee, strategies etc wanazitumiq kutibiwa Nairobi Hospital hata private hospital hapa wengi hawaendi.

Conclusion; hospital ni biashara na utu. Biashara izingatiwe ili huduma iboreke na utu uzingatiwe. Usiache watu njiapanda kisha ulaumu watu wanaolipa employees kuhudumia wateja wako.
 
Hospitali binafsi nazenyew wanamatukio yao, "mjazie jazoe vipimo bima italipa"

Ile nayo ni biashara kama biashara zingine tu
Karibu kila hospitali ina wawakilishi wa NHIF. Ina maana nao wanashiriki wizi mkuu?
 
wataumizwa vipi wakati wote walishiriki kukitengeneza? au na wewe ni miongoni mwa malipyoto
 
Na bado hamjasema ninyi wezi wakubwa ,mnataka panad mlipwe 500 wakati mtaani ni 250?mnafanya biashara kwenye afya za watu ,kama hautaki si unaacha hakuna aliyekulazimisha ,tibu kwa cash
Wewe ndezi hujawahi kuumwa wala kuuguza uone taabu ya kutumia bima ya NHIF. Tena ukae chini utulize tako kilaza mkubwa wewe!
 
wataumizwa vipi wakati wote walishiriki kukitengeneza? au na wewe ni miongoni mwa malipyoto
Tangu lini wanachama wa NHIF walishirikishwa kwenye mabadiliko ya bei na vifurushi? Leo umevuta cha wapi mkuu?
 
Kwanza. Naunga mkono pendekezo la kuwa na wanachama katika majadiliano yanayofanyyika badala ya haki ya sasa wanajadili wayu wengine ilihali wachangiaji wakiwekwa pembeni kana kwamba hawama mchango juu ya kinaghoendelea.

Tunakoelekea Nhif inaelekea kubaya kwani hata hizo dawa zinazopigiwa debe hazipo. Wiki moja iliyopita niliambiwa kwenda kununua dawa aina ya "furesimade" au la six. Na hiyo nni hospitali ya rufaa ya mkoa wa mwanza.

Kutokana na myukano unaoendwlea nimebaini kuwa kinachoitwa kitita kipya kwa hakika ni malipo mapya yatakayotolewa na mfuko kwa watoa huduma.

Kama issue ni hiyo na kuna nia njema ya kulimaliza suala hili, wekeni hadharani hiyo bei mpya kwani watanzania wataweza kuwashauri njia ya kufuata kuliko ujanja ujanja huu.

Na kwa jinsi hali inavyokwenda ndani ya Nhif ni matumaini yangu kuwa litaibuka jingine kubwa la kutatiza kuhusu mfuko huu ambak siku hizi kusogelea huduma zao na maofisa wao ni kama kuingia mbuga ya serengetj ukiwa ni mwindaji haramu.
 
Suala la Kitita kipya cha NHIF sio tuu linaathiri hospital za private tuu, bali hata za serikali. Bei nyingi haziko realistic. Bei ya bidhaa za afya mtaani ni kubwa kuliko fedha wanayolipa Bima. Mathalani, bei ya Cuevettes za kupimia wingi wa damu zinauzwa around 2000 Tsh, na Bima wanalipa kipimo cha wingi wa damu ( Hb) 1500 tsh. Hapo biashara lazima iwe ngumu. Nashauri serikali wakae, waliangalie upya suala hili ili kunusuru sekta binafsi ya afya. Tukumbuke kuwa, sekta hii imeajiri vijana wengi wa Kitanzania wanaotegemea ajira hizo kuendesha maisha yao ya kila siku.

Hata hospital za serikali, siamini kama wanakubaliana sana na kitita hicho, ila watu wanaogopa kusema tuu kwa sababu za kisiasa lakini ukweli ni kwamba, kitita hicho hakina tija kwa wananchi. Tutegemee wateja wa NHIF kutakiwa ku top up malipo ya baadhi ya huduma kwa baadhi ya hospital hasa za Private.
 
Karibu kila hospitali ina wawakilishi wa NHIF. Ina maana nao wanashiriki wizi mkuu?
sjajua kuhusu hilo , ila hospital nazo ni biashara zile, labda zolew kubwa sana ila za level ya kati muda mwingine unapimwa vitu vingine hata havina maana ili wafanye kazi
 
sjajua kuhusu hilo , ila hospital nazo ni biashara zile, labda zolew kubwa sana ila za level ya kati muda mwingine unapimwa vitu vingine hata havina maana ili wafanye kazi
Hilo lipo karibu kila hospitali inayotoa huduma ya NHIF
 
Reactions: Lax
Shida ilianzia pale kuchota mihela ktk mifuko ya kijamii,, walipoona utam wakaamia na NHIF,,

Utalalamika wapi? Na wenye Mpini ni wao? Ukikumbuka una familia inakutegemea basi unaamua kuchil,
 
Shida ilianzia pale kuchota mihela ktk mifuko ya kijamii,, walipoona utam wakaamia na NHIF,,

Utalalamika wapi? Na wenye Mpini ni wao? Ukikumbuka una familia inakutegemea basi unaamua kuchil,
Nchi ya kijinga sana hii ndugu yangu wewe acha tu miCCM iendelee kuitafuna nchi. Serikali ya CCM inawaona watanzania wote kama mazombie tu!
 
Natamani hili andiko alione kila mtu.
Umefafanua vizuri sana..🙏
 
Shida ni kwa wafanyakazi wa umma ambao ni lazima wajiunge na nhif ila kwa wale wa binafsi wengi wataachana na hii bima watajiunga na bima zingine.
 
Natamani hili andiko alione kila mtu.
Umefafanua vizuri sana..🙏
Leo serikali, NHIF na AFTHA wanakaa meza ya majadiliano kujadiliana kuhusu vifurushi vipya. Hili ndilo lilitakiwa kufanyika badala ya kuwakomoa wanachama. Inaonekana AFTHA wana uchungu na wagonjwa kuliko CCM na serikali yake. Hii ni nchi ya kiqumer sana..
 
Karibu kila hospitali ina wawakilishi wa NHIF. Ina maana nao wanashiriki wizi mkuu?
Kwani inachukua billion ngapi kumnyamazisha afisa wa NHIF ilu apige kimya watu wakifanya yao?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…