Ukweli Mgumu Kuhusu Maisha Niliogundua - Nimeamua Kuwa Mkweli Nanyi

Joined
Jul 30, 2024
Posts
5
Reaction score
28
Wadau,

Nimekaa chini nikafikiria sana kuhusu jinsi dunia ilivyo, na nikaona niwaambie ukweli mgumu. Kama ukweli usiofurahisha unakukwaza haraka na hupendi kusikiliza, basi pita tu. Huu ujumbe si kwa ajili yako.

Ukweli ni huu:

Dunia ni katili.

Utakataliwa. Utapoteza watu uliowapenda. Utafanya kazi kwa bidii sana kwa kitu na bado hutakipata. Utalia. Kutakuwa na kipindi maishani mwako utahisi kila kitu kinaanguka, na wakati mwingine kitaanguka kweli.

Lakini kujifanya maisha ni mepesi kuliko yalivyo, hakutakuandaa kuikabili.

Kwa hiyo kuna vitu 3 nimejifunza na naamini kila mtu anatakiwa kuvielewa:

1. MITANDAO YA KIJAMII SI KIPIMO CHA MAISHA YAKO

Tumekosea sana. Tumeifanya mitandao kuwa kipimo cha maisha.

Unaona mtu mzuri zaidi yako, unajiona wewe ni mbaya. Unaona mtu tajiri zaidi yako, unajiona umechelewa maishani. Unaona watu wanapost mapenzi yao, unaanza kuhisi mahusiano yako hayafai.

Lakini unafanya kosa kubwa. Unalinganisha maisha yako yote halisi ambayo hayajahaririwa, na video ya sekunde 15 ambayo mtu kachagua kukuonyesha wewe.

Vingi vya vitu mtandaoni vimetengenezwa makusudi kukushikilia u-scroll tu, kukuuzia kitu, kukufanya uhisi hisia ili ubaki humo.

Mimi nasema jiburudishe, mimi pia nafanya hivyo. Lakini chunguza sana kile unachoingiza akilini mwako. Ukikitazama kitu kwa muda mrefu na kukiamiini, kitaanza kuwa ndio kawaida yako, wakati sio kawaida.

Mimi mwenyewe napambana na hili pia. Ndio maana nawaambia jaribuni kitu kimoja: Wekeni simu chini kwa siku moja tu. Sio kwa sababu simu ni mbaya, ila nataka ujithibitishie mwenyewe kuwa bado wewe ndiye unaeamua nini kiingie akilini mwako, sio simu.

Kama ukiamka asubuhi na huwezi kumaliza siku nzima bila kuingia TikTok au IG, basi wewe na mimi tuna tatizo.

2. UNATAKIWA KUWA MTU WA THAMANI

Sisemi thamani yako kama binadamu, hiyo tayari unayo. Nasema thamani ya kivitendo.

Dunia inafanya kazi hivi: Unaweza kufanya nini? Unajua nini? Unawachukuliaje watu? Watu wanaweza kukutegemea? Unaweza kuwasiliana? Kuunda kitu? Kutatua tatizo? Unawajua nani?

Dunia haikudai mahusiano unayotaka. Haikudai pesa unayotaka. Haikudai mwili au kazi unayotaka, kwa sababu tu umeitaka sana. Inasikika kama ukatili, lakini ukweli huu ndio unaokupa uhuru.

Badala ya kulalamika, jiulize: Niko wapi sasa na nini naweza kufanya kuboresha?

Hupendi muonekano wako? Fanya kitu. Nenda gym, tengeneza ngozi yako, vaa vizuri. Ndio, rekebisha unachoweza kurekebisha, lakini pia fanyia kazi moyo wako unaodhani sura yako ndio thamani yako yote.

Huna pesa? Sawa, lia. Niko serious, lia kwanza. Inaumiza. Halafu baada ya kulia, tafuta ni ujuzi gani unaweza kujifunza, ni kitu gani ulicho nacho unaweza kuuza kwa dunia.

Maisha sio sawa. Wengine wameanzia maili 10 mbele yako. Wengine wamezaliwa na utajiri. Unaruhusiwa kusema sio haki, lakini bado lazima uamue utafanya nini baada ya hapo. Ukijiambia kila siku kwa nini huwezi kusonga, hiyo sababu ndiyo itakayokuzuia kusonga kweli.

3. KUWA MTU MPOLE BILA KUWA DHAIFU

Hii ndio muhimu zaidi.

Una haraka kiasi gani kumsamehe mtu akimkosea? Ego yako inataka kushinda kila mabishano? Ukikosea, unajifunza au unajichapa mwenyewe?

Wewe ulivyo leo ni muhimu sana. Lakini unayechagua kuwa kila siku ni muhimu zaidi.

Mimi naamini kwa Mungu, na naamini maisha haya ni ya muda mfupi tu. Siku moja pesa itabaki, nguo zitabaki, sifa itabaki, lakini wewe hutabaki.

Kwa hiyo jenga maisha mazuri, jitunze, tafuta pesa, kuwa na uwezo, kuwa na manufaa. Dunia ya nje ina umuhimu. Lakini usijisahau wewe ni nani wakati unapambana kuitafuta dunia.

Kuwa mgumu kudanganywa. Kuwa makini na kile kinachoingia akilini mwako. Kuwa na uwezo. Kuwa na manufaa. Kuwa na upendo. Samehe haraka. Kubali ulipokosea.

Na maisha yatakapokukataa - na yatakukataa tu - kuwa na uwendawazimu wa kusema: "Hii inauma. Sawa. Lakini nitafanya nini kuhusu hili?

Dunia itakuambia kila siku nini uthamini, uwe nani, utumie wapi pesa yako, uwe mtu wa aina gani. Kazi yako ni kuelewa dunia inavyofanya kazi bila kuiruhusu dunia ikuamulie wewe uwe nani.

Nimeandika haya kutoka moyoni. Mnaonaje wadau?
 
Yote ni ubatili. Fanya kikupacho furaha. Usiumize wengine. Saidia unapoweza...na muda wako ukifika nenda! Nobody cares 🚮🚮🚮

IMG-20261001-WA0032.jpg
 
Inspiration speakers
 
soma kitabu cha muhubiri. anywah
 
Siku ukiacha kutafuta kujithibitisha ndipo utaona uzuri wa dunia na urahisi wa maisha
 
Back
Top Bottom