Serikali ianzishe utaratibu wa kujenga machinga complexes za kutosha kila mwaka ili kukabili kundi la watanzania wanaomaliza masomo kwenye hatua za awali na wengine wanaoendelea kujitafuta.
Hata hivyo serikali iwe inafuatilia mgawanyo wa vizimba vya biashara kwenye masoko, maana baadhi ya maeneo wasimamizi wanajigawia wenyewe vizimba na kuvikodisha kwa pesa isiyo rafiki.