Mkwawe
JF-Expert Member
- Jun 10, 2016
- 3,132
- 5,508
- Thread starter
- #381
Kuokoka ndiyo nini?????kanisa lote la katoliki linaabudu misingi ya kishetan na halifanani kabisa na kanisa la kwanza la mitume. ukitaka kuamini hilo, fanya comparison ya kila kitu, weka kanisa la mitume la kwanza lile lililozaliwa siku ya pentecost upande mmoja na upande mwingine weka kanisa katoliki. anza kulinganisha;
1. kanisa la kwanza waliomba kwa Jina la Yesu tu, wakatoliki wanaomba kwa Jina la Yesu, la Maria, na wafu.
2. Kanisa la kwanza lilikuwa na misingi ya Roho Mtakatifu, watu waliookoka walikua wanajazwa Roho, katoliki hawaamini kujazwa Roho Mtakatifu na wanapinga wokovu. kitabu cha Matendo kinasema kanisa likaongezeka kwa wale waliokuwa wakiokolewa, watu walikuwa wanaokoka.wakatoliki wanahitaji kuokoka.
3. kanisa la kwanza kitabu cha Matendo liliombea wagonjwa, lilifukuza pepo, hadi ilifika kipindi Paulo au nisema Petro na mitume wengine walikuwa wanapita kivuli chao tu kikipita kwa mgonja anapona, kanisa katoliki hawawezi hata kuombea mtu aliyepagawa na mashetani tu, na wanapinga mambo ya kuombeaombea yasiyoendana na canon law.
4. kanisa la kwanza liliheshimu zaidi Biblia kuliko chochote, katoliki wanaheshimu canon law kuliko hata Biblia. ndio maana umeona ametokea padri US akapinga misimamo ya paoa hasa kwenye ushoga na transgenders, ila PAPA amemsimamisha na kumvua cheo.
5. kanisa la kwanza walikuwa wananena kwa lugha, katoliki ukinena kwa lugha wanakufukuza, hawataki kabisa kusikia icho kitu. hata wale karismatic wanaopambana kufuata system ya kuokoka wanafukuzwa kabisa kwenye makanisa.
yapo mengi ila ngoja niishie hapa. Wakatoliki wanaabudu dini, sio Mungu na hata uwaambie utasikia wanakwambia sisi ndio kanisa la kwanza, unawauliza kanisa la kwanza lilikuwa linaabudu kama ninyi? hawana jibu wanakwambia sisi ndio wa kwanza. Biblia yenyewe hawasomi, majority ya wakristo wasiosoma Biblia ni wakatoliki. Jueni ya kwamba, kwenda kanisani kila jumapili, kuamini kwamba ukifa utaombewa hukohuko kaburini ili usamehewe dhambi, ni uongo, mnahitaji kuokoka ili muepukane na jehanum ya moto. Mungu awasaidie.
Unaokoka vipi na huku hauna tumaini la maisha yako ya duniani
Neno la Mungu linasema "....atakayevumiliana hadi mwisho ndiye atakayeokoka.."
Je wewe umeufikia mwisho upi???
Unataka tuokoke kwenye kanisa lipi?
Mlima wa moto, mikocheni?
Ufufuo na uzima?
Kwa mzee wa upako?
Feel free church ya masanja mkandamizaji?
Ngurumo ya upako kwa Geor Davie?
Kimara temboni kwa kuhani musa?
Kwa Nicolas Suguye?
Full Gospel ya kakobe?
Kwa Rose shaboka?
Yaani nyie wenyewe hamjielewi hamna huo umoja wa ROHO MTAKATIFU halafu unatafuta madhaifu ndani ya ukatoliki ili mpate ukamilifu wenu?
Yote uliyoyaainisha hapo juu ni uongo mtupu
1. Wakatoliki tunaamini katika Mungu mmoja aliye na nafsi tatu wanaotenda kazi kwa namna yao... Mama Maria maombi take tunaamini yako karibu sana na mwanaye kwa kwa kuwa ni neo hilo la Mungu linalosema "..amebarikiwa kuliko wanawake wote.." ndilo linalotupa nguvu ya kuamini utukufu wake na nafasi take ndani ya kanisa.. Ni Kama wewe unavyomuamini mwamposa na mafuta take kuwa kupitia kukanyaga mafuta ya mwamposa ndiyo Yesu anakutendea nasi tunaamini mama take Yesu ana nafasi ya karibu kwa mwanaye juu ya kutuombea kwake. Watakatifu wapo walikuwepo nao tunaamini ni washindi huko mbinguni wanaimba na kusifu na kuabudu hivyo nasi tunatamani kuwa kama wao kwa kurejea maisha yao ya utakatifu na kiimani tunaweza kuwasiliana nao kupitia sala. Je sio neno la Mungu linalosema
Luka 15:7
Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.
Je ni akina Nani hao watakaofurahi? Sio malaika na watakatifu? Je kufahamu uwepo wa watakatifu ni dhambi?
Walokole mmepotoka na sio ajabu shetani alianza kuwasambaratisha nyinyi na vikanisa vyenu kabla ya kuja kutujaribu sisi
2. Hujui lolote kuhusu ukatoliki sisi tuna hadi sherehe na sala kwa ajili ya Mungu ROHO MTAKATIFU na wewe unasema hatuamini katika ROHO MTAKATIFU, kweli? Je kuwjazwa na ROHO MTAKATIFU ndiyo kuropoka "shikarabazakonendakafuekwa rama" huko ndo kujazwa na roho mtakatifu?
Tunaamini katika wokovu, tunaamini katika kuokoka ila kuokoka kwa roho na kweli, elewa neno kuokoka kwa roho na sio mwili huu na rohi inaokoka baada ya kuhitimisha safari ya ulimwengu huu. Huwezi kuwa kwenye bahari mahindi yakapiga baadaye yakapoa ukasema umeokoka ilhali ufukweni hujatia nanga, huo ni uongo na kujidanganya mwenyewe
3. Kanisa katoliki linaombea wagonjwa na kufukuza mapepo kwa huduma inayoitwa "EXORCISM" ila utofauti wetu na wenu ni kuwa nyie mtataka ITV, TBC, STAR TV, CHANNEL TEN, WASAFI TV, TVE, AZAM, Instagram, Facebook, Twitter, thread, Jamiiforums wote wajue kuwa nyie ni mahodari wa kutoa mapepo. Ile ni huduma inahitaji faragha ya wahanga ila sio kwenu nyie hamna staha
4. Biblia haikuwepo hadi kufikia karne ya 10, unabisha? Wakatoliki ndiyo waliokusanya vitabu vya manabii na mitume pamoja na kuiita biblia, je kwanini tusiheshimu kitu ambacho tumekipigania. Unaona msivyojua hata historia ya ukristu wa kale. Nyinyi walokole ni wajinga na hamjitambui na ndiyo maana mmekuwa mitaji ya matapeli. PUMBAVU zenu
5. Kunena kwa lugha hakukufanyi kwa mkristu Safi mbele za Mungu, hiyo ni karama Kama ilivyoainishwa na mtume Paulo
1 Wakorintho 14:4
Yeye anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake; bali ahutubuye hulijenga kanisa.
Na wakarismatiki huheshimika ndani ya kanisa isipokuwa tu wale ambao huenenda kinyume na taratibu zilizokuwepo hao hawawezi kuonge lugha moja nasi
Kama una hoja zingine sema tu wala usiishie hapo maana huko kwenu ndiyo kuchafu hata hapatamaniki, huko kila mtu mjuaji kila mtu anaijua biblia, kila mtu huko kwenu ana ndevu hajulikani Nani ana ndevu na Nani hana wote huko wanaamua cha kufanya kwa utashi wake eti hadi wachungaji wanawake hamna akili nyie mnaitukana injili na kumkosoa Kristu kumfanya aonekane mbaguzi kumbe ni upumbavu wenu na ujuaji wenu