Ukweli ni kwamba bodaboda ana fursa na anamzidi kipato Mwalimu

Ukweli ni kwamba bodaboda ana fursa na anamzidi kipato Mwalimu

Nazungumzia net take home 60K kwa siku.
Sio hiyo 60K uanze kutoa pesa ya mafuta nk.
Namaanisha faida ya 60K baada ya kutoa gharama zote za uendeshaji wa hiyo bodaboda.
Vijana mna kwama wapi kuelewa vitu vidogo kama hivi?
Namaanisha ukitoa kila kitu unabaki na elfu sitini bodaboda anapata hiyo pesa
 
Ni kwa sababu hujui maana ya fedha. Ya boda haina sifa ya kuitwa fedha. Ina sifa ya kuitwa hela. Lakini mshahara unakuwa na sifa ya fedha, pesa na hela kulingana na nyakati.
Watu wengi mnapenda pesa ikiwa katika hali ya karatasi hii tunayoiona. Na ndicho watu wengi huhesabu. Lakini hatuhesabu(we do not account) the unseen value of money. We count and account cash.
Mshahara una thamani isiyoonekana.
Hilo ni moja.
La pili: Kwa mtu yeyote yule, la muhimu ni unagawanyaje kipato chako baada ya kupata. Issue kubwa sio kiasi ukichopata. Issue ni unatumiaje akili yako kuongoza ulichokipata. Hapo ndio kuna complex algebraic equations.
Hhhahaha mkuu acha mbwembwe
 
Hivi vichwa ndugu zangu tuvitumie kufikiri zaidi. Mwalimu ana uwezo wa kwenda bank kukopa pesa na kumiliki bodaboda tano ambazo zitamletea salio kila siku. Kwa maana nyingine anasimama kama meneja huku akiendelea na ajira yake. Unaanza kumlinganisha na mwendesha bodaboda?
Ona walimu wanawaza madeni tu dah [emoji28][emoji28][emoji28]
 
Kwani kipato sindopesa, manake maisha yake mazuri
Hapana kipato na ubora wa maisha ni vitu viwili tofauti na ndio maana tunashuhudia walimu wakimiliki nyumba nzuri, magari mazuri na wanasomesha watoto shule nzuri Kila siku na wakiugua wanatibiwa hospital nzuri na ndio kundi kubwa ambalo watoto zao ndio hawa bodaboda, mawakili, mameneja ofisi kubwa kubwa nk

Ila bodaboda tunashuhudia wakisifiwa tu humu Mitaandaoni ila 1.Wanaisha gheto
2. Asilimia 80% hawana familia
3. Ukienda MOI au bugando au KCMC wakidaiwa bill za matibabu hospital baada ya kupata ajari nakushindwa kulipa

4. Wanazaa ovyo ovyo na kutelekeza watoto

Angalia Sasa ubora upo wapi hapo kipato au jinsi unavyoishi
 
Mbona mgumu kuelewa, madeni sio mazuri. Akikopa anakuwa fukara wa kutupwa mshahara chini ya moja ya Tatu unaishi maisha magumu kama shoe shine

Kabisa mkuu sio million mbili. Million moja tu Kwa mwalimu shida ndio mana kwenye benki mshahara ukitoka tu nivurugu tupu hewa inakuwa nzito pananuka wamebanana na masulupwete Yao kama malofa
Punguza wivu walimu wataku**** mbea mwanao shauri yako wewe wachezee tu
 
Tuseme ukweli either muongezewe mishahara na stahiki nyingine lakini mwalimu unachomshinda Bodaboda ni uwezo wa kukopa tena uwe unakopesheka sasa, mwalimu kumaliza mwaka ana balance ya milioni mbili huyo anatakiwa heshima
Na huo ndio ukweli walimu wengi Ila sio wote tunaishi nao...wanamaisha ya chini Sana ... Yaani si kazi ya kulinga nayo...Mimi Sina Elimu kubwa likin sitamani kua mwalimu....

Sijajua tatizo Ni Nini Ila wengi wao amebweteka na mishahara ...
Hicho ndicho kinawa cost wlimu wengi.
 
Yawezekana lakini hebu ngoja....

Mwalimu anafanya kazi masaa 7 kwa siku tano kwa wiki.... Boda akifanya kazi kwa masaa hayo hapindui

Mwalimu ana likizo ya mwaka.... Boda akienda likizo kaumia

Mwalimu akiugua mshahara uko palepale.... Boda akiugua kaumia

Mwalimu akipata dharura bado mpunga unaingia.....

Na kikubwa zaidi, mwalimu anaweza kumiliki na kuendesha bodaboda akitaka lakini boda hawezi kuwa mwalimu

Haya nayo mkayatazame

Au nasema uongo ndugu zangu?
Mjadala wa vijana wa mwaka wa kwanza chuo huu tena ajabu wananzisha mijadala uku waliowasomesha ni wajomba zao ambao ni walimu, mama yake na kalia nyumbani wajomba ni walimu wamemlea kafika chuo anaosma kozi tofauti na uwalimu anaanza dharau walimu wakati kula yake nk imesimaamiwa na mwalimu
 
Kwa macho yangu nikiwa mwanafunzi nilishuhudia walimu wakizichapa ofisini sababu ya chai...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mimi nilishuhudia mwalimu akiuza barafu.....nilikuuliza maswali mengi Sana hdi Leo sijawahi pata jibu Tena mwalimu wa secondary...

Siku moja nilimfata na kumuuliza Alikua n mama flani wamakamo....

Hakunijibu kitu Zaid ya kusema we acha tu kijana

Walimu weng kinacho wa cost Ni kuish kwa kutegemea mishahara tu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Mimi nilishuhudia mwalimu akiuza barafu.....nilikuuliza maswali mengi Sana hdi Leo sijawahi pata jibu Tena mwalimu wa secondary...

Siku moja nilimfata na kumuuliza Alikua n mama flani wamakamo....

Hakunijibu kitu Zaid ya kusema we acha tu kijana

Walimu weng kinacho wa cost Ni kuish kwa kutegemea mishahara tu.
Kwahiyo bakhresa anaeuza ice cream za jero jero nae hali ni tete?
 
Bodaboda kupata 50000 kwa siku inawezekana sana lakini kinachowaponza hawana nidhamu ya pesa kabisa. Bodaboda wengi ni vijana hawawazi kusave sababu anajua kesho atatafuta na atapata tena hivyo pesa yao inaishia kwenye pombe, kamari/madubwi ( hapa asilimia 80 ya hela inaishia), bangi na kuhonga wanawake.

Bodaboda hawana uchungu na hela kabisa yeye kumpeleka mwanamke bure asidai hata 100 ni kawaida badi hajalipia guest na kumlisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
Unaongea kiwepesi sana unaijua 50000 wewe?
 
Kuna mjadala unawaka Moto kwenye jukwaa la MMU kuwa Kati ya mwalimu na bodaboda yupi yupo kwenye sehemu nzuri ya kipato na kuendesha maisha yake ya kila siku.

Iko hivi :bodaboda akitulia vizuri na akajenga uamini Kwa wateja Kwa siku hakosa elfu hamsini mpaka sitini ukipiga Kwa mwezi ni mara tano ya mshahara WA mwalimu anaelipwa laki nne au 5 Kwa mwezi. Hata hivyo bodaboda pesa Yao Ina-vary ila Hawa maticha ipo fixed mpaka miaka mitano au sita atakapopanda daraja [emoji28][emoji28][emoji28][emoji28].

Nafunga mjadara sasa. Mwalimu ni kada ya mwisho kwenye kipato hata muuza magazeti anampita
Acha Ujinga Basi umesahau kuwa hizo Bodaboda 80% Wamiliki ni Walimu ambao wanawapa Mkataba hiyo Ajira hao Bodaboda
 
Ukiona biashara yoyote inafanywa na watu wengi bai jua biashara hiyo inaleta pesa na faida ya haraka.
Fact:Bodaboda ni kama biashara zingine za road.....yaani ukitoka tuu wewe ni helaa. Kama wale yangeyange.😊
Biashara hii ina hela na inalipa saana tatizo liko kwa wanaoifanya.
Wengi hawana elimu ya shule,hawana elimu ya maisha,hawajawahi kushika pesa hivyo hupagawa kushika pesa za ghafla.
Hawajawahi kumiliki mademu wakali (tatizo kubwa liko hapa),atapakia bure,chips atamnunulia na pesa atampa na lodge atalipia plus muda alopoteza palee aaarrrgghhh!!!!
Wengi wao ni washamba,hawajapitia vyuoni hivyo kuna bata hawajazila so wako kwenye mshangao wa bata.
Wana matumizi yasiyo na mpangilio coz anajua akiingia road tuu mkwanja huo.
Ni bodaboda wachache saana wanaojielewa na ndo wanao make things happen.
Nimeifanya hii biashara kwa kuendesha road mwenyewe. Wanawake ndio wateja wakubwa wa hii biashara na ndo wauaji wakubwa wa hii biashara.
 
Back
Top Bottom