Ukweli na Uwongo upi hudumisha ndoa? Au vyote?



Hiyo bibilia haikusema udanganye pia, sasa ya kusema mwanamke ni kiumbe dhaifu na anastaili adanganywe ni mpya kwangu. Bora useme ukweli, mugombane anune lakini mwisho yataisha, atajua kuwa mumewe ni mkweli ila yeye tu anahofia.
Labda mwanamke hasie kuwa na akili timamu ndio anapenda kudanganywa.

Na vizuri kasema ukweli, je kama angeonekana na watu wanao mfaham hapo Ubungo anaingiza mwanamke na watoto ndani ya gari lake, na habari zikafika kwa mkewe siku ingine, nazani moto ungelipuka na angeshindwa kuzima, pengine na talaka angedai. Nyie wanaume wengine hamfikiri mbali.............
 
Ukweli mwingi na uongo kidogo
 
Ukweli utabaki kuwa ukweli tu. Uongo sio mzuri. Huyo ananuna nuna hujambembeleza siku nyingi.
 
Ukweli utabaki kuwa ukweli tu. Uongo sio mzuri. Huyo ananuna nuna hujambembeleza siku nyingi.
Given the Choice...,
Ukweli alafu nikupoteze au nikufanye usikitike na kuumia wewe kipenzi changu au
Uongo ingawa utaniumiza mimi lakini nipo tayari kubeba mzigo huo na kukufanya uendelee kufurahia..... Utachagua nini

au mfano;
Rafiki yako kipenzi baada ya kuwa amelewa alinitaka Je nikwambie huku nikijua fika kwamba nitavunja urafiki wenu wa muda mrefu na ni kwamba sababu ya pombe ndio alifanya hayo.....? Je itakuwa Busara kwa mimi kuvunja urafiki wenu, na kukufanya wewe usikitike na kuumia Just for the sake ya kusema Ukweli???, au kama wazazi wangu hawakutaki Je nikwambia huku nikijua kwamba hiyo itajenga ufa kwenye familia??
 
bora uniambie ukweli wewe mwenyewe kuliko nije nigundue mwenyewe. Nikigundua ulinidanganya nitaumia zaidi. Kwa mfano uliotoa wazazi wako hawanitaki halafu unanificha, utanificha hadi lini? Sema ukweli ili nijue tunakabiliana vipi na hiyo hali kuliko kunyamaza mwisho wa siku impacts zake zitakuwa ni kubwa zaidi. Ukweli siku zote unamuweka mtu huru. Hebu fikiria huyu mtoa mada angemdanganya mkewe halafu ikatokea akapata matatizo huko alikompeleka mdada, ni vipi angejieleza kwa mkewe kwamba hakuwa na intentions zozote mbaya! I do speak the truth bila kujali utamuumiza mtu.
 
Si ukweli wala uongo kinachoweza kudumisha ndoa, ni mchanganyiko. Hata maandiko yanatuhasa tuwe wa kiasi. Sometimes huwa namdanganya wife, sometimes namwambia ukweli - bora kudumisha amani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…