Ukweli ni kitu gani?

Ukweli ni kitu gani?

Ukweli ni Mungu mwenyewe. Sababu neno la kweli linadumu milele na Uongo ni shetani na shetani hatoweza kudumu milele

Sent from my SM-J530F using Tapatalk
 
Yesu alipoulizwa ukweli ni nini alijibu nini ? Na hilo jibu ni ukweli kwa wakristu , sasa waislam ukweli wao ni upi ? Labda ujumlishe ukweli wa dini zote ugawe kwa idadi yake ! Labda ukifa utaona ukweli !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukweli ni mantiki inayokubalika na wengi.
Binadamu hawezi kuujua ukweli. Binadamu huishi kwa theories(nadharia) na principles(kanuni). Ukweli upo tu kwenye falsafa. Falsafa ya ukweli itakupeleka kwenye mamlaka ya mwisho ambayo ni Mungu. Hakuna binadamu anayeweza kuwa na hakika ya asilimia mia moja kuwa anasimamia ukweli. Ila binadamu anapojiweka chini ya mamlaka, ataishi kwa kufuata nadharia na kanuni za ile mamlaka, nayo kwake ndiyo itakuwa kweli. Hii inapelekea hitimisho kuwa hakuna universal truth kwa binadamu. Universal truth exists only under authority external to human beings.
 
Kitu kinachokaribia ukweli kinapatikana kwenye hesabu 2+2=4 duniani kote jibu lake linafamika . Kuna mwanafalsafa alinena "the truth is found in numbers "

Sent from my TECNO-N2 using JamiiForums mobile app
 
Ukweli ni kule mtu kujiaminisha kua asemalo au analo liamini kuwa ni Ukweli na akawa na uwezo wa kutetea analolisema au kuliamini kwa hoja madhubuti zitakazo weza waaminisha wanaomfuata au kumsikiza kuwa asemayo ni kweli tupu.

Sent from my OPPO A57 using JamiiForums mobile app
 
Watu wanajaribu kusema ukweli sio imani na ukweli ni ukweli..kwamba imani nyingi ni uongo yani si kweli.
Lakini ukweli ni kwamba ukweli wenyewe ni IMANI tu kwa maana ya kuwa watu watakachoamini ndiyo huwa kweli kwao..mfano zamani watu waliamini jua linazunguka dunia na ilikuwa kweli yao lakini leo tunaamini tofauti...Sayansi hubadilika zamani waliamini Atom is the smallest unit of matter lakini wakagundua smaller particles kama electrons na protons..so unaweza shangaa miaka 1000 ijayo watu wakaamini Jua halipo kabisa...haya maisha ni game tunachezwa na Aliens wanaojiita malaika.

Sasa haijalishi jua lipo au la! Maisha haya ni halisi au La!Jua linazunguka dunia au La!Atom ndiyo ndogo zaidi au la! lakini watakachoamini watu ndo itakuwa kweli yao....na huo ndo ukweli
 
Habari wana JF

Wakati tunaelekea mwisho wa mwaka kwenye msimu wa sikukuu nimejaribu kutafakari peke yangu hili jambo tajwa hapo juu (ukweli ni kitu gani?) bila mafanikio. Msingi wa tafakari yangu unatokana na maandiko matakatifu (biblia agano jipya) ambapo Yesu aliulizwa na Pilato je ukweli ni kitu gani? Bahati mbaya muandishi hakueleza kama Yesu alijibu na jibu lake lilikua ni lipi? (kwa wale wenye uelewa zaidi ya huu watanijuza pia).

Kwa kutumia uwezo wangu nimejaribu kujiuliza hili swala muda mrefu sana nisipate jibu lake. Mara nyingine utaona watu wanabishana na kila mmoja ana amini anachosema ni cha ukweli, sasa hapo shida ndipo inapoanza ukweli ni upi sasa?

Tafsiri ya kwanza inaweza ikawa, ukweli unaweza ukawa ni maneno au jambo analolisema mtu amabalo analoliamini na yuko tayari kulishuhudia lakini linaweza likawa sahihi au siyo sahihi. Ni nini basi kinachoamua usahiii wa jambo? mara nyingi ni imani (dini au mila), mapokeo, maono (jinsi lilivyoonwa) na mazoea. Hali kadhalika imani, mapokeo, maono na mazoea yanaweza yakawa na tafsiri tofauti kati ya waumini wa imani moja na nyingine, au jamii moja na nyingine au mtazamaji mmoja na mwingine.

Kwa maana hiyo basi jambo moja linaweza likawa na tafsiri zaidi ya moja kulingana na imani, maono, mapokeo na mazoea. Kwa mustakabali huo basi, ukweli ni kitu gani? je kuna ukweli mmoja (universal truth) au kuna various versions of truths? Naomba kujuzwa.
Bwana YESU hakumjibu pilato kwa sababu moja tuu ni sawa na ww unamjua raisi wa nchi afu siku unaonana nae sehemu ana kwa ana unaanza kumuuliza huyo raisi kuwa raisi n nani ndivo ilivotokea kwa pilato kuuliza kweli ni nini wakati ukwel n kuwa KWELI alikuwa amesimama mbele yake katika mahubiri yake alisema waziwazi YEYE NDIYE NJIA, KWELI NA UZIMA
 
