Nakwambia hivi, Tanganyika kwa sasa ndio inatusitiri sisi wazanzibar. Bila Tanganyika hatuna ulinzi, usalama wala umeme.
Karafuu iliyokuwa inatupa jeuri ilishakufa kitambo sana, na kwa uvivu wetu tumeshindwa kuifufua, na sasa tunasikia huko Tanganyika mlishaanza kuotesha na kuvuna karafuu yenu kwa fujo.....
Bandari ya Zanzibar iko mahututi maana kila jirani yetu (Beira, Mombasa, Comoro, Eritrea, Djibout, Dar, Mtwara, Tanga) alisha imarisha bandari yake, Zanzibar hatuna tena upekee wa kibandari....
Zanzibar tumebakia na Utalii pekee yake (ambao ni wa msimu, na watalii wenyewe wengi huanzia bara au kumalizia bara maana huko wako huru kuvaa chochote, kula mwaka mzima (huku kula hadharani kipindi cha Ramandan ni mwiko!), kula chochote (hata kitimoto), kunywa chochote(pombe), hapa Zanzibar watalii wanapita kwa siku zisizozidi tatu (kushangaa mchanga mweupe wa beach ambao umegundulika umejaa vilivyo kule Tanganyika (Kigamboni), kutafuna machoko wakizenji na kubwia unga kwa uhuru kisha kusepa zao). Bahati mbaya sana na huo utalii pekee hautoshi kuendesha maisha ya wazanzibar zaidi ya 1.5milioni kwa siku zaidi ya 90.
Yote kwa yote, mmasai ameshaingia Zanzibar na sasa anataka kutawala utaliii wote.
Nasema hivi, Zanzibar bila Tanganyika twafaa!
Mtanganyika anatujali mnooo.