Ukweli Mchungu: Watanzania watalipenda sana Bunge lijalo

KARLO MWILAPWA

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2019
Posts
3,250
Reaction score
5,509
Habari WanaJF,

Binafsi ninaamini Bunge lijalo litakuwa ni Bunge la kufurahisha sana na lenye changamoto kuliko bunge lenye wabunge wengi Wa upinzani ndani yake. Ni bunge litakalojadili na kufanya maamuzi makubwa yenye maslahi mapana kwa taifa letu. Ni bunge litakalothibitisha ubora na viwango vyote vinavyotakiwa bila hata upinzani wa vyama kuwepo.

1. Watanzania wengi wanaamini kwamba, Saudi za wana-CCM bungeni ndio zimeleta mabadiliko tunayoyaona nchini yaliyotokea kwa kipindi kifupi sana. Na bado waliamini sauti zile zilikuwa chache kuleta maendeleo yaliyokusudiwa ndio maana kwa hiari yao wakaamua kulifanya bunge kuwa la wabunge Wa CCM tu. Hivyo naamini litakuwa ni bunge LA watanzania wote wapenda mabadiliko.

2. Binafsi naamini hoja zitazopelekwa bungeni, zitawagusa watanzania kwa asilimia karibu mia na zitapitishwa kwa asilimia kubwa na kufanya maamuzi magumu na makubwa kwa maslahi ya taifa kuharakishwa. Maamuzi hayo yatapendwa na watu na kulipenda binge licha ya kuwa litakuwa ni la karibu la chama kimoja.

3. Bunge lijalo litawasahaulisha watanzania juu ya hofu yao ya nafasi ya upinzani kwenye mfumo Wa vyama vingi vya siasa na wataona kuwa hata chama kimoja kinatosha kuelezea ukomavu wa demokrasia na kuleta mawazo mbadala wa sera.

Waliofikiri watanzania wataona bunge lijalo halina tija bila wingi wa wapinzani ,wamekosea sana bunge lijalo ndio litaloleta upinzani wa kweli wa hoja na mipango
 
Serikali ya CCM imetawala huyu ni Rais wa tano sasa.. matatizo ya mikataba badhirifu ilisainiwa na haohao, elimu duni bado tunayo, ukosefu wa ajira uko palepale, Rushwa, kazi za kujuana, matukio ya kutekana, mlundikano wa kesi na ahadi lukuki zisizotekelezeka huku mkiikumbatia katiba yenye utata mwenyekiti NEC anateuliwa na Rais. maji bado tatizo n.k

Nafikiri hakuna jipya litakalofanyika maana hata huko nyuma hakukuwa na wapinzani wa kusema watawashinda ndio zenu za ilimradi!
 
Hayo yalipaswa yaonekana kwenye vikao vya CCM kwanza. Kama CCM walikuwa wanaweza kuleta hoja za mvuto, walingoja mpaka wanajisi Uchaguzi kisha ndio waanze kuwa na mvuto?
 
Wana mpango wa kulirusha live.... mbali na Star TV, Channel 10 na baba lao TBC, wanajaribu kuongea na ITV na Azam pia ili watanzania waone utendaji wa bunge la CCM... hoja moja......kauli moja.
 
Habari WanaJF,

Binafsi ninaamini Bunge lijalo litakuwa ni Bunge la kufurahisha sana na lenye changamoto kuliko bunge lenye wabunge wengi Wa upinzani ndani yake. Ni bunge litakalojadili na kufanya maamuzi makubwa yenye maslahi mapana kwa taifa letu. Ni bunge litakalothibitisha ubora na viwango vyote vinavyotakiwa bila hata upinzani wa vyama kuwepo.

1. Watanzania wengi wanaamini kwamba, Saudi za wana-CCM bungeni ndio zimeleta mabadiliko tunayoyaona nchini yaliyotokea kwa kipindi kifupi sana. Na bado waliamini sauti zile zilikuwa chache kuleta maendeleo yaliyokusudiwa ndio maana kwa hiari yao wakaamua kulifanya bunge kuwa la wabunge Wa CCM tu. Hivyo naamini litakuwa ni bunge LA watanzania wote wapenda mabadiliko.

2. Binafsi naamini hoja zitazopelekwa bungeni, zitawagusa watanzania kwa asilimia karibu mia na zitapitishwa kwa asilimia kubwa na kufanya maamuzi magumu na makubwa kwa maslahi ya taifa kuharakishwa. Maamuzi hayo yatapendwa na watu na kulipenda binge licha ya kuwa litakuwa ni la karibu la chama kimoja.

3. Bunge lijalo litawasahaulisha watanzania juu ya hofu yao ya nafasi ya upinzani kwenye mfumo Wa vyama vingi vya siasa na wataona kuwa hata chama kimoja kinatosha kuelezea ukomavu wa demokrasia na kuleta mawazo mbadala wa sera.

Waliofikiri watanzania wataona bunge lijalo halina tija bila wingi wa wapinzani ,wamekosea sana bunge lijalo ndio litaloleta upinzani wa kweli wa hoja na mipango
U mjinga sana.
 
Back
Top Bottom