Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 2,158
- 5,626
UKWELI MDOGO KUHUDU KASONGO.....
Muite Ngiri(Phacochoerus africanus) au
Warthog(tamka Wart-hog) au muite Pumba.
Wenyewe mmeamua kumuita Kasongo(si jina Rasmi)
Ni Mnyama anayepatikana kwenye Familia inayoitwa Suidae ambayo miongoni mwao Wamo Nguruwe Pori(Hogs na Pigs) na Nguruwe wa Kufugwa.
Sifa zao kuu.....
-Wana kwato zilizogawanyika kwa mbili(Artiodactyls) lakini hawacheuwi(Non Ruminant)
-Wanazaa Watoto zaidi ya Mmoja au Mapacha(mulitiparous) na ni wao pekee wenye uwezo huu miongoni mwa wanyama wenye kwako...wawe wanacheuwa(Ruminants) au hawacheuwi.
...............................................................................................
×Pumba aka Kasongo anafanya shughuli zake Mchana(Diurnal) na usiku hulala.
×Makazi yake ni kwenye Mashimo(Fossorial) ambayo hachimbi mwenyewe bali huchimbwa na Muhanga wakati akijitafutia kitoweo ambacho ni Wadudu hasa Mchwa.
Pumba anakula Nyasi na Mizizi yake na ndio maana mara nyingi huonekana anakula huku amepiga magoti.Hii humsaidia kuchimba vizuri mizizi ya Nyasi kwa kutumia Pua yake.
Kumbuka taya la juu ni refu kuliko la chini na ana shingo fupi.Asipopiga Magoti zoezi la kukata nyasi na kuchimba mizizi lingekuwa gumu zaidi.
Tofauti na Sifa nyingi za Bandia anazopewa,Ngiri ni Mnyama anayekimbia Km 55 tu kwa saa lakini sifa yake nyingine ni kusahau mapema sana pale anapokimbizwa na adui na akafanikiwa kumzidi Mbinu na Maarifa.
Pia wakati anaingia kwenye Shimo lake la kulala huwa anageuka Kinyumenyume ili kesho asubuhi asipate tabu ya kuwaza anatokaje.Yaani pakikucha anachomoka Nduki Kali kwa hiyo kama kuna adui anamsubiri Mlangoni ataishia kuona Vumbi.
Sambamba na hilo anaingia Kinyumenyume ili hata ikitokea adui akataka kujaribu kuingia kwenye Shimo lake atakutana na Silaha nzito ambazo ni Meno yake makali na Marefu.
Kumbuka.....Ngiri/Pumba harushi mateke wala hawezi kujilinda kwa namna yoyote kutokea Nyuma.Ulinzi wake uko kwenye Meno pekee.Hata Pembe kanyimwa.
Analosahau ni hili......
Wakati akiwa ametoka asubuhi kwenda kuhemea ana uhakika gani kwamba adui hajatangulia kwenye Shimo lake ili anapoingia Kinyumenyume aanzwe Makalio?
Hapo tunaiachia Asili yenyewe ndio inajua kwa nini haimpi huo ufahamu wa kukagua kwanza Makazi yake!
Ukimtazama Pumba huyu pichani utaona kuna Meno yametokezea ambayo ndio silaha yake ya pekee lakini Chini ya Macho kidogo kuna hayo Manundu marefu.
Hayo yanamuongezea sura ya kutisha zaidi hivyo Adui anaweza kuona si Meno tu bali ana silaha nyingine kama Pembe hivi kumbe hizo ni Zuga tu hazitumiki kwenye Mapambano.
Kazi zake nyingine nawaachia kina BRAZA CHOGO ,braza bonge UMUGHAKA na wenzake wanaoshinda na kukesha chaka watusaidie huwa wanaona zinatumika Vipi.
Asanteni!