Uchaguzi 2020 Ukweli mchungu: Zipo kura za WanaCCM wa JF kwa Lissu, hazipo kura za wanaCHADEMA wa JF kwa Rais Magufuli. Ushindi unaanzia hapa!

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Rais Magufuli umelikoroga sasa na ulinywe tuu maana hakuna namna.

Ukitumia ubabe kwa watanzania watakupiga kwenye sanduku la kura, sisi tunasema usitumie ubabe. Tukakusihi kutoka mwaka 2016 kwamba ubabe hausaidii, tukawambia usifanye hivyo ukakaidi, sasa utapigwa! Tulikuonya usiende na njia hiyo, ukaona sisi ni vibeberu uchwara, utapigwa! Na mimi nasema wakupige tu kwenye sanduku la kura maana hakuna namna sasa! Enh, ubabe ukiutumia kwenye uongozi utapigwa kwenye kura! Na acha upigwe tu!

Kiukweli njia ya uongozi na mwenendo alioenda nao Rais Magufuli kwa hii miaka mitano ni ya hovyo sana na akirudi kwa wananchi ataona matokeo yake. Mimi binafsi nimejikuta nikifurahia matokeo yake ingawa mwanzoni nilipaaza sauti abadilike. Namshukuru Mungu kwa kuendelea kumjengea ubabe. Sasa anaenda kuvuna!

Sina shaka na kina johnthebaptist aka bwasheeee, Pascal Mayalla na wengine wengi ambao ni wanaccm ILA kura zao hazitaenda kwa Magufuli. Hiyo ni hatua nzuri ya ushindi na bado huko mitaani.

Tukirudi kwa wanachadema sijaona na haitokaa itokee kura ya mwanachadema yeyote kwenda kwa Magufuli!

Upo uongozi wa kimsimamo unaozingatia sheria na ubabe uchwara, watanzania hawako tayari kuchagua "Ubabe uchwara, wamepitia mengi!
 
Inawezekana pale wanaccm kupitia mwenyekiti wa NEC kuhakiki kweli kashindwa na akatangaza matokea halisi.

Vinginevyo katika hali hii hii ya kuteua ndg, jamaa na marafiki wakurugenzi na wengine kwenye tume sidhani kama tutafua dafu, nao wanajua akishindwa wanafia ndani.
 
Tukirudi kwa wanachadema sijaona na haitokaa itokee kura ya mwanachadema yeyote kwenda kwa Magufuli!
Mwenye akili hawezi kumpa Magufuli kura. Atapewa na wale wanaofaidi utawala wake, pamoja na hayo MWENYE AKILI hata kama anafaidi utawala wake atamnyima kura! MAANA CONSCIOUS YAKE INAMWAMBIA KUWA HIKI UNACHOKIFANYA SIYO SAWA
 
Umesema ukweli mtupu, ila je, kwa hii tume ya uchaguzi unategemea nini? Labda itokee miujiza ya M/Mungu ndipo chama pinzani chaweza kukabiziwa nchi!
 
Ni hesabu rahisi sana kutegemea JF kuingia ikulu! Ni kweli ni chombo cha habari ila sioni members wa kuweza kumuingiza Rais ikulu hapa! Subscriber wake bado ni wachache sana!

Wajikite zaidi kuwafikia wananchi na jamii ya chini hawa ndo wapiga kura!
 
Mmmmh.....πŸ€”
Nakubali kutokukubaliana........
Vile naona spana imewabana wasiobanika......
Tutaelewana tu.......Magufuli 5 tena......
Walio na wananchi kwa upendo wala hawajapigwa spana na hilo ni onyo kwa Magufuli.
 
Huku mtazipata nyingi maana si ndo kichaga chenu Cha kutoa matusi tu baada ya kula bangi na kulewa konyagi.

JPM anakubalika Sana believe or not. Ila si vibaya kujifurahisha na kutoa stress za hapa na pale kwa kuamini usiku kua mchana kisa una kibatari kinachokupa mwanga wa kuona tumbo lako
 
Ilikuwa ndoto yakwo.. πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
Rudi kulala ukaote tena.. kabla hujapasuka kichwa.. umehama wewe kwenda huko humu JF. Sijui umeiba nini ukatumbuliwa.. 😁 utajijwu..

Magufuli 2020
 
Ni hesabu rahisi sana kutegemea JF kuingia ikulu! Ni kweli ni chombo cha habari ila sioni members wa kuweza kumuingiza Rais ikulu hapa! Subscriber wake bado ni wachache sana!

Wajikite zaidi kuwafikia wananchi na jamii ya chini hawa ndo wapiga kura!
Wananchi ndiyo walilipia matibabu ya Lissu seuse kumpa kura
 
Nitawashangaa sana watumishi wa umma ambao watampigia kura Magufuli wakati watumishi wa umma ndio kundi pekee lililo ongoza kwa kunyanyaswa na kupuuzwa na utawala wa awamu ya 5,kwa muda wa miaka 5 watumishi wa umma wamehesabiwa kama ndio mashetani wa serekali ya Magufuli.

Na nitawashangaa sana wakulima watakaompa Magufuli kura zao,wakati serekali ya Magufuli haijawahi kuwahesabu kuwa nao ni wananchi ambao wana haki ya kufaidi matunda ya serekali yao kwa kuuziwa pembejeo za kilimo kwa bei nafuu na kuuza mazao yao kwa bei ya juu.
 
Naona unaweweseka sasa! Jitahidi kumtafutia kura msaliti wa nchi yetu
 
Hahahaaaa........ Lisu atatuuza kwa mabeberu.

Dr Magufuli ni Lulu na yule Lisu ni sawa na gololi za kuchezea watoto!
 

Leo umemwamukia haswa huyo JPM- Labda atastuka maana juzi kati nimesikia mjeda anasema wao hawana chama , sijui alikuwa anampelekea ujumbe gani...
 
Leo umemwamukia haswa huyo JPM- Labda atastuka maana juzi kati nimesikia mjeda anasema wao hawana chama , sijui alikuwa anampelekea ujumbe gani...
Ndoto za Alinacha hizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…