Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Yule tunashampa angalizo, kama akiendelea kutuhadaa ajue 2025 ataangukia kidevu.Vipi kuhusu lile tapeli la salasala gwaji boy
Ulimaanisha nini hapa mkuu?Mpaka wa mkuu wa mkoa utazani kitimoto kinacho zurura barabarani
Labda huwa anachagua baadhi ya maeneo hasa kwa kuangalia yale maeneo yenye wakubwa wengi, ili wasije kumshtaki kwa aliemteua na matokeo yake kitumbua chake kiingie mchanga.Wasalaam Mkuu,
Binafsi naona post yako imejaa majungu. Mimi kama mkazi wa Kinondoni nampongeza sana Mkuu wa Wilaya Mh. Saad kwa namna anavyoongoza. Tangu amehamia hapa ame-perfom vizuri sana tena bila mbwembwe tofauti na watangulizi wake.
Mh. Saad amejitengea siku ya Alhamisi kusikiliza kero mbalimbali hususani migogoro ya Ardhi na kuzitatua hapohapo. Ni kiongozi mwenye hofu na Mungu ni ngumu kuingilika kifisadi. Mungu mbariki Mh. Saad, Mungu wabariki wakazi wa Kinondoni.
Mimi sina chama mkuu.Rudisha kadi!
Unaunga mkono kivipi?Naunga mkono ulichoandika mkuu.
Mkuu huyo DC anaitwa mh Saad Mtambule.Anaitwa nani?nasoma uzi sioni jina
hivi wewe kunguni una akili kweli? Umesema ni Wilaya yenye maendeleo na ina matajiri na viongozi wengi kuliko Wilaya zote nchini.Habari zenu wanaJF wenzangu,
Wakubwa leo sina mengi ya kuelezea, ila ukweli ni kwamba mkuu wa wilaya yetu ya Kinondoni aliepo ofisini sasa hafai hata robo kuongoza wilaya yetu.
Kila mtu anafahamu kwamba wilaya ya Kinondoni ndio wilaya inayoongoza kuwa na wasomi wengi nchini, ndio wilaya inayoishi viongozi wengi nchini, ndio wilaya inayoongoza kuwa na matajiri wengi nchini na ndio wilaya iliyoendelea kimakazi kuliko wilaya yoyote ile nchini.
Hivyo nilitarajia kutokana na sifa hizo nilizotaja hapo juu, pengine serikali ingekuletea kiongozi au mkuu wa wilaya ambae atakuwa na elimu pamoja na ujuzi wa ku deal na watu wenye sifa nilizozitaja hapo juu, na badala yake naona tumeletewa mtu ambae ni kama vile hajui ni nini alichotakiwa au anachotakiwa kukifanya katika wilaya hii.
Maeneo mengi ambayo yanatakiwa kupatiwa ufumbuzi yeye hana maono wala muda nayo, hashirikiani na mamlaka kubwa za serikali kutatua kero za sisi anaotuongoza kama vile kupigania na kusimamia miundo mbinu ya ujenzi wa barabara mbali mbali ambazo zinatakiwa kujengwa, utatuaji wa migogoro ya ardhi, changamoto za usafiri katika maeneo ambayo hayafikiki, upatikanaji wa maji nk.
Najua kuna watu watasema kwamba ooh toka lini mkuu wa wilaya akajenga barabara, lkn ukweli ni kwamba juhudi zake na uambanaji wake vinaweza kubusti na kuchangia ujengaji huo.
Yani jamaa anashindwa kupambania wilaya yake hata na wakuu wa wilaya wenzake kina DC Komba (Ubungo) , DC Matinyi (Temeke) , DC Bulembo (Kigamboni) nk ambao kila siku hukutana na wananchi wao kwa ajili ya kuwasikiliza kero zao na baadae kuangalia njia ya kuzitatua kero hizo.
Yeyote ambae yupo karibu na DC huyo hapa JF, naomba amfikishie ujumbe na kumwambia mh DC ajitafakari vizuri kama yeye kwa elimu yake na uwezo wake anao uwezo wa kweli wa kuongoza wilaya yetu, au ameamua tu kukaa ofisini kutafuna kodi za wavuja jasho bila tija yoyote.
Bora DC Godwin Gondwe alijitahidi kushirikiana na wananchi kwa namna moja au nyingine, lkn huyu wa sasa hamna kitu na ni kama vile kaletwa mahala asipopajua au kupapenda.
Wana Kinondoni safari hii tumeamua kuwa kitu kimoja katika kufuatilia na kusimamia maendeleo yetu. Kamwe hatutokubali kuona vichelema mbali mbali vinaletwa katika wilaya zetu kuja tu kupiga picha na kukaa ofisini kusubiri mshahara wa mwezi bila kupigania maendeleo yetu na haki zetu.
Asanteni wakuu.
Sababu si jamaa ashazieleza hapo juu au unataka sababu zipi tena?Unaunga mkono kivipi?
Ebu toa sababu.
saad mtambuleAnaitwa nani?nasoma uzi sioni jina
Sisi chama chetu kilikuwa kinapokea mamilioni ya ruzuku toka 2005 hadi 2020, jumlisha makato ya wabunge kila mwezi, hapo sijaweka milioni 100 za Sabodo alizotoa zijenge ofisi kuu ya chama, lkn zote zimetafunwa na mwenyekiti akishirikiana na genge lake. Mbona hatulalamiki?
??Mimi sina chama mkuu.
Ok mkuu.Sababu si jamaa ashazieleza hapo juu au unataka sababu zipi tena?
Mwandishi mzuri wa umbea kama huu unatakiwa utupe jina kamili la muhusika na historia yake fupi,halafu ndio utuletee fact za anavyofeli utendaji Kwa Sasa.
Jina hilo hapo mkuu.saad mtambule