Ukweli ni kwamba bodaboda ana fursa na anamzidi kipato Mwalimu

Unastaafu 2054, maana yake kwa sasa una miaka 29
Kwa miaka hiyo 32 iliyobakia utaingiza jumla ya Tsh 400,000
Hongera
 
Mtoa mada uliwahi kuwa mwalimu? Maana wawajua sana
 
Sio kweli mm Mara ya kwanza dar nilipanga mwananyamala mmliki ni bodaboda
Ndugu yangu Mwananyamala viwanja viliisha miaka ya 70-80. Ukimwona mtu ana nyumba huko ujue ni mzee au amenunua hivi karibuni .
Na kununua kiwanja nyumba Mwananyamala kwasasa at least uwe na 40 million.
Sema huyo mtu alikuwa na pesa zake sasa maisha yamempiga kawa bodaboda. Au ni nyumba ya urithi.
Ikumbukwe kazi ya bodaboda imekuja miaka hii.
 
Mtoa mada ana bifu na walimu....
Walimfanyaje sijui

Ila kwamba boda anatunza hadi 50K kwa siku hiyo ni uongo, ila yawezekana kwa wachache mno 1/1000
Sana sana wabeba magendo, wavusha wahamiaji haramu,
 
Naona unateseka sana[emoji3][emoji3]
 
Ila bado 1.2m haitoshi
 
Bodaboda karibu kila siku ninapanda. Na ninayajua maisha yao.
Bodaboda ni kazi ya mwisho Tanzania.
Haina chochote.
Ni kazi za ma looser.
Acha kusikiliza story za kijiweni.
Boda boda wamejazana kila sehemu, wanalogana hatari.

Kuna mmoja alikuwa analalamika kuwa hapati abiria, ila wenzake wanabeba hadi mara 4 wenyewe hawajabeba hata 1
 
Boda boda wamejazana kila sehemu, wanalogana hatari.

Kuna mmoja alikuwa analalamika kuwa hapati abiria, ila wenzake wanabeba hadi mara 4 wenyewe hawajabeba hata 1
Kuna kijiwe juzi niliwakuta wanapanga njama za kumfukuza bodaboda mwenzao eti kisa anawaibia kwa chuma ulete
 
Hao boda boda asilimia 69% wanaendesha bodaboda za waalimu
 
Kuna anko mmoja alinunua boxa karibu miaka mitano sasa hivi, kila siku yeye hana hela za kufanya matengenezo ya chombo chake, ukimuuliza mbona boda boda wengine wamejenga na nyumba kwa kazi hii hii, anadai hayo ni meneno ya vijiweni, hela inayopatikana kwenye boda boda inaishia kwenye matumizi ya kila siku.
 
Mbagara boda boda unapanda kwa 500 ni wengi kuliko abiria
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…