Hivi kabla ya kuandika huwa tunakuwa tumepata taarifa au. Hayo majadiliano na watoa huduma si yamefanyika kwa takribani miezi 8..NHIF ilipotaka kuanza kutumia huo utaratibu mpya si Waziri alisitisha ikabidi warudi kwenye meza ya mazungumzo sio peke yao bali awepo mediator ambayo TIRA ilihusika ku mediate.
Kwenye maridhiano yeyote kuna kupata na kuachia baadhi na hilo limefanyika.
Kutokubaliana kwenye baadhi ya masuala ni sehemu ya maridhiano.
Mgogoro wa gharama kubwa za tiba na dawa ambazo vituo binafsi vimekuwa vikipeleka bili zao zilipwe na NHIF ambazo hazilingani na bei ya soko au uhalisia huo ni ufisadi mkubwa wa fedha za wanachama.
Mf. Unakuta kipimo x ni sh 50,000 sehemu ya kwanza.. Kipimo hichohicho ni sh 80,000 sehemu ya pili.. Kipimo hicho hicho ni sh 250,000 sehemu ya tatu.. Halafu wote huko wanapeleka bill NHIF iwalipe kwa sababu wateja wa bima walipata kipimo hicho hicho sehemu tofauti tofauti hivi kweli wewe ndiye ungekuwa umepewa dhamana ya kusimamia hiyo michango ya wanachama ungefanya nini???
Ungeona ni sawa tuu.
Tukumbuke tumumbuke kuwa fedha zote zilizopo bima ya afya ni michango ya wanachama sio za serikali, nasisitiza ni za wanachama sio za serikali... Je wanachama wangepewa nafasi kuhudhuria hayo majadiliano juu ya suala la bei za huduma zisizolingana na uhalisia je unadhani wangekuwa upande gani?
Kosa nalo liona ni wachangiaji wa mfuko wa bima ya afya kutoshirikishwa kwa vile hakuna chama cha wachangiaji wa bima ya afya Tanzania.
Mijadala wanakaa wanaotaka kulipwa fedha yaani watoa huduma ambao kipaumbele kwao ni super profit kama ilivyo kwenye biashara yeyote..
Wanajadiliana na mtunza fedha za wanachama bila wanachama wenyewe kushirikishwa waamue juu ya gharama zipi wanaruhusu zikubaliwe au laa.
Kitakachoenda kutokea endapo bima ya afya wakikubaliana na suala la kila kituo kjiamulia chenyewe gharama za dawa na matibabu watakavyo na bima ikawalipa tuu... Mfuko huo lazima ufe....
Au viwango vya kuchangia lazima vipandishwe na mwanachama asilalamike na la tatu ambalo ndilo linaendelea sasa ni matibabu yamelimitiwa sana sana, masharti ni mengi na kuna huduma zitaendelea kuondolewa.
Mnaoenda hospital mnajionea jinsi huduma za bima siku hizi zilivyongumu utadhani unataka kuchukua mkopo benki.
Nakubaliana na concept yako by 60% na uko sahihi ku focus kwenye mgonjwq maana huduma ya hospital ni wito kabisa na short of that utakiwi kuwa kwenye medical profession!! Hili nadhani liko wazi.
40% yangu nataka itambue kuwa wale watu wanaofanya kazi pale wana watoto, mama ,baba, wake na waume wa kutunzwa huko majumbsni kwao. Wanahitqji mishahara kutoka kwa mwajiri mwisho wa mwezi. Sasa kama wewe NHIF unaniletea wagonjwa wengi na wewe hutaki kunilipa onetime ili nami niwe na madaktari na wauguzi wa kutosha kulingana na wingi wa wagonjwa wako then hata mimi nina haki kukataa. Wa kwanza asiyejali ni wewe na lawqmq unakuja kuniangushia mimi. Hunisaidii ku deal na wagonjwa wako na yet ni wengi sana wanahitaji double or three times ya human resources and medicines resources ili kumudu nafanyaje? Obviously nitashindwa na nitafunga hospital na kufanya hata wale wateja wengine wakose huduma!!
Wewe NHIF umeishalipwq na wateja wako ili uwape huduma. Ila wewe hulipi wateja wako(mahospital). Inawezekana vipi uende kulaumu tena hospital? Ungewalipa kwa muda tuone.
Tatu kama unabadilisha modality ya bei basi na wewe NHIF jali wateja wako njoo mezani tujadili mapema na tu conclude siyo kuja kunilazmisha ghafla ukitaka nichukue watu wako.ambao ni wengiiii kwa hela ndogo ili hali na mimi nime engage madaktari wa juu tayari na ambao wana mikataba ya kazi siwezi kurudi kwao kushusha mishahara yao bila wao kuondoka na kugoma maana watadhsni nawaibia huku nalipwa fedha nyingi(coz ya NHIF na private hospital) a consultant doctor hajui yanayoendelea, he is a professional na hayo ni mambo ya administration huko, yeye anataka alipwe na administration issues his/her business!!
Na kumbukeni running a hospital ni sawa na ku run kiwanda ,its a 24hrs nonstop running shift ya employees na vifaa na madawa yawepo kwenye shelf kuwapa wagonjwa otherwise watu watakufia mapokezi na mgonjwa kufia mapokezi au hakupewa huduma ni unyama kwa medical professionals heri wangefunga aende kwingineko kuliko kumuua mlangoni kwao kisa huduma mbovu au dawa au vifaa havipo.
So aliyewaacha hapa watu njia panda ni NHIF na siyo hospitals. Kila jambo lina mwanzilishi na hapa ni NHif. Mimi naamini nhif hawajali. Most likely wanaona gharama ni kubwa kwa hiyo wameacha ku solve tatizo ili watu wahamie huduma za serikali ili wao wafanye savings , sometimes hizi nchi zetu hazijali. Nadhani mentality ni kuwa huduma haijakosq nendeni vituo vya afya au hospital za mikoa, deeper inside wanawaza kisiasa tu kuwa kwqnza wakulima wapiga kura wengi hawaendi huko ma private hospitals so no pressure ni hawa tu wafanyakazi wa serikalini wenye NHIF ndo wanaenda.
Again hapa anayeumia ni most likely ofisa wa serikali. Maana yule ambaye hana anendelea. Na wengi wenye bima binafsi including hao mawaziri wenyewe utakuta wana bima za Jubilee, strategies etc wanazitumiq kutibiwa Nairobi Hospital hata private hospital hapa wengi hawaendi.
Conclusion; hospital ni biashara na utu. Biashara izingatiwe ili huduma iboreke na utu uzingatiwe. Usiache watu njiapanda kisha ulaumu watu wanaolipa employees kuhudumia wateja wako.