Ukweli mchungu: Zanzibar tunaishi kwa kudra za Tanganyika!

Kwamba tukikopa nje tunawapa 4% ya pesa za mikopo anadai sio sawa,
Hayo ya Zitto ni porojo..

Halafu inapokuja suala la kulipa mikopo Tanganyika pekee ndo hulipa. Fikiria itakuwaje kama Znz wakitakiwa walipe mikopo yote waliyowahi kupokea kupitia Tanganyika, si visiwa vitapigwa mnada?!

Kumbuka pia kuna mikopo huwa inakopwa na Tanganyika kwa ajili ya Znz tuu, ingawa hata hii mlipaji ni Tanganyika pekee
 
Dubai ni Dubai tu na ZNZ itabakia ZNZ. Kwanza ZNZ ikitolewa kwenye Muungano tambua kuwa nayo itakufa na kuzaa Pemba na Unguja.

Ni rahisi kuwa na Muungano wa Tanzania na ZNZ kuliko muungano wa Pemba na Unguja. Tofauti za kihistoria za hivi visiwa viwili inamezwa na Muungano. Watagawana mbao halafu baada ya hapo tutaanza kubeba mzigo wa UNHCR kama inavyotokea Kigoma na ngara kwa kambi za wahutu na watusi kutoka Burundi/ Rwanda
 
Wazanzibari wanaojielewa hawataki huu muungano uvunjike, wachache wasiojitambua wanalia na kulalama kwa kusema wanaminywa, ukiwauliza wanaminywa wapi hawajui na hawasemi...

Mfano leo hii muungano ufe

1. Hawana jeshi imara la ulinzi na usalama, sababu 80% jeshi hili kiutawala limebase bara kuliko visiwani... Hapa watahangaika sana, na ndio utakuwa mwanya kwa wasiotaka amani huko kuleta vurugu

2. Hawana uchumi imara wa kusema wanaweza kujitegemea na mambo yakaenda, watalazimika kuingiza wahisani wengi visiwani + madeni + kugawa visiwa kwa kisingizio cha uwekezaji, matokeo yake kuwa na madeni mazito kisha kuwa taifa tegemezi kwa kiasi kikubwa

3. Hawana ardhi ya kilimo cha kutosheleza, chakula kwa kiasi kikubwa kinatoka nje ya Zanzibar, vinaingia kutoka bara na nchi nyingine, so vyovyote vile ndani ya muda mchache kutatokea mfumuko wa bei na kusababisha hali ngumu ya maisha

4. kunawezekana kukawepo kundi la watu/wafanya biashara/viongozi linasubiri wazanzibari wajichanganye wafuate mihemko ya kuvunja muungano kisha kuwe na kukomoana, cha huku ni cha huku na cha huko ni cha huko...

Watu watafakari kabla ya kutaka kuvunja Muungano wasije kuja kujuta hapo baadae... Hasa wazanzibari mjitafakari sana
 
"kutafuna machoko wakizenji na kubwia unga kwa uhuru kisha kusepa zao"

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]aisee wakikukamata[emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1787]
 
Kumtegemea binadamu ni dhambi
Mimi naamini mtaishi na mnaweza kuwa mbali sana kwa kujitegemea wenyewe
Hata huku tunaishi kwa kudra za Mungu tu kupitia kwa wazungu na misaada yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…