Ukweli ni kwamba, mkuu wa wilaya ya Kinondoni hafiti kabisa kuongoza wilaya yetu

Ukweli ni kwamba, mkuu wa wilaya ya Kinondoni hafiti kabisa kuongoza wilaya yetu

Huyu DC alikua DED Arusha DC baadae akateuliwa DC NJOMBE halafu akaletwa Kinondoni. Kiukweli uwezo wake ni mdogo sana hana command ya DC. Afadhali awe DAS tuuu.
Huu ulioandika hapa ndio ukweli wenyewe. Ubarikiwe mkuu kwa kuliona hilo.
 
Naunga mkono ulichoandika mkuu.

Hivi karibuni mkuu wa wilaya ya Kinondoni baada ya malalamiko ya muda merfu aliamuru wavamizi wa maeneo ya wazi zikiwemo barabara huko Mbezi Beach "B" waondoke sehemu hizo kwa muda wa siku !4 alizowapa. Siku hizo alizowapa zimekwisha na wamekaidi agizo hilo na kumleta mganga wa kienyeji toka Mtwara kuja kuwafanyaia zindiko wasiondolewe!!!
Mkuu wa wilaya aelewe kuwa kama agizo lake halitatekelezwa la kuwaondoa wavamizi hawa itakuwa dosari kubwa sana kwa serikali kwani uvamizi wa maeneo huku MBezi Beach kando kando ya mto Dumbwi utashamiri zaidi na kuharibu mazingira. Sio hivyo tu, hawa wavamizi wataamini kuwa ushikina wao unaweza kuithibiti serikali jambo ambulo ni hatari sana kwa maendeleo ya nchi.
Tuanajua kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa uko karibu na wanasiasa wanatumia uvunjifu wa sheria kutaka kujipendekeza kwa wananchi na moja ya njia wanazotumia ni kuwaruhusu watu wajenge maeneo yasiyoruhusiwa. Mkuu wa wilaya lazima ajue kuwa matatizo yote ya uvamizi na ujenzi holela ambao baadae unaleta matatizo huchagizwa na viongozi wa serikali za mitaa. Itakuwa busara kama Mkuu wa wilaya atalinda heshima yake kwa kusimamia uutekelezaji wa agio lake huko Mbezi Beach ili liwe fundisho/ precedent kwa wavamizi wengaine. Kutofanya hivyo ni kuahirisha tatizo ambalo huko mbele litakuwa kubwa zaidi.
DC simamia maamuzi yako otherwise you will give fodder to your detractors.
 
Kati ya teuzi bora kabisa za Mheshimiwa Rais ni huyu Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni ni Mtu makini,Msikivu na anajua kuishi na Kila mtu yuko Vizuri sana yaani kwa lugha ya Ndg yetu humu jukwaani Pascal Mayalla anasema yuko Humble down to Earth.!
Kinondoni ni wilaya ngumu kuiongoza kwani madiwani wake wanajihusisha na biashara haramu ya madawa ya kulevya! Sio SirI kuwa biashara hiyo inachangia uvamizi wa maeneo kando ya barabara na kando ya mto Ndumbwi huko KAWE!
Mkuu wa wilaya hana budi kuwa thabiti katika kusimamia maamuzi yanayolinda sheria na heshima ya serikali.
 
Wewe itakuwa CCM tena wale wanaojifanya bila wao.. mambo hayaendi.... Akija mtumishi yeyote wa serikali mnajifanya kumwambia eti "tusikilize sisi utakaa sana hapa" mkibanwa kwenye mbavu mnaanza kutafuta huruma kwenye mitandao ya kijamii... Fanyeni Kazi bana... Achane hizo bana mtawarithisha watoto wenu domo au?

NB: huko china au japani, wanawafundisha watoto wao kilimo, ujenzi, nidhamu, kupenda Kazi na ubunifu... Nyie mmekaza na umbea tu...
Nimeandika hii baada ya kusoma huo umbea wako... Maana imeniuma sana kwakuwa naelewa kinacho endelea....
Mkuu wa wilaya ya Kinondoni ameipa heshima serikali kwa kufuata sheria na kuvunja mabanda ya wavamizi wa barabara kule Mbezi beach B!
Amewaonesha kuwa serikali Haitishwi na Imani za kishirikina katika kutekeleza majukumu yake!
Tunaomba aendelee kusafisha sehemu zingine ambako kuna uvunjaji wa sheria na hasa kuhusu uchafuzi wa Mazingira!
 
Daah kweli nimeamini kuna chuki binafsi na usiamini mambo ya mtandaoni. Utendaji kazi wa huyu DC hauhitaji kumulikwa kwa tochi au kupimwa na darubini. Itisha mkutano wa hadhara kila kata tupate public opinion juu ya huyu DC nina uhakika atapata zaidi ya 95%

Ni msikivu, mnyenyekevu, hana kujikweza kama wengine. Kuna mgogoro mkubwa sana wa taasisi ya dini moja ambao umedumu miaka 12 ameweza kuutatua bila hata kujitangaza au kupiga picha na viongozi wa pande zote mbili kuashiria kumalizika kwa mgogoro kama ambavyo wengine wangefanya.
 
Back
Top Bottom