UKWELI MCHUNGU: Wakatoliki wenzangu Papa Francis ni mjumbe wa shetani ndani ya kanisa

Hahahaaaaaaaa,dini ni kikundi tu watu wahuni ndo maana wanasisitiza zaidi sadaka kubwa
 
Credit; MsasaNews
ASKOFU MKUU ATENGWA KATIKA HUDUMA ZA KANISA KWA KUMKOSOA PAPA...

Na VENANCE JOHN

Askofu mkuu Carlo Maria Vigano ambaye ni aliwahi kuwa balozi wa papa nchini Marekani ametengwa na kanisa lake Katoliki baada ya kuwa mkosoaji mkubwa wa Papa Francis na kuwa na mwelekeo tofauti na imani ya kikatoliki.

Taarifa ya Vatican imesema kuwa Askofu huyo amekataa kutambua na kutii mamlaka ya Papa na kuikataa huduma ya komuniyo na waumini wa Roman Katoliki na mafundisho yake.

Mwaka 2018 Vigano aliwashangaza wengi alipomtaka Papa Francis kujiuzuru na mkutuhumu kuwa Papa Francis anajua shutuma na unyanyasaji unawakuta mafrateli (wanafunzi wa upadre) uliotekelezwa na Kadinali wa zamani wa Washington DC, Theodore McCarrick huku Papa Francis akishindwa kumchukulia hatua.

Wakati alipokuwa mwanadiplomasia wa Vatican (Balozi wa Papa) alitukumika kufanya kazi kwa niaba ya Papa.

Leo Vatican imeeleza kwamba Vigano ametengwa kufuatia mchakato wa hukumu kukamilika ingawa Askofu Vigano mwenyewe amesema hatambui uhalali wa mchakato huo.

Hivi karibuni Askofu huyo alisema kuwa kuchaguliwa kwa Papa Francis kuishika Upapa kungetakiwa kufikiriwa kuwa batili na kumtuhumu Papa kwa uzushi na imani potofu.

Pia amemtuhumu Papa kwa kuunga mkono na kuwafanya marafiki wa kanisa watu wa mapenzi ya jinsia moja (Mashoga).

Mwaka 2018 Vigano baada ya kumtaka Papa Francis ajiuzulu, maaskofu wengine walimuunga mkono askofu mkuu huyo kauli ambayo ilikosolewa na baadhi wa viongozi wa Kanisa.

Taarifa ya Vatican imesema kuwa Askofu mkuu huyo ili kuondolewa adhabu hiyo, mpaka akutane na serikali ya Kanisa inayoongozwa na Papa (Holy See
 
Du kazi ipoo
 
Siyo papa tu, kanisa lote ni wakala wa shetani.
 
Chanzo cha hii habari nina mashaka nacho kama ni chanzo sahihi. Ni kama kusoma tamko la serikali ya Tanzania kutoka Gazeti la Uganda au Rwanda wakati tunajua tamko la serikali tunaweza kulisoma ama kwenye tovuti ya Ikulu, kutoka tamko la waziri mwenye dhamana au mamlaka ya serikali yanayohusika nchini au vyombo vya habari vya serikali.
 
Uko sawa
 
Unabisha nini
 
Wakatoliki, hata tusemwe na mkatoliki mwenzetu au na asiye mkatoliki, tutakusikiliza, ukimaliza tunakuacha na kuelekea kanisani kusali, halafu kwenye kitimoto na bia.

WE HAMIA UNAKOTAKA...!!
 
Wakatoliki, hata tusemwe na mkatoliki mwenzetu au na asiye mkatoliki, tutakusikiliza, ukimaliza tunakuacha na kuelekea kanisani kusali, halafu kwenye kitimoto na bia.

WE HAMIA UNAKOTAKA...!!
Suala sio kuhamia kaka suala ni kuambiana ukweli ili tuwe huru. Kanisa sio papa Kanisa ni LA wote waamini hivyo tunapaswa kuishi katika haki na si mazoea
Yaani ukiongelea wakatoliki kindakindaki basi ni Mimi
 
Suala sio kuhamia kaka suala ni kuambiana ukweli ili tuwe huru. Kanisa sio papa Kanisa ni LA wote waamini hivyo tunapaswa kuishi katika haki na si mazoea
Yaani ukiongelea wakatoliki kindakindaki basi ni Mimi
Ukweli gani unausema. Na je hata unajua ukweli ni nini au ukoje au kusema tu kwamba unasema ukweli ndio ukweli? Ni ukweli gani unaousema na unauthibitishaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…