Ukweli ni jambo sahihi ambalo mtu anaweza kulithibisha kwa kutumia milango zita ya faham ya binadam
Tatizo linakuja katika ukomo na madhaifu y milango hiyo hapo ndio unaanza kukuta mambo tata huzuka
Lakin pia kuna vitu huvunja zile prinsples zinaazoongoza dunia hapa ndio utaona ukweli unaweza kuwa uwomgo muda wowote na uwongo kuwa ukweli
 
Habari wana JF

Wakati tunaelekea mwisho wa mwaka kwenye msimu wa sikukuu nimejaribu kutafakari peke yangu hili jambo tajwa hapo juu (ukweli ni kitu gani?) bila mafanikio. Msingi wa tafakari yangu unatokana na maandiko matakatifu (biblia agano jipya) ambapo Yesu aliulizwa na Pilato je ukweli ni kitu gani? Bahati mbaya muandishi hakueleza kama Yesu alijibu na jibu lake lilikua ni lipi? (kwa wale wenye uelewa zaidi ya huu watanijuza pia).

Kwa kutumia uwezo wangu nimejaribu kujiuliza hili swala muda mrefu sana nisipate jibu lake. Mara nyingine utaona watu wanabishana na kila mmoja ana amini anachosema ni cha ukweli, sasa hapo shida ndipo inapoanza ukweli ni upi sasa?

Tafsiri ya kwanza inaweza ikawa, ukweli unaweza ukawa ni maneno au jambo analolisema mtu amabalo analoliamini na yuko tayari kulishuhudia lakini linaweza likawa sahihi au siyo sahihi. Ni nini basi kinachoamua usahiii wa jambo? mara nyingi ni imani (dini au mila), mapokeo, maono (jinsi lilivyoonwa) na mazoea. Hali kadhalika imani, mapokeo, maono na mazoea yanaweza yakawa na tafsiri tofauti kati ya waumini wa imani moja na nyingine, au jamii moja na nyingine au mtazamaji mmoja na mwingine.

Kwa maana hiyo basi jambo moja linaweza likawa na tafsiri zaidi ya moja kulingana na imani, maono, mapokeo na mazoea. Kwa mustakabali huo basi, ukweli ni kitu gani? je kuna ukweli mmoja (universal truth) au kuna various versions of truths? Naomba kujuzwa.
Ukweli ni kile ambacho kimetendeka au hakikutendeka ambacho kinyume chake ni uongo. Uongo ni kile ambacho hakikutendekea au kile ambacho kimetendeka. Ukweli ni kinyume cha uongo
 
Hata unachokiona sio kweli, unaona tu photocopy ya kitu halisi, ukweli ni nini? Labda Plato wa kale alichosema "the word of ideas" hasa katika msemo wake "allegory of the cave".
 
Habari wana JF

Wakati tunaelekea mwisho wa mwaka kwenye msimu wa sikukuu nimejaribu kutafakari peke yangu hili jambo tajwa hapo juu (ukweli ni kitu gani?) bila mafanikio. Msingi wa tafakari yangu unatokana na maandiko matakatifu (biblia agano jipya) ambapo Yesu aliulizwa na Pilato je ukweli ni kitu gani? Bahati mbaya muandishi hakueleza kama Yesu alijibu na jibu lake lilikua ni lipi? (kwa wale wenye uelewa zaidi ya huu watanijuza pia).

Kwa kutumia uwezo wangu nimejaribu kujiuliza hili swala muda mrefu sana nisipate jibu lake. Mara nyingine utaona watu wanabishana na kila mmoja ana amini anachosema ni cha ukweli, sasa hapo shida ndipo inapoanza ukweli ni upi sasa?

Tafsiri ya kwanza inaweza ikawa, ukweli unaweza ukawa ni maneno au jambo analolisema mtu amabalo analoliamini na yuko tayari kulishuhudia lakini linaweza likawa sahihi au siyo sahihi. Ni nini basi kinachoamua usahiii wa jambo? mara nyingi ni imani (dini au mila), mapokeo, maono (jinsi lilivyoonwa) na mazoea. Hali kadhalika imani, mapokeo, maono na mazoea yanaweza yakawa na tafsiri tofauti kati ya waumini wa imani moja na nyingine, au jamii moja na nyingine au mtazamaji mmoja na mwingine.

Kwa maana hiyo basi jambo moja linaweza likawa na tafsiri zaidi ya moja kulingana na imani, maono, mapokeo na mazoea. Kwa mustakabali huo basi, ukweli ni kitu gani? je kuna ukweli mmoja (universal truth) au kuna various versions of truths? YOUR TRUTH, MY TRUTH AND THE TRUTH, Naomba kuju

Subjective and objective truth

Kwa maana hiyo basi jambo moja linaweza likawa na tafsiri zaidi ya moja kulingana na imani, maono, mapokeo na mazoea. Kwa mustakabali huo basi, ukweli ni kitu gani? je kuna ukweli mmoja (universal truth) au kuna various versions of truths? YOUR TRUTH, MY TRUTH AND THE TRUTH, Naomba kujuzwa.
Kuna kweli za aina mbili...ukweli unaoujua wewe pengine kutokana na vyanzo ulivyovitaja hapo juu na ukweli unaotokana na uhalisia wa jambo husika.
 
Your version of the truth, my version of the truth and the truth
 
Back
Top Bottom