Somoe
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 754
- 282
Kaka pole sana, sio kila siku lazima useme ukweli hata uongo unasaidia sana kujenga ndoa, kwa hili suala lako ungemdanaganya tu mama asikngekuwa vile ulivyomkuta kwa mfano ungesema nilikutana na rafiki yangu (wa kiume) pale Ubungo akaniomba nimpeleke Tegeta hivyo nimechelewa kurudi kwa sababu ya msongamano wa magari, hapo ungekuwa salama kwamba ni kweli Tegeta umeenda, hata kama kuna mtu aliona gari lako angeshuhudia hivyo hivyo ungebaki salama.
Unapoishi na mkeo jaribu kuishi kwa akili kwa sababu unaishi na kiumbe dhaifu (sio maneno yangu jamani, ni biblia imesema, akina dada msinishambulie tafadhali).
Hiyo bibilia haikusema udanganye pia, sasa ya kusema mwanamke ni kiumbe dhaifu na anastaili adanganywe ni mpya kwangu. Bora useme ukweli, mugombane anune lakini mwisho yataisha, atajua kuwa mumewe ni mkweli ila yeye tu anahofia.
Labda mwanamke hasie kuwa na akili timamu ndio anapenda kudanganywa.
Na vizuri kasema ukweli, je kama angeonekana na watu wanao mfaham hapo Ubungo anaingiza mwanamke na watoto ndani ya gari lake, na habari zikafika kwa mkewe siku ingine, nazani moto ungelipuka na angeshindwa kuzima, pengine na talaka angedai. Nyie wanaume wengine hamfikiri mbali.............