lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,571
- 35,475
Mgogoro huu kati ya Ukraine na Urusi unaongoza kwa propaganda kuliko mgogoro wowote ule toka vita kuu ya pili ya Dunia.
Ukisikiliza propaganda za nchi za west unaweza kudhani Urusi imechukiwa na Dunia nzima.
Lakini ukweli sio hivyo.
Hali halisi Iko hivi.
Nchi zinazoichukia ama kuonesha kuitenga Urusi ni nchi zote za west.
Hata hizo za west baadhi ni kama zinalazimishwa TU kuitenga Urusi ili kuonesha umoja wao.
Wenye chuki wakubwa wa Urusi ni USA na UK.hawa wanawalazimisha west wengine waichukie Urusi kwa sababu zao za kihistoria.
Ukichunguza kwa undani nchi kadhaa za west zinaona kweli Urusi kachokozwa lakini haziwezi kusema hadharani kwani zitaonekana wasaliti wa NATO.
Na hata kujiunga na NATO ni kama zinashawishiwa na USA mwenye malengo binafsi.zipo nchi za West wala hazina hofu na Russia.
Mfano mdogo TU ni German,German siku zote anaiona Russia kama partner wake kibiashara.na ndio maana ikaingia mkataba mkubwa sana ulaya wa Bomba la gesi Nord stream3.
Na nchi nyingi nyinginezo za west.
Tuje Africa.
Karibu Africa nzima wala hawachukizwi na Urusi katika mgogoro huu.
Njoo Middle east,tukiamza na mshirika mkubwa wa USA Israel,huyu wala hajailaan Urusi,
Nchi nyingine ambazo hazijachukizwa na Urusi ni Iraq,Iran,Said Arabia,Yemen,Lebanon,Syria,na nchi nyingine kadhaa.
Njoo Far East na Asia.
Nchi karibu zote hazijakerwa na Urusi isipokua Japan,Korea kisini na vi nchi vichache.
America ya kisini.
Hizi nchi nyingi wala hazina tatizo na Urusi,zaidi Zina tatizo na USA hivyo hazina
Lakini wakubwa wa Asia kama China,India na vinchi vingine wala havina time na alichokifanya Urusi.
Kwa Nini nimeyasema haya.
USA anapiga propaganda kuwa Urusi imetengwa na Dunia nzima,lakini ukweli ni kwamba nchi zimekua zikilazimishwa kulaani ama kuweka ikwazo dhidi ya Urusi.
Kulaani ni kitu kinachotokea moyoni mtu akikulazimisha umlaani Adui Yako Haina nguvu kama ukimlaqni kwa hisia zako wewe mwenyewe.
USA imetishia hata kuziwekea vikwazo nchi zitakazoendelea kufanya biashara na Urusi. Sasa ugomvi wa USA na Urusi utawalazimaishaje wengine wamtenge Adui Yako? Wakati wao wanamuona mshirika wao wa masuala mengine?
Njoo nchi zilizokua soviet ya zamani.
Nchi nyingi zinazomchukia Urusi ni zile zilizo upande wa Magharibi wa Urusi,lakini nyingi zilizo upande wa Mashariki mwa Urusi kama kyugistan,Tajikistan,Uzebakistan na baadhi Yao hawana wala habari na Urusi. Kwa kufupisha ukiangalia majumuisho ya nchi zote za duniani utaona ni Chache sana zimekerwa na Urusi.
Kwa kifupi nchi nyingi sana hapa duniani zinaona mambo anayoyatenda USA kwa mataifa mengine kivita lakini hakuna hata nchi moja iliyomwekea vikwazo na hata kutaka kumtenga.
Tena wanaona jinsi USA aktaka kuvamia nchi nyingine jinsi anavyoomba nchi nyingine zimsaidie (washirika) lakini zinaona jinsi anayopoga vita nchi zisimsaidie Urusi kwa chochote.
Sasa Hali hii inazikera nchi nyingi sana hapa duniani. Kwa Hali hiyo nchi zinazomchukia Urusi ni Chache sana ukilinganisha na jinsi USA anavyoeneza propaganda Zake.