UKWELI MCHUNGU: Wakatoliki wenzangu Papa Francis ni mjumbe wa shetani ndani ya kanisa

Kuokoka ndiyo nini?????

Unaokoka vipi na huku hauna tumaini la maisha yako ya duniani

Neno la Mungu linasema "....atakayevumiliana hadi mwisho ndiye atakayeokoka.."

Je wewe umeufikia mwisho upi???

Unataka tuokoke kwenye kanisa lipi?
Mlima wa moto, mikocheni?
Ufufuo na uzima?
Kwa mzee wa upako?
Feel free church ya masanja mkandamizaji?
Ngurumo ya upako kwa Geor Davie?

Kimara temboni kwa kuhani musa?
Kwa Nicolas Suguye?
Full Gospel ya kakobe?
Kwa Rose shaboka?

Yaani nyie wenyewe hamjielewi hamna huo umoja wa ROHO MTAKATIFU halafu unatafuta madhaifu ndani ya ukatoliki ili mpate ukamilifu wenu?

Yote uliyoyaainisha hapo juu ni uongo mtupu
1. Wakatoliki tunaamini katika Mungu mmoja aliye na nafsi tatu wanaotenda kazi kwa namna yao... Mama Maria maombi take tunaamini yako karibu sana na mwanaye kwa kwa kuwa ni neo hilo la Mungu linalosema "..amebarikiwa kuliko wanawake wote.." ndilo linalotupa nguvu ya kuamini utukufu wake na nafasi take ndani ya kanisa.. Ni Kama wewe unavyomuamini mwamposa na mafuta take kuwa kupitia kukanyaga mafuta ya mwamposa ndiyo Yesu anakutendea nasi tunaamini mama take Yesu ana nafasi ya karibu kwa mwanaye juu ya kutuombea kwake. Watakatifu wapo walikuwepo nao tunaamini ni washindi huko mbinguni wanaimba na kusifu na kuabudu hivyo nasi tunatamani kuwa kama wao kwa kurejea maisha yao ya utakatifu na kiimani tunaweza kuwasiliana nao kupitia sala. Je sio neno la Mungu linalosema
Luka 15:7
Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.

Je ni akina Nani hao watakaofurahi? Sio malaika na watakatifu? Je kufahamu uwepo wa watakatifu ni dhambi?

Walokole mmepotoka na sio ajabu shetani alianza kuwasambaratisha nyinyi na vikanisa vyenu kabla ya kuja kutujaribu sisi

2. Hujui lolote kuhusu ukatoliki sisi tuna hadi sherehe na sala kwa ajili ya Mungu ROHO MTAKATIFU na wewe unasema hatuamini katika ROHO MTAKATIFU, kweli? Je kuwjazwa na ROHO MTAKATIFU ndiyo kuropoka "shikarabazakonendakafuekwa rama" huko ndo kujazwa na roho mtakatifu?
Tunaamini katika wokovu, tunaamini katika kuokoka ila kuokoka kwa roho na kweli, elewa neno kuokoka kwa roho na sio mwili huu na rohi inaokoka baada ya kuhitimisha safari ya ulimwengu huu. Huwezi kuwa kwenye bahari mahindi yakapiga baadaye yakapoa ukasema umeokoka ilhali ufukweni hujatia nanga, huo ni uongo na kujidanganya mwenyewe

3. Kanisa katoliki linaombea wagonjwa na kufukuza mapepo kwa huduma inayoitwa "EXORCISM" ila utofauti wetu na wenu ni kuwa nyie mtataka ITV, TBC, STAR TV, CHANNEL TEN, WASAFI TV, TVE, AZAM, Instagram, Facebook, Twitter, thread, Jamiiforums wote wajue kuwa nyie ni mahodari wa kutoa mapepo. Ile ni huduma inahitaji faragha ya wahanga ila sio kwenu nyie hamna staha

4. Biblia haikuwepo hadi kufikia karne ya 10, unabisha? Wakatoliki ndiyo waliokusanya vitabu vya manabii na mitume pamoja na kuiita biblia, je kwanini tusiheshimu kitu ambacho tumekipigania. Unaona msivyojua hata historia ya ukristu wa kale. Nyinyi walokole ni wajinga na hamjitambui na ndiyo maana mmekuwa mitaji ya matapeli. PUMBAVU zenu

5. Kunena kwa lugha hakukufanyi kwa mkristu Safi mbele za Mungu, hiyo ni karama Kama ilivyoainishwa na mtume Paulo
1 Wakorintho 14:4
Yeye anenaye kwa lugha hujijenga nafsi yake; bali ahutubuye hulijenga kanisa.

Na wakarismatiki huheshimika ndani ya kanisa isipokuwa tu wale ambao huenenda kinyume na taratibu zilizokuwepo hao hawawezi kuonge lugha moja nasi

Kama una hoja zingine sema tu wala usiishie hapo maana huko kwenu ndiyo kuchafu hata hapatamaniki, huko kila mtu mjuaji kila mtu anaijua biblia, kila mtu huko kwenu ana ndevu hajulikani Nani ana ndevu na Nani hana wote huko wanaamua cha kufanya kwa utashi wake eti hadi wachungaji wanawake hamna akili nyie mnaitukana injili na kumkosoa Kristu kumfanya aonekane mbaguzi kumbe ni upumbavu wenu na ujuaji wenu
 
Roman Catholic ni kanisa lenye nidhamu sana, na haliendekezi mabishano. Hivyo unapolisema na kulichafua hutasikia ukijubiwa Kwa maana hawawezi bishana na mtu ambaye sio mwelewa.
Wapi nimelichafua kanisa
 
Tatizo kubwa kwa wakatoliki na ukatoliki ni kule kumkataa Yesu Kristo na Biblia kwa gharama ya kuambatana na vitu vingine kama kumshika Maria (tena wakufikirika), kumshika Papa na mapokeo ya wazee wa kale wa huko Roma.
Kwani Maria ameamwakosea jambo gani nyinyi walimwengu?

Kumshika papa shida iko wapi?

Wazee wa kale wa Roma ni akina Nani?
 
Ukweli ni huu..
Yesu alikamatwa na kuhukumiwa na Waroma kwa fitna za wayaudi..Baade askari wa Kiyahudi wakamsulubu kikatili kabisa. Baaae kuna wahuni wa Kirumi wakaiukia kwao Italy wakidai wao ni watakatifu wanamtukuza Yesu; Kumbuka hawa ni Waroma walewale waliomkamata kule Yerusalem na kumtia hatiani kwa kukashifu Miungu yao. Baadae kuna Makanisa nayo yakaanza kuwatukuza Wayahudi kwamba ni wateule na wanaweka bendera za Uyahudi Makanisani kwao;Kumbuka Wayahudi ndio walimsulubu na Yesu na ndio walikwenda kumshtaki kwa watawala wa Kirumi.

Majumuisho:
Huu ukristo unaofundiswa pale Rome sio ambao Yesu aliufundushi na hata kitabu alichowafundisha wale Warumi walikibadilisha na kuweka yale waliyoyataka wao. Warumi hawakutaka yale mafundisho sahihi yawafikie watu ndio maana hata kanisa lilitekwa kutoka Jeresulem hadi Ulaya. Leo eti kilatini ndio lugha ya kanisa badala ya Kigalilaya
 
Kwa hiyo, kwa kuandika haya ndiyo umeshuhudia ukweli? Mbona unajitekenya na kucheka mwenyewe?
 
Oneni huyu
 
Hata kama lakini hatuhami
Mnagamaje Sasa na mshakuwa na mizizi huko? Baba mtakatifu ndio kanisa na asemacho yeye limesema kanisa. Mnaweza kuona ni kawaida tu as maisha yakiendelea. Hapa mwanzo inawezakuwa ngumu kumeza😄.
 
Mnagamaje Sasa na mshakuwa na mizizi huko? Baba mtakatifu ndio kanisa na asemacho yeye limesema kanisa. Mnaweza kuona ni kawaida tu as maisha yakiendelea. Hapa mwanzo inawezakuwa ngumu kumeza😄.
Ni kweli nina mizizi ya ukatoliki lakini tangu hata kabla papa hajabariki ushoga nilishajitoa kitambo, kiufupi dini /dhehebu yoyote ile mimi napinga. Dini ni utapeli.
 
Ni Freemasonry na lazima afuate misingi yake.
Hapo kapandishwa cheo
 
umenena vyema, huu ndio ukweli mtupu... wakatoliki hata kuomba hawajui.. wao mpaka sala wanasoma vitini ndo wamesali hivyo, roho ya mpinga kristo italipotosha kanisa katholic, wana mambo mengi ya ajabu yasiyokuwa na msingi wa neno la Mungu.
 
Ni kweli nina mizizi ya ukatoliki lakini tangu hata kabla papa hajabariki ushoga nilishajitoa kitambo, kiufupi dini /dhehebu yoyote ile mimi napinga. Dini ni utapeli.
Unaishi vipi Sasa kumwabudu Mungu
 
Kumwabudu Mungu sio lazima kwenda kanisani. Kama unatambua lipi jema na lipi baya unamwabudu kivyakovyako.
Ndio ndio kwa hapa nakuunga mkono. Wapo manabii lakini nao wapo 🔥 sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…