Hmaster
JF-Expert Member
- Dec 27, 2010
- 346
- 86
Juzi nilikuwa maeneo ya Ubungo ambapo nilikutana na dada furani akiwa na watoto wa2 na mizigo kadhaa na baada ya kusalimiana aliniomba nauli ya daladala ili aende Tegeta kwa dada yake kwani alikuwa ameibiwa pochi yake ambayo ilikuwa na pesa akiwa safarini kutokea Songea. Mimi kwa vile nilikuwa na gari na kwa namna alivyoonyesha huzuni niliona bora nimchukue tu kwenye gari yangu hadi Tegeta kisha nikarudi hadi Magomeni ninapoishi. Kwa sababu ya foleni nyingi na muda ulipita sana kabla ya kurudi home, hata hivyo my wife wangu nilimweleza kila kitu lakini badala ya kuona umuhimu wa mimi kumsaidia mwanamke mwenzake yeye alikwenda mbali zaidi na aliamua kukata simu na hakupatikana hadi nafika home. Baada ya kufika nikamkuta tayari yupo kitandani akiwa na nguo zake zote, eti ndo keshakasirika na kuamua kulala hiyo saa tatu na wakati huwa tunalala hata saa 5 kila siku. Nilipojaribu kumwamsha ili aniandalie chakula alinijibu niende kula kwa malaya niliyemsindikiza Tegeta. Nilijitahidi kumwelewesha lakini ilishindikana. Nikajiandalia chakula mwenyewe, nikaoga na kisha kulala kwa maana kwa hali hiyo hata kumchombeza sikuweza. Sasa swali ni je Ukweli na Uwongo upi hudumisha ndoa, au vyote? Wenye experince na mambo haya waweke hapa maana sasa najiandaa kuwa mwongo kwa vile ukweli umenitokea puani. Na kama wanawake humu jf watueleze wenyewe kipi wanataka kutoka kwetu kati ya hivyo vitatu ili wawe na amani. Nawasilisha